Kuna ombwe juu ya chanzo chetu na ulimwengu!

Evolution mpaka leo hii ni nadharia (Theory) tu,.... Laws of physics zinaelezea tu jinsi ulimwengu unavyo operate,. so swali linabaki palepale kwamba Je, ujuzi ulitumika ili kuweza kuunda mifumo mbalimbali tuliyoikuta ulimwenguni,?

Yaani kwamba mifumo imetokea tu without any reasoning Intelligence? kwa mfano mfumo wa mvua kunyesha na kurutubisha ardhi ili kufanya mimea iweze kuota na uhai wa viumbe mbalimbali uweze kuendelea,.. kwamba hii imetokea without any reasoning and intelligence?,.. au tazama mfumo wa kuzaliana kwenye viumbe mbalimbali ukiangalia unaona kabisa ni programmed na logically arranged,... Je, ujuzi haujatumika?
Watu ni vyepesi kuamini kwamba tupo kwenye simulation kuliko kuamini uwepo wa mungu, Elon musk alishawahi kukili kwamba kuna chance kubwa sana ya ulimwengu wetu kuwa kwenye simulation tena sio base simulation, Neil degrase tyson kasema odds ya ulimwengu wetu kuwa kwenye simulation ni 50/50, hivyo kama kuna uwezakano wa kuwa kwenye simulation basi kuna intelligence inayohusika na kutengeneza ile simulation, watasema labda ni advance cillivization au powerful quantum computer ila ukiingiza tu neno Mungu mjadala unaanza
 
Hichi ndicho nilichosema hapo nyuma kuwa binadamu akifahamu namna ya kudhibiti kifo mambo mengi yatagundulika. Imagine wewe, Mtanzania ambaye hujafanya ugunduzi wowote unayo hii curioisty, vipi kwa zile big brains zilizogundua kuwa dunia ni duara na kuna space? Leo zingekuwa na mtazamo upi iwapo zingekuwa hai?
Kwamba kuna big brains waligundua Dunia ni duara?,.. kabla ya kugundua walijua ina umbo gani?😅
 
Watu ni vyepesi kuamini kwamba tupo kwenye simulation kuliko kuamini uwepo wa mungu, Elon musk alishawahi kukili kwamba kuna chance kubwa sana ya ulimwengu wetu kuwa kwenye simulation tena sio base simulation, Neil degrase tyson kasema odds ya ulimwengu wetu kuwa kwenye simulation ni 50/50, hivyo kama kuna uwezakano wa kuwa kwenye simulation basi kuna intelligence inayohusika na kutengeneza ile simulation, watasema labda ni advance cillivization au powerful quantum computer ila ukiingiza tu neno Mungu mjadala unaanza
Shida kuu ni sifa za Mungu mkuu ndo mgogofo unapoanza
 
Watu ni vyepesi kuamini kwamba tupo kwenye simulation kuliko kuamini uwepo wa mungu, Elon musk alishawahi kukili kwamba kuna chance kubwa sana ya ulimwengu wetu kuwa kwenye simulation tena sio base simulation, Neil degrase tyson kasema odds ya ulimwengu wetu kuwa kwenye simulation ni 50/50, hivyo kama kuna uwezakano wa kuwa kwenye simulation basi kuna intelligence inayohusika na kutengeneza ile simulation, watasema labda ni advance cillivization au powerful quantum computer ila ukiingiza tu neno Mungu mjadala unaanza
Hahh upo sahihi ukitaja kwamba hiyo wanayoita intelligence ndiyo Mungu hawataki kukubali(Wakati kimsingi Mungu ni Jina tu unaweza ukaita vyovyote utakavyo ili mradi unamaanisha the Intelligence behind mifumo mbalimbali ya ulimwengu),...na sababu kubwa ya kupinga ni kwamba Binadamu tumepewa akili ambazo kuna namna zinafanya tujiona wakubwa sana hatutaki kuwa down to anyone,.... yaani asiwepo mkubwa mwenye uwezo kuliko sisi sio Mungu wala the so called alien yoyote,... binadamu tunatamani tuujue ulimwengu wote na tuweze ku control kila kitu Jua, Mwezi, bahari, space na ulimwengu kwa ujumla yaani tunataka kwa atleast mifumo yote ya ulimwengu iwe imetengenezwa na powerful quantum computer ambayo sisi binadamu tunaweza kui manipulate na kuiongoza tunavyotaka.

Ila kimsingi kwenye viumbe binadamu tumependelewa uwezo wa kufikiri,... so ukiangalia Binadamu ni kama tumepewa uwezo wa kuwaongoza viumbe wengine kwenye dunia tukiamua tuweke mazingira vizuri tunaweza na tukiamua tuue viumbe wengi/wote tubaki sisi tu tunaweza na kufanya mabalaa yote,... I mean tuna uwezo wa kuweka mambo sawa na kuharibu na kiburi chetu kinaanzia hapo.
 
Mimi ni yule wa dunia duara inayozunguka,.. ila ukiniomba uthibitisho kwa kweli sina ngoja tuendelee na tafiti.
Oh, basi nimekufananisha. Ni hivi, kuna mtu huwa anasema dunia ni kama sahani. Sasa sisi binadamu huwa za kuambiwa tunachanganya na zetu, hata kama hakuna ushahidi usio na shaka kuwa dunia ni duara ila ushahidi uliopo ukiulinganisha na ushahidi wa kwamba dunia ni kama sahani kisha ukachanganya na zako, utajua pa kuegemea. Ila Kama ulivyosema, tuendelee na kusubiri tafiti labda kuna jingine litaibuka. Ila kwa sasa kusema dunia ni kama sahani kwangu mimi hapana.
 
Hilo neno "duara" ndo lina wachanganya

hateeb10 ni team flat earth,
 
Evolution mpaka leo hii ni nadharia (Theory) tu,.... Laws of physics zinaelezea tu jinsi ulimwengu unavyo operate,. so swali linabaki palepale kwamba Je, ujuzi ulitumika ili kuweza kuunda mifumo mbalimbali tuliyoikuta ulimwenguni,?

Yaani kwamba mifumo imetokea tu without any reasoning Intelligence? kwa mfano mfumo wa mvua kunyesha na kurutubisha ardhi ili kufanya mimea iweze kuota na uhai wa viumbe mbalimbali uweze kuendelea,.. kwamba hii imetokea without any reasoning and intelligence?,.. au tazama mfumo wa kuzaliana kwenye viumbe mbalimbali ukiangalia unaona kabisa ni programmed na logically arranged,... Je, ujuzi haujatumika?
Kwani eveolution kuwa theory tatitizo ni nini? Mbona General Relativity ni theory?
 
We umetumia neno duara, hata sahani ni duara 🤣, ila ungetaja tufe hapo mngeelewana , ngoja mwenyewe atajibu
Ooh, hahahaha. Dah, lugha hizi. Nimewaza labda ningesema dunia ni kama chapati ila nayo ni duara. Inamaana tufe si duara?
 
🤣 nyingi tu mkuu, we wasikilize atheist in their perspective utanielewa
Niliona unajadiliana na mtu kuhusu Huruma,.. kwamba kwanini matatizo yapo ikiwa Mungu ana huruma?

Mimi naona tunashindwa kuelewa kwasababu hatutaki kusoma na ku push akili zetu kuelewa zaidi,.... ngoja nijaribu kuelezea kama utanielewa:

Kwa mfano ishu ya huruma & kwanini mabaya yanatokea wakati Mungu ana huruma,.... Mfano kwenye Qur'an kuna aya inasema "....Mungu habadilishi hali za Jamii/watu husika mpaka wao watakapoamua kubadilika......" sasa hapa tumepewa nyenzo kubwa ambayo ni "Akili" kupitia akili ndiyo utajua kwamba Mungu ametuhurumia sana.,, akili inatufanya tujue kipi kina madhara tuepuke na kipi kina faida tukifanye,.. ukiangalia kuna mateso mengi binadamu tunapitia kutokana na jinsi sisi wenyewe tulivyoamua kuendesha maisha yetu,. tukiamua kubadilisha tabia zetu tukaishi kwa kuthaminiana na kujaliana kwenye hali tofauti regardless ya rangi wala mitazamo asilimia kubwa ya mateso hayatokuepo,..

Lakini pia kwenye kusoma kuhusu Mungu anavyofanya huruma zake kuna sehem anasema...." Wala usidhani Mwenyezi Mungu amepuuzia wanayoyatenda madhalimu. Anawaakhirishia tu mpaka siku ambayo macho yatakodoka yakibaki yametazama kwa kutetemeka.”

Hiyo inajibu kwamba Kuna mambo Mungu anayaachia yatokee haijalishi sisi tutayaona ni mabaya kiasi gani, Yeye ameshayapangia muda wa kuyahukumia,.....

Pia miongoni mwa changamoto ninayoiona kwa atheist ni mtazamo wao juu ya kifo& uhai,.. atheist wengi wanaona Uhai ni kitu bora na kifo ni kitu kibaya au kuangamia, (Sasa huo mtazamo kwa uelewa wangu sio sahihi,.. What if kwa Mungu uhai na kifo ni vitu vya kawaida sana kwake? huenda sisi tunathamini uhai kwakuwa hatujui kuna nini nyuma ya kifo,. what if kifo ni utulivu usio na purukushani za uhai... kuna uwezekano ukijua yaliyo nyuma ya kifo ukabadili mtazamo).

Nimejaribu kufafanua sikulazimishi kukubaliana na mimi ila nadhani kuna concept umepata..., kama kuna sehem hujaelewa unaweza kuuliza.
 
Kwani eveolution kuwa theory tatitizo ni nini? Mbona General Relativity ni theory?
Ukishaambiwa theory maana yake ni kitu cha kusadikika hakuna uthibitisho 100%,.. kitu hakiwezi kuwa theory 100% na fact 100% at the same time,...
 
Pia miongoni mwa changamoto ninayoiona kwa atheist ni mtazamo wao juu ya kifo& uhai,.. atheist wengi wanaona Uhai ni kitu bora na kifo ni kitu kibaya au kuangamia, (Sasa huo mtazamo kwa uelewa wangu sio sahihi,.. What if kwa Mungu uhai na kifo ni vitu vya kawaida sana kwake? huenda sisi tunathamini uhai kwakuwa hatujui kuna nini nyuma ya kifo,. what if kifo ni utulivu usio na purukushani za uhai... kuna uwezekano ukijua yaliyo nyuma ya kifo ukabadili mtazamo).
Au kama vile tuseme watoto wapo tumboni kwa mama yao wakiwa mule kwao hyo ndio dunia yao wanajua akishazaliwa ndio mwisho wa maisha yake ila kuzaliwa kwake ni mwanzo wa maisha mengine, wakiwa mule wanaweza kubishana na kuambiana hakuna aliyeenda kwenye huo ulimwengu na akarudi hivyo tutajuaje kama kweli kuzaliwa siyo mwisho wa maisha Lax
 
Alah! hateeb10 kumbe ndiye? Sasa mbona anajikataa tena?
Unajua ishu ipo kwenye kuthibitisha,.. mimi nikikuomba unipe uthibitisho kwamba dunia ni duara na inazunguka huwezi ukaleta au inawezekana?

Kabla big brains hawajagundua kwamba dunia ni duara,.. Jamii iliamini dunia ina umbo gani?,.. na Big brains ni uthibitisho gani walitoa kwa jamii juu ya ugunduzi huo? huenda kweli Dunia ni duara linalozunguka ila sidhani kama kuna uthibitisho ambao hata layman ukimuuliza atajibu kwa usahihi.
 
Au kama vile tuseme watoto wapo tumboni kwa mama yao wakiwa mule kwao hyo ndio dunia yao wanajua akishazaliwa ndio mwisho wa maisha yake ila kuzaliwa kwake ni mwanzo wa maisha mengine, wakiwa mule wanaweza kubishana na kuambiana hakuna aliyeenda kwenye huo ulimwengu na akarudi hivyo tutajuaje kama kweli kuzaliwa siyo mwisho wa maisha Lax
Well hapa umeiweka kitaalamu zaidi,..
 
Back
Top Bottom