Kuna ombwe juu ya chanzo chetu na ulimwengu!

Inaonekana umekata tamaa ya kufikiria zaidi,.. ila ombwe lipo na sababu ya ombwe kuwepo si athari ya Dini wala Sayansi bali ni akili zetu,... Akili zetu zinapenda kudadisi hakuna namna utaizuia akili ya binadamu kujiuliza maswali juu ya ulimwengu kwa ujumla,.. hata maendeleo ya kiteknolojia unayoyaona ni matokeo ya akili ya binadamu,.. Binadamu sio sawa na Panzi, Kuku na viumbe wengine kama ulivyosema.
Binadamu ni kiumbe mdadisi...... There's nothing wrong about it mkuu. Hata mimi nadadisi pia.

Na kwenye udadisi wetu tumevumbua vitu vingi sana vinavyo tusaidia kutimiza jukumu letu mama la kupambana kuishi kadiri tuwezavyo
 
Hahh kwahiyo Wewe na Panzi akili zenu zipo sawa,..? Hamna tofauti?😅

Binadamu ana uwezo mkubwa mno Binadamu tumeweza mpaka ku manipulate mifumo ya viumbe hai mpaka leo tuna Kuku wa maabara,. watoto wa maabara na mambo mengi makubwa,... Panzi anaweza??

Dah hivi Jamii forum si ni home of Great Thinkers?
Mkuu usawa tunao uzungumzia sio usawa wa KIAKILI....... Ni mzunguko wa maisha.
Kila kiumbe ana upekee wake
 
Mkuu mimi ninacho maanisha ni kwamba wote tumejikuta tumezaliwa na kuikuta hii Dunia kwenye huu USTADI wa hali ya juu kabisa.
Na JUKUMU LETU MAMA ni kuhakikisha tunapambana tuishi ili tuzaliane kadri tutakavyoweza the same as Funza, Tumbili, Samaki, Nyoka, nk nk

Tofauti yetu kubwa na viumbe wengine ni kwamba sisi tupo more intelligent PENGINE kuliko viumbe wengine na ndio maana tunajipa UMAALUMU na tuna hangaika kutafuta MUUMBA na sababu za kutuumba jambo ambalo HALINA MAANA YOYOTE

Kula, kunywa, kupambana na changamoto zako zinazo hatarisha maisha yako HAKUNA maana yoyote zaidi ya hiyo........ Failed to do so u die
kama species pekee tulio na akili nyingi ni jukumu letu kuilinda nyumba tuliyopo na hatuwezi kuilinda kama hatujui imejengwaje na inafanya kazi vipi, je hii ni nyumba pekee vipi kama kuna nyingine ambayo tutaenda kama hii ikiharibika, je hii ni nyumba au gereza.
 
Hahh kwahiyo Wewe na Panzi akili zenu zipo sawa,..? Hamna tofauti?😅

Binadamu ana uwezo mkubwa mno Binadamu tumeweza mpaka ku manipulate mifumo ya viumbe hai mpaka leo tuna Kuku wa maabara,. watoto wa maabara na mambo mengi makubwa,... Panzi anaweza??

Dah hivi Jamii forum si ni home of Great Thinkers?
Huo uwezo mkubwa ndiyo mbwembwe zenyewe mkuu 🤣🤣🤣 Mwisho wa siku unakufa kama wanavyokufa panzi 🤣🤣
 
Mkuu usawa tunao uzungumzia sio usawa wa KIAKILI....... Ni mzunguko wa maisha.
Kila kiumbe ana upekee wake
Sawa., Sasa mwanzo ulisema hakuna ombwe, lakini kimsingi kila binadamu (karibia wote) hujiuliza swali lilelile: ilikuwaje sisi na viumbe wengine tukawa hivi tulivyo? Na ulimwengu pamoja na sheria zake ziliwezaje kuwepo na kuanza kufanya kazi namna hii tulivyokuta? Hadi sasa, hilo ni ombwe, kwa sababu bado hakuna majibu ya moja kwa moja na yenye uthibitisho kamili kwamba kila kitu kilianza vipi.

Kwa hiyo, tunaposema kuna ombwe hatumaanishi binadamu tunajiona special kuliko viumbe wengine, bali tunazungumzia kiu ya kiasili ya udadisi kutaka kuelewa asili yetu, na kutaka kujua chanzo cha hizi sheria za ulimwengu na mifumo yake.
 
Huo uwezo mkubwa ndiyo mbwembwe zenyewe mkuu 🤣🤣🤣 Mwisho wa siku unakufa kama wanavyokufa panzi 🤣🤣
Hahh hivi unajua kama Binadamu washafanya majaribio mpaka ya dawa za kuzuia kifo(Yaani wapo binadamu wanaoamini kwamba kuna namna ukichezea mifumo unaweza ukaishi milele😅)?

simaanishi kwamba Binadamu tunaweza kuzuia kifo ila nakuonyesha kwamba Binadamu tuna uwezo mkubwa wa kufikiria kiasi ambacho hatuamini kwenye kutowezekana (Impossibilities),. akili ya Binadamu kuna muda inamuambia kila kitu kinawezekana......

NB: Jiulize kwanini Ndege wamepewa mbawa za kupaa lakini Binadamu hawajapewa Mbawa ila wamepewa akili ya kutengeneza vyombo vya usafiri wa anga,....
 
Mkuu uko sahihi!
Lakini mimi naona kama binadamu siyo kwamba tuna Akili au uwezo kuliko viumbe wengine 🤣🤣
Kila kiumbe ana Akili na uwezo kwenye 18 zake.
Kuna virus hawasikii dawa ambazo binadamu anazitengeneza, na kama ikitokea dawa inayowaingia hao virus basi hujitengenezea kinga dhindi ya hiyo dawa (hapo binadamu akae Tena maabara atoe dawa mpya, maana ya kwanza tayari haifanyi Tena kazi)
Yaani Kwa ufupi inapoishia Akili ya binadamu ndiyo Akili ya kirusi imeanzia hapo kwenda mbele

Sijui umeielewa mkuu au nimekuchanganya zaidi 🤣
 
kama species pekee tulio na akili nyingi ni jukumu letu kuilinda nyumba tuliyopo na hatuwezi kuilinda kama hatujui imejengwaje na inafanya kazi vipi, je hii ni nyumba pekee vipi kama kuna nyingine ambayo tutaenda kama hii ikiharibika, je hii ni nyumba au gereza.
Mkuu mimi nafikiri kiumbe MUHARIBIFU kuliko wote anayeongoza KUIHARIBU hii Dunia yetu ni sisi BINADAMU kwa sababu za kujipa huo UMAALUMU
 
hapo sikupingi nakubaliana na wewe ila pia kumbuka specie yetu ipo kwenye hatua changa za civilization sidhani kama tumefika hata miaka mil 2, bado tunagundua vitu ni kama mtoto mchanga atafanya hivi ila anajifunza mdogo mdogo hivyo huenda baada ya miaka 1000 ijayo tutakuwa tushakomaa na uharibifu utapungua
 
Sawa., Sasa mwanzo ulisema hakuna ombwe, lakini kimsingi kila binadamu (karibia wote) hujiuliza swali lilelile: ilikuwaje sisi na viumbe wengine tukawa hivi tulivyo? Na ulimwengu pamoja na sheria zake ziliwezaje kuwepo na kuanza kufanya kazi namna hii tulivyokuta? Hadi sasa, hilo ni ombwe, kwa sababu bado hakuna majibu ya moja kwa moja na yenye uthibitisho kamili kwamba kila kitu kilianza vipi.

Kwa hiyo, tunaposema kuna ombwe hatumaanishi binadamu tunajiona special kuliko viumbe wengine, bali tunazungumzia kiu ya kiasili ya udadisi kutaka kuelewa asili yetu, na kutaka kujua chanzo cha hizi sheria za ulimwengu na mifumo yake.
Msingi wa kwanza wa KIUMBE chochote kile ni kupambana kuishi kulingana na "sheria za Dunia tulizo zikuta" kadiri awezavyo ili azaliane....... Hayo mambo ya kutaka kujua Dunia ilianzaje ni MBWEMBWE tu na sio OMBWE

Ikiwa litatokea jambo la kutishia existence yetu hapa Duniani hilo tutaitwa OMBWE

Mkuu kwa sehemu kubwa Binadamu tunajipa huo u special kwa "kuamini" kuna aliyetuumba ili TUITAWALE Dunia na blah blah kibao za life after death
Kwa bahati mbaya sana mfumo wa maisha yetu sasa una LAZIMISHA toka utotoni mtu kuwa Brainwashed kwamba kuna MUNGU muumba wa vyote na ametuumba kwa sababu maalumu na katupa MUONGOZO

Hata ukikua na kuja kubaini ni UONGO kuhusu Mungu bado zile athari zinabakia kwenye namna yetu ya kufikiri linapokuja swala la kudadisi kuhusu "mwanzo" wa dunia........ Kama sio MUNGU ni nani sasa KAUMBA? Hili swali ni matokeo ya athari za mwanzo kuhusu tulivyo aminishwa kuna Mungu
 
Mkuu mimi nafikiri kiumbe MUHARIBIFU kuliko wote anayeongoza KUIHARIBU hii Dunia yetu ni sisi BINADAMU kwa sababu za kujipa huo UMAALUMU
Hatujipi umuhimu bali sisi ni muhimu,... Jiulize kwanini tuharibu sisi na sio viumbe wengine? kwanini Binadamu ndiyo tunafanya maendeleo makubwa na sio viumbe wengine? akili zetu zina uwezo mkubwa sana na hii si kujipa umuhimu bali ndiyo uhalisia.
 
hapo sikupingi nakubaliana na wewe ila pia kumbuka specie yetu ipo kwenye hatua changa za civilization sidhani kama tumefika hata miaka mil 2, bado tunagundua vitu ni kama mtoto mchanga atafanya hivi ila anajifunza mdogo mdogo hivyo huenda baada ya miaka 1000 ijayo tutakuwa tushakomaa na uharibifu utapungua
Hili linawezekana mkuu.
Lakini mimi naona kadiri tunavyokwenda hali inazidi kuwa mbaya zaidi

Tunaacha hata kutumia vitu vya asili na tunahamia zaidi kwenye artificial zaidi
Nahisi kama binadamu wajao watakua na maisha mafupi sana
 
Mimi nina mtizamo tofauti kidogo, Tunaposema kuwa nishati haikuumbwa SI KWELI TUNAKOSEA, Chakula ni kichocheo cha nishati, kuni zinachochea moto ili tupate nishati ILIYOKO NDANI YAKE.
Kwa ufupi mmea una nishati, mwanadamu ana nishati na Mungu ni nishati.
Ukiwa kama nishati unatetema, unatetema katika viwango tofautitofauti mfano 3D,4D na 5D Kutegemeana na mwili wako umepata kichocheo cha uwezo gani mfano: huzuni,furaha,hofu, Mapenzi, uhalisi n.k katika hizi nishati inayokupa mtetemo wa juu zaidi ni uhalisia(Authenticity) ukiwa katika uhalisia wako unakuwa na mtetemo wa hali ya juu sana.
Huyo Mungu ni nishati ipi?
Chanzo Cha nishati hapa duniani ni jua na chanzo Cha maisha hapa ulimwengu huu wa kwetu ni jua.
 
Msingi wa kwanza wa KIUMBE chochote kile ni kupambana kuishi kulingana na "sheria za Dunia tulizo zikuta" kadiri awezavyo ili azaliane....... Hayo mambo ya kutaka kujua Dunia ilianzaje ni MBWEMBWE tu na sio OMBWE

Ikiwa litatokea jambo la kutishia existence yetu hapa Duniani hilo tutaitwa OMBWE

Mkuu kwa sehemu kubwa Binadamu tunajipa huo u special kwa "kuamini" kuna aliyetuumba ili TUITAWALE Dunia na blah blah kibao za life after death
Kwa bahati mbaya sana mfumo wa maisha yetu sasa una LAZIMISHA toka utotoni mtu kuwa Brainwashed kwamba kuna MUNGU muumba wa vyote na ametuumba kwa sababu maalumu na katupa MUONGOZO

Hata ukikua na kuja kubaini ni UONGO kuhusu Mungu bado zile athari zinabakia kwenye namna yetu ya kufikiri linapokuja swala la kudadisi kuhusu "mwanzo" wa dunia........ Kama sio MUNGU ni nani sasa KAUMBA? Hili swali ni matokeo ya athari za mwanzo kuhusu tulivyo aminishwa kuna Mungu
Kwanini unasema Binadamu tunajipa u-special? Binadamu hatujipi u-special bali ndiyo tumeumbwa hivi tupo na akili kubwa kuliko viumbe wengine,..

Sisi tuna uwezo wa kuvifanya viumbe vingine vile tunataka,.. hata Dunia tukiamua kuiharibu tunaweza hiyo inatosha kukuonyesha jinsi gani Binadamu ni viumbe special wenye akili kubwa na hatari!

Just Imagine Binadamu ameweza kugundua Bunduki, atomic bombs na vitu vingi vya hatari,... kuna kiumbe kinaweza kunusurika iwapo Binadamu tutaamua kuharibu? Binadamu ndiyo viumbe ambao tunakaa vikao na mikutano mbalimbali kujadili jinsi ya kulinda uwepo wa viumbe wengine wasitoweke Duniani.....
 
Hili linawezekana mkuu.
Lakini mimi naona kadiri tunavyokwenda hali inazidi kuwa mbaya zaidi

Tunaacha hata kutumia vitu vya asili na tunahamia zaidi kwenye artificial zaidi
Nahisi kama binadamu wajao watakua na maisha mafupi sana
Miaka mingi iliyopita wakati binadamu yupo sawa na asili, maisha ya kuishi yalikuwa miaka 30 tu.

Miaka ijayo maisha yatakuwa marefu Hadi kufikia miaka 200
 
Kwanini unasema Binadamu tunajipa u-special? Binadamu hatujipi u-special bali ndiyo tumeumbwa hivi tupo na akili kubwa kuliko viumbe wengine,..

Sisi tuna uwezo wa kuvifanya viumbe vingine vile tunataka,.. hata Dunia tukiamua kuiharibu tunaweza hiyo inatosha kukuonyesha jinsi gani Binadamu ni viumbe special wenye akili kubwa na hatari!

Just Imagine Binadamu ameweza kugundua Bunduki, atomic bombs na vitu vingi vya hatari,... kuna kiumbe kinaweza kunusurika iwapo Binadamu tutaamua kuharibu? Binadamu ndiyo viumbe ambao tunakaa vikao na mikutano mbalimbali kujadili jinsi ya kulinda uwepo wa viumbe wengine wasitoweke Duniani.....
Ila sio special
Bado tunategemea nature kwenye vitu vingi.
Bado ni wanyama na primates Kama walivyo bonobo
 
Back
Top Bottom