Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,243
- 12,772
Pamoja na mgao wa umeme, kuna sehemu hazitakiwi kukatiwa kabisa. Nimemsikia GUSSIE anasema wasikate umeme Kariakoo. Ukweli ni kuwa Kariakoo ni moja ya maeneo yanayotakiwa kukatiwa kabisa umeme iwapo kuna mgao.
Kariakoo ni eneo ambalo dola za nchi hii zinaoenda kupotea. Ndiko hazina ya nchi hii inakoenda kutumika kuagiza vitu nje. Faida ya Kariakoo kiuchumi kwa nchi hii huwezi kuilinganisha na Miji kama Geita, Kahama au Chunya ambayo huzalisha dhahabu zinazoleta pesa za kigeni.
Hizi pesa za kigeni ndizo zinalipa mikopo na kununua mahitaji kama mafuta na madawa nje ya nchi. Hizi pesa za kigeni ndizo zinaenda Kariakoo kusaidia uagizaji wa vitu nje ya nchi. Kiuchumi, miji inayokuingizia pesa za kigeni hutakiwi kabisa kuikatia umeme, utajiongezea tatizo juu ya tatizo.
Miji au sehemu zinazozalisha kwa ajili ya export ni muhimu kiuchumi kuliko soko "mjinga" lolote nchini hapa. Miji ya watalii kama Arusha, Moshi, Karatu; miji ya madini kama Geita, Kahama, Chunya; sehemu zinazozalisha kuexport kama SEZ's nk hazitakiwi kabisa kukatiwa umeme.