Hivi yale makelele ya Mgao wa Umeme na Sukari kuadimika yameishia wapi?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,042
49,727
Chadema Kwa Sasa mtakuja na ajenda gani maana zile kelele za sukari na mgao wa umeme vimepotea ghafla 🤪🤪

View: https://www.instagram.com/reel/C4ODa8RtTt9/?igsh=MXFlNmkwZzA3ZGJ2dw==

----
Wakati makali ya mgao wa umeme na bei juu ya sukari vikianza kupungua kwa baadhi ya maeneo nchini, wachumi wameshauri njia za kupita ili hali hiyo izidi kuimarika na kuleta utulivu wa kiuchumi.

Mgao wa umeme nchini ulianza Septemba mwaka jana kwa kile kilichoelezwa ni kutokana na upungufu katika uzalishaji kwenye vyanzo mbalimbali ikiwemo vya maji.

Kutokana na tatizo hilo, Rais Samia Suluhu Hassan alitoa miezi sita kwa bosi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Gissima Nyamo-Hanga aliyekuwa amemteua wakati huo kushughulikia mgao wa umeme na kuumaliza.

Katikakati ya sakata tatizo hilo, sukari nayo ilianza kuadimika na kupanda bei kufikia Sh5,000 hadi Sh6,000 kwa kilo kwa baadhi ya mikoa. Hata hivyo, upatikanaji wake ulikuwa ni wa shida hadi kuifanya Serikali kuiingilia kati na kutangaza bei elekezi Sh3,000 hadi Sh3,200 kutegemeana na maeneo.

Ili kukabiliana na uhaba huo, Serikali pia iliipa kazi Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuagiza sukari badala ya viwanda vilivyodaiwa kushindwa kutimiza jukumu hilo kikamilifu.

Februari 23 mwaka huu, Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe akizungumza katika mkutano wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus aliwaomba wananchi kuwa wavumilivu wakati Serikali ikishughulikia upatikanaji wa kudumu wa sukari.

Bashe alisema “kama Serikali isingechukua hatua ya NFRA kuingilia uagizaji wa sukari, nchi ingekuwa katika hali mbaya zaidi.

Mgao wa umeme na uhaba wa sukari vilisababisha makali ya maisha kuongezeka.

Wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao kwa kutumia nishati ya umeme walikwama na kuzifunga na wengine kupata hasara.

Ahueni yapatikana

Ahueni sasa imeanza kurejea na mgao wa umeme umepungua kwa baadhi ya mikoa, kama wanavyoeleza baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili.

Msemaji wa Tanesco, Kenneth Boymanda akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Machi 4, 2024, amesema Dar es Salaam kwa sasa haipo kwenye mgao.

“Jiji la Dar es Salaam linaloongoza kwa matumizi ya umeme kutokana na ukubwa wa shughuli za kiuchumi likitumia megawati 516 kwa sasa haina mgao,” amesema Boymanda

Mbali na Dar es Salaam, Boymanda amesema upungufu kwa ujumla umepungua kwa zaidi ya asilimia 85. “Mfano mkoa wa Arusha, ulikuwa na upungufu wa megawati 40 lakini sasa ni kama megawati 10 ambazo haziathiri idadi kubwa ya wananchi.”

Februari 24 mwaka huu, mashine namba tisa katika mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) iliwashwa na umeme wake megawati 235 ukaingizwa katika Gridi ya Taifa. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko alisema megawati hizo zimepunguza mgao.

Dk Biteko alisema mwezi huu mtambo namba nane utawashwa na megawati nyingine 235 zitaingizwa kwenye gridi, hivyo kumaliza kabisa changamoto ya mgao.

Kutokana na ahueni hiyo ya umeme na sukari, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) Dk Paul Loisulie amesema upo umuhimu wa bidhaa hizo kutengamaa kwani ziliondoa utulivu kwa wafanyabiashara, familia na wanasiasa.

"Pale ambapo kulikuwa na uhaba wa sukari na umeme hakukuwa na utulivu wa kila mtu, mama ntilie, familia, ofisini hata wanasiasa wenyewe walikosa utulivu, maana yake vitu vinapotengamaa vinarejesha utulivu," amesema.

Hoja hiyo haipingani na iliyotolewa na Mchambuzi wa Masuala ya Uchumi, Oscar Mkude akisema kuanza kuimarika kwa vitu hivyo kutaonekana kwenye uchumi wa nchi unaohitaji umeme.

“Umeme usipokuwepo uzalishaji unahitaji kutumia mafuta na gharama yake ni kubwa, hivyo kusababisha mfumko wa bei.

“Tumeona hizo megawati 235 zilizoingizwa zimepunguza kidogo makali ya mgao, kama itaendelea hivi hadi Aprili mwishoni, tunaweza kuanza kuona kupungua mfumuko wa bei, lakini ni ikiwa itatengemaa na upatikanaji wake usiyumbe, huku pia ikitegemea na nishati ya mafuta.

Amesema,“kwenye sukari, bado upatikanaji haujatengemaa, tunaagiza nje na kutumia fedha nyingi za kigeni. Hii itaendelea kuleta stress (msongo) kama tutaweza kupambana tatizo lisijirudie, kwa viwanda vyetu vya ndani kuzalisha sukari ya kutosha kupunguza au kumaliza tatizo.”

Mkude amesema, licha ya mvua kutajwa kuwa changamoto, uzalishaji haukuwa mzuri kwani mvua pekee isingeleta ombwe kubwa.

Hali ya sukari ilivyo

Katika maeneo kadhaa, wananchi wameanza kununua sukari kwa Sh3,200 huku mengine ikiendelea kusalia Sh4,500 hadi Sh5,000 kwa kilo moja.

Mkoani Kilimanjaro, kilo moja ya sukari hivi sasa inauzwa Sh3,200 kwa rejareja kutoka Sh4,000 hadi Sh5,000 na Sh3,000 kwa jumla kutoka Sh3,500 sawa na ilivyo kwa baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam.

Tabata, Dar es Salaam kilo moja ya sukari ni Sh4,000 hadi Sh4,500 na mjini Kibaha mkoani Pwani ni Sh4,500 hadi Sh5,000.

Mjini Morogoro, baadhi ya maduka yanauza sukari kwa Sh4, 000 na mengine Sh4,800 huku wauzaji wakibainisha kuwa bei hiyo inatokana na namna walivyoipata.

“Kidogo kuna ahueni kwenye upatikanaji, japo bei ni Sh4,500 hadi Sh4,800 lakini inapatikana,” alisema Seleman Mutabazi wa Morogoro.

Mjini Dodoma, nako foleni kwenye maduka ya mawakala wa sukari imepungua.

Mfanyabiashara wa rejareja wa sukari mkoani humo, Grace Kanjanja alisema upatikanaji wa bishaa hiyo umeimarika baada ya mawakala usambazaji kuongezwa kutoka wawili hadi wanne na bei kupungua kutoka Sh5,500 hadi 6000 kwa kilo na sasa huuzwa Sh3,250.

Kwa upande wake, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Haidary Gulamali ambayo ni wakala wa sukari mkoani humo, Sameer Hussein alisema kampuni hiyo iliagiza tani 162 za sukari kutoka Brazil, Machi 2 mwaka huu na sasa mfuko wenye ujazo wa kilo 50 unauzwa Sh140,000, sawa na Sh2,800 kwa kilo.

Wilayani Sengerema mkoani Mwanza bei imepungua kutoka Sh4,000 kwa kilo hadi Sh3,500. Pia, Stendi ya Nyegezi, mfanyabiashara Engel Bernard alisema anauza kilo moja kwa Sh3,900.

Mkoani Kigoma, kilo ya sukari inauzwa kwa Sh3,500 ikipungua kutoka Sh3,700 ya awali.

Mfanyabiashara eneo la Ujiji mkoani Kigoma, Joshua Isack alisema wananunua mfuko wenye ujazo wa kilo 25 kwa Sh80, 000 (Sh3,200 kwa kilo), jambo linalowalazimu kuiuza kwa Sh3,500.

Mjini Geita wameendelea kuuza kilo Sh3, 800 (rejareja) na jumla Sh3, 500.

Hali ya upatikanaji wa umeme

Kuhusu upatikanaji wa umeme, inaelezwa makali ya mgao yamepungua tofauti na siku za karibuni, ingawa sasa kinachofanyika ni kukatika na kurudi ndani ya muda mfupi mara kwa mara.

“Ule utaratibu wa kukataa asubuhi hadi usiku sasa haupo, isipokuwa wanaukata dakika 10 wanarudisha, baada ya muda mfupi wanakata tena na kurudisha, kuna ile katakata ya mara kwa mara, lakini makali yamepungua,” amesema Anna Julius wa Morogoro.

Jolita Kamoli wa Tabata Magenge Dar es Salaam alisema huduma ya umeme inapatikana muda wote tofauti na ilivyokuwa mwezi uliopita.

“Tunazishukuru mamlaka kwa kuchukua hatua kutuondolea mgao, maana ilikuwa shida tulikuwa tunafanya biashara ya vinywaji ilikuwa changamoto umeme unakata asubuhi unarudi saa tatu usiku biashara hatufanyi lakini sasa hali imekuwa sawa,”amesema.

Mfanyabiashara wa kuku, Bernad Chuwa wa Mbezi Dar es Salaam ambaye mwezi uliopita alipata hasara ya shilingi laki nane kutokana kwa mzigo wake kuharibika, naye amesema mgao umepungua.

“Kwa sasa hali ni tofauti walau kwa wiki hii sijaona umeme ukikatika mara kwa mara,” amesema kauli sawa na ya mfanyabiashara wa saluni, Deta Suleiman ambaye amekiri kutopitia mgao wa umeme kwa siku za hivi karibuni.

Chanzo: Mwananchi
 
Huko wanakosema watatoka na ajenda ya ugumu wa Maisha then wanafanya kikao kwenye hoteli wakila upepo wa bahari 😂😂

Huo ugumu Kwa nini wasituoneshe mfano kwa.kukaa chini ya mti kufanya kikao?

Tafuteni mambuzi ndio muwadanganye.
Wanaodiskasi ugumu wa maisha ya watu wao wanakula vyuku na mvinyo ,,hiyo bajeti na posho wangeenda kuchimba hata visima vya maji huko vijiji vyenye shida
 
Wanaodiskasi ugumu wa maisha ya watu wao wanakula vyuku na mvinyo ,,hiyo bajeti na posho wangeenda kuchimba hata visima vya maji huko vijiji vyenye shida
Wacha mavijana majinga yaendelee kutumika kama mabega ya Wala vyuku wa Chadema 😂😂
 
Wanaodiskasi ugumu wa maisha ya watu wao wanakula vyuku na mvinyo ,,hiyo bajeti na posho wangeenda kuchimba hata visima vya maji huko vijiji vyenye shida
Wapewe mamlaka ya ukusanyaji mapato kwa njia ya kodi,kikokotoo n.k halafu tuone kama hawachimba hivyo visima.
 
Back
Top Bottom