Kahama na Makambako hii miji iandaliwe kuwa miji ya viwanda na biashara kwani imeanza kujipambanua kama Kwala Pwani

Mk boy

JF-Expert Member
Nov 3, 2020
2,293
1,706
Hii itasaidia kupunguza msongamano dsm kwa sababu mikoa husika imesha weka dhamira ya miji hii kuwa na bandari kavu.

2 miji hii imezungukwa na maeneo yenye uzalishaji wa mazao ya chakula ya kutosha ambayo pia ni malighafi viwandani, 3 Nimiji iliyo kaa kimkakati kutokana na Geographical position ni rahisi kuyafikia maeneo mbalimbali katika kanda husika na nchi jirani 4 itasaidia Pato la taifa kuongezeka kwani wakianzisha viwanda vitaingiza Sana pesa za kigeni na hii miji ipo jilani na sehemu zenye migodi mfano makambako ipo jilani na mgodi wa makaa ya mawe ya chuma liganga na mchuchuma ludewa na mkoa husika umedhamiria makambako iwe ya viwanda hivohivo na kahama 5 baada ya miaka kadhaa.

Hii itapelekea kuwa sasa Majiji ya biashara na uwekezaji kama plan za kwala kwani ni miji yenye miundombinu yote muhimu kama reli cha msingi kwa kahama ni kuitoa isaka hadi eneo walilo target bandari kavu kwa makambako reli ipo jilani na eneo la mradi.maana Reli ndo nguzo kuu ya duniani kwa miji ya viwanda na biashara mfano Africa kusin Ina miji SITA ya aina hii.

FB_IMG_16676312485395943.jpg
2018-01-31-1200x675.jpg


Hii ni plan ya pwani ambayo wangeitekeleza hata kwenye miji hii ya kahama na makambako kwani tayari imejipambanua kuwa hivo na mazingira ,maeneo yanaruhusu 👇👇👇👇SERIKALI imelieleza Bunge kuwa inatekeleza mpango wa kuanzisha, kupanga na kuendeleza jiji la kibiashara na uwekezaji katika eneo la Kwala mkoani Pwani. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula amesema hayo bungeni Dodoma wakati anawasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Dk Mabula alisema katika kufanikisha mpango huo, wizara hiyo kwa kushirikiana na wizara nyingine za kisekta imeshiriki katika kuandaa mpango kabambe wa jiji hilo. Alisema mpango kabambe unahusisha eneo lenye ukubwa wa hekta 181,130 linalojumuisha vijiji 30 vya halmashauri za wilaya za Kibaha (16), Chalinze (9) na Kisarawe (5).

“Uanzishwaji wa Jiji hilo unalenga kupata eneo kubwa zaidi la uwekezaji wa viwanda na shughuli nyingine za kiuchumi na pia kupunguza msongamano wa shughuli mbalimbali za kiuchumi katika Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam.

#HabarileoUPDATES
 

Attachments

  • 1703042105170.jpg
    1703042105170.jpg
    58.4 KB · Views: 14
  • 1703042105170.jpg
    1703042105170.jpg
    58.4 KB · Views: 8
  • 1702914137702.jpg
    1702914137702.jpg
    36.3 KB · Views: 12
Kiwanda cha mipira ya mikono cha Bohari ya Dawa (MSD) kilichopo Idofi,Makambako mkoani Njombe kimefanikiwa kupata ithibati ya ubora (GMP).

Hatua hii itawezesha kiwanda hicho kuanza uzalishaji wa bidhaa hiyo na kuuza.

Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha mipira ya mikono 20,000 kwa saa sawa na jozi 10,000 za mipira ya mikono kwa saa.
1707451345805.jpg
1707451112479.jpg
1707451121692.jpg
1707451127485.jpg
1707451132985.jpg
1707451127485.jpg
 
Tumefanya Kikao Kizuri kati yetu Viongozi wa Mkoa wa Njombe( RC na RAS) Pamoja na viongozi wa TAZARA na Taasisi ya Wataalamu wabobezi wa usafirishaji - Chaterd Institute of Logistic and Transport( CILT) Tumekubaliana kwa Pamoja kwamba tuwape kazi ya kufanya upembuzi wa mradi wa uanzishwaji na ujenzi wa Bandari ya Nchi Kavu eneo la Makambako-Itakayotoa huduma muhimu za kiuwekezaji ili kuwezesha ufanisi wa usafirishaji kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya mkoa wa Njombe (Chai,Parachichi,Ngano,na bidhaa zote za Mbao) Multfunctional Dry Port with EPZ Flavour(uwepo wa Bandari hii utaisaidia sii tu Njombe bali nchi katika usafirishaji wa baadhi ya mazao ya kilimo,kama chai,Parachichi,nk-ambayo yamekuwa yakitumia zaidi bandari ya Mombasa kuliko Bandari yetu.Eneo hili tutawaalika wawekezaji katika Smart Containers,Timber treatment Plant,na wawekezaji wengine kwa kadri fursa zitakavyotambuliwa,tutaandaa pia eneo maalumu kwa ajili ya ubebaji wa Makaa ya Mawe pale mradi wake utakapokuwa tayari kuanza ili kurahisisha biashara.Naanza kuyaalika Mabenki na Sekta binafsi ya Tanzania na nje ya Tanzania katika fursa hizi.
Pichani ni Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi.Judica Omary,Mtendaji Mkuu wa TAZARA Mr.Fuad Abdallah, Viongozi wa CILT-Makamu Mwenyekiti -madame Mtaki,Katibu Mtendaji wa CILT -Mzee Sawaka,Mr.Otieno Igogo Mdau wa Badandari,wadau kutoka Tanzania Shippers Council,Uwakilishi kutoka Shirika la Reli TRC, Mr.Khan mshauri Mwelekezi TAZARA na CILT. Karibuni.
1708075365029.jpg
 
Kazi zimeanza makambakohttps://www.facebook.com/reel/1432620897350100/?mibextid=rS40aB7S9Ucbxw6v
 
Tazara makambako mizigo kutoka mikoa ya iringa ,njombe ,ruvuma na baadhi ya maeneo ya mbalari DC mbeya inapakiliwa hapa ko uhitaji wa bandari kavu kubwa ni mkubwa zaidi hii imeshakuwa ndogo sasa
1711451397331.jpg
1711451404588.jpg
Tanzania-administrative-zones-Modified-map-adopted-from-Suleiman-2018-Suleiman-2018~2.jpg
 
Wadau wa parachichi kutoka India wakiwa kwenye eneo la viwanda vya parachichi makambako tc
glr-28-31 (4).jpg
glr-28-31 (1).jpg
glr-28-31 (3).jpg
glr-28-31 (2).jpg
 
Moja ya maeneo yaliyo tengwa kwaajili ya industrial park kahama mc
1696872779244-jpg.2961426
 

Attachments

  • 1696872779244.jpg
    1696872779244.jpg
    115.3 KB · Views: 6
Moja ya maeneo yaliyo tengwa kwaajili ya industrial park makambako tc
1703037483324.jpg
 
Back
Top Bottom