ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,042
- 49,727
Ifahamike kwamba Barabara ndio kichocheo kikubwa Cha Maendeleo ikifuatuwa na umeme.
Mwaka 2005 Serikali ilitangaza Bungeni Hadi kufikia 2020 ,Makao Makuu ya Mikoa yote Tanzania Yatakuwa Yameunganishwa na Barabara za Lami.
Hawakuishia hapo wakasema Barabara zote Kuu za Kuunganisha Nchi na Nchi jirani Zitakuwa na lami.
Lakini Hadi naandika Makala hii,kina Jumla ya Mikoa 21 ya Tanzania ambayo Bado haijaunganishwa Kwa Barabara za lami.
Kuna vipande vina lami na vumbi na Kuna vipande havina lami kabisa Toka mkoloni alivyozianzisha na Baadhi ya Barabara hazipitiki kabisa kipindi Cha mvua.
Nimekuwa najiuliza kama miaka zaidi ya 60 Bado tumeshindwa kuifungua Mikoa yetu Kwa lami,Sasa Wilaya tutazifungua lini? Je kama Taifa tunakwama wapi? Je hatuoni Kuna haja ya Kupitia Upya vipaombele vyetu?
Mikoa ifuatavyo Bado haijaungamishwa na Barabara za lami.Yaank ukitaka kuifikia lazima uzunguke kwingine ambapo ni time consuming,expensive and boring.
1.Mbeya-Singida
2.Mbeya-Tabora
3.Ruvuma-Morogoro
4.Ruvuma-Lindi
5.Morogoro-Lindi
6.Iringa-Singida
7.Tanga-Manyara
8.Arusha-Mara
9.Arusha-Simiyu
10.Njombe-Morogoro
11.Tabora-Kigoma
12.Songwe-Katavi
13.Tanga-Morogoro
14.Kigoma-Kagera/Geita
15.Singida-Simiyu
16.Iringa-Tabora
17.Kigoma-Katavi
18.Kilimanjaro-Manyara.
19.Mbeya-Katavi
20.Mtwara-Iringa
21.Iringa-Katavi.
Ushauri Wangu Kwa Serikali
Kama tunataka kutimiza lengo na Ufanisi wa Ujenzi wa Barabara na kufungua Uchumi wa watu Wetu basi tuzingatie yafuatayo;
1.Tujenga Barabara chache Kwa Vipaombele badala ya mtindo wa Sasa wa kutapanya Rasilimali kukidhi matakwa ya Kisiasa.
-Una Bajeti ya Bil.600 unaigawanya Kwa Barabara zote Nchi nzima ambako Barabara ya km 200 au 500 unaipa pesa bil 10-25 ambapo itakuchukua miaka zaidi ya 10 kuzimaliza.Lakini tungechagua Barabara za kipaombele chache na kuzipa Rasilimali Kila mwaka tungekuwa tunatoka na Barabara zilizokamiliaka na zinazozalisha.
2.Tubadili mtindo wa financing.
-Badala ya kusubiria makusanyo ya kudunduliza Kwa Wananchi wakiuza pamba na dengu,ni Bora Serikali itoe infrastructure bond ambazo Taasisi mbalimbali,makampuni na watu biabafsi watatoa pesa na pesa ya ujenzi kupatika.Unavyochelewa ujenzi ndivyo hata gharama zinaongezeka.
3.Tuwe na mifumo ya Kushirikisha Sekta binafsi kujenga Barabara
-Mfano badala ya kutegemea Serikali kuu Moja kwa Moja tunaweza tumia mifumo ya kushirikiana na sekta binafsi kwenye ujenzi kama Nchi zingine zinavyofanya.
4.Tuwezeshe Wakandarasi Wetu wa Ndani Badala ya kutegemea Wageni Kila kitu.
-Ukiwa na mkandarasi wako wa ndani Badala ya kimlipa Dola kama hao wa Nje tutawalipa Kwa Shilingi yetu hivyo kuokoa Fedha za kigeni na kuleta mzunguko wa pesa ndani ya Nchi.
5.Serikali Isiogope Kukopa Kwa Ajili ya Kuwekeza Kwenye Miundombinu.
-Huwa zinatoka ripoti hapa kwamba Tanzania ni Kati ya Nchi Zenye Madeni madogo.Unajiuliza nafasi ya kukopa unayo harafu unashangilia kutokopa wakati unaogelea kwenye umaskini,tumelalia uchumi Kwa sababu Nchi haifikii.Ni ujinga kushangilia umaskini.Tukope tuweke pesa kwenye Barabara, uzalishaji ukianza pesa zitarudishwa.
My Take
Serikali ijitathmini na kujisahihisha.
Pia Soma Serikali kopeni pesa WB/IMF/AfDB mjenge barabara kutoka Mpanda-Iringa-Mtwara ili kuunganisha DRC na Bandari ya Mtwara

Barabara muhimu zilizobeba uchumi wa nchi ambazo zimetelekezwa. Serikali tupieni jicho
Wote kwenye maeneo yetu tunahitaji Barabara kulingana na umuhimu wake kuchochea uchumi wa mtu mmja mmja na Taifa Kwa ujumla. Pamoja na umuhimu huo Kuna Barabara ambazo ni za Muhimu sana Kwa maendelea ya Nchi na watu lakini bahati mbaya sana Serikali ni kama imezitelekeza. Serikali azipe...
www.jamiiforums.com