Ni miaka miwili kamili leo hii tangu aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hayati John Pombe Magufuli afariki dunia.
Kifo cha Magufuli kilipokelewa kwa hisia tofauti na watanzania wengi wakionesha kushtushwa na kifo cha ghafla cha rais aliyekuwa madarakani.
Magufuli alifanya mengi yaliyowafurahisha watanzania lakini pia alifanya mengi yaliyowachukiza watanzania. Wapo wanaodai uongozi wa Magufuli uliwaumiza wao binafsi au biashara na ajira zao. Kama taifa kuna watu wanaona uongozi wa Magufuli ulitenda mambo yaliyoliumiza taifa letu kiuchumi na kijamii.
Je, kuna haja ya kufanyika maridhiano kati ya serikali (kwa niaba ya Magufuli) na wananchi ambao wengi wameonesha hasira zao kwa uongozi wa awamu ya tano wa hayati Magufuli?