Kuna haja kwa Watanzania kumsamehe hayati Dkt. John Magufuli. Nini kifanyike?

Taja makosa yake ili tujue tunaanzia wapi. Achana na tuhuma maana zinaweza kuwa kweli au si za kweli.
Elezea MAKOSA YA DHAHIRI (ya kweli) aliyoyafanya
A picture speaks thousand words.
Screenshot_20230316-012242.jpg
 
Aliwabana wezi sasa ndio Hawa wanapiga kelele.
Tumeshawafahamu wote.
Yaani watu wote wanaokosoa ule utawala wa kimbilikimo ni wezi? Watu kundika juu ya ufedhuli wa kile kipindi cha giza ni kupiga kelele? Ukisikia watu kukosa hoja ndiyo hii! Lakini haishangazi kwani hata kipindi kile hakikuwa kipindi cha kupambanisha hoja; kilikuwa kipindi cha hoja kupigwa rungu!

Marehemu alibana wezi wa awamu iliyotangulia ili aweze kustawisha wezi wa awamu ya tano ambao kusema kweli walikuwa waporaji na wabaya mara elfu kuliko wa awamu zote zilizotangulia. Ubaya wa wezi wa awamu ya tano ni kwamba walilenga kuua taasisi na vyombo rasmi vya nchi na kuvipora majukumu yake kwa umma na badala yake vyote vikaelekezwa kutumikia genge la uhalifu, wezi na wanyang'anyi! Ofisi ya CAG ni chombo rasmi cha kikatiba cha kuwezesha nchi kusimamia matumizi mazuri ya rasilmali zake.

Aidha Prof. Assad alijipambanua kama mzalendo na mwanataaluma mahiri, asiyeyumba, asiyerubunika na aliyekuwa tayari kuisadia nchi hii kudhibiti wizi wa rasilmali za umma. Nini kilimtokea? Si Katiba ya nchi ilivunjwa ilimradi tu aondolewe ofisini? Vyombo vya habari vina nafasi kubwa sana katika kuibua vitendo vya wizi, ufisadi na ubadhirifu na kuisadia nchi kupambana na matendo hayo; alivifanyaje, si alivifungia na kuvinyamazisha? Asasi za kiraia ni washirika wazuru sana wa serikali makini yenye dhamira ya kupambana na maovu katika jamii ikiwa ni pamoja na wizi wa mali ya umma; aliviua!

TAKUKURU ni chombo cha serikali cha kupambana na rushwa; hatua yake ya kwanza alipoingia madarakani ni kumstaafusha Mkurugenzi Mkuu, kwa kuamini kuwa hataweza kukubali kupokea maelekezo yasiyozingatia dhamana ya taasisi hiyo.

Badala yake akapeleka Polisi akijua hao wamelelewa kupokea amru tu. Matokeo yake TAKUKURU ikaacha kupambana na rushwa ikafanya kazi kisiasa. Kifupi, marehemu hakuwa na dhamira hata chembe ya kupambana na wizi na ufusadi; alikuwa anafanya hadaa tu ili aweze kufanya mambo yake! Bahati mbaya raia wengi "wanyonge" walidanganyika sana na kauli nyepesi za rais wa wanyonge, nchi hii imechezewa sana na vitendo vya kutumbua watumishi bila kufuata sheria!

Alifanya nini kuhusu 1.5t/= ambazo zilipotelea hazina na kubainishwa na mamlaka ya kikatiba, yaani CAG? Na sasa tunasemaje kuhusu billions za plea bargain zilizofichwa China. Ipo siku haya yote yatafanyiwa kazi.
 
Ni miaka miwili kamili leo hii tangu aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hayati John Pombe Magufuli afariki dunia...
Ukiacha Nyerere,viongozi wote wa ccm waliopita ni majambazi,ilibidi wawe jera kwa maovu waliyofsnya.

Richa ya kwamba Kuna watu wazuri ccm,lakini Kuna hari Fulani majambazi ndio uchukua uongozi, Ahmed Salim angekuwa Rais mzuri kuliko Kikwete,lakini wakakata jina lake.

Sasa hv tunaongozwa na mtu asie na Elimu ya maana,mtu mwenye uzoefu wa kuongoza NGO,leo kapewa ukuu wa nchi!

Ilibidi watu wenye akili nyingi mfano Profesa Anna Tibaijuka ndio awe Raisi lakini ndio tunaongozwa na kilaza
 
Jaffari Amini aliwahi kufanya maridhiano kwa niaba ya familia yake dhidi ya watu walioguswa na madhira ya utawala wa Idd Amin, hivyo ajitokeze mtoto wa Magufuli afanye maridhiano hayo, Kwani Serikali nayo ni muhanga wa awamu ya tano
 
Jaffari Amini aliwahi kufanya maridhiano kwa niaba ya familia yake dhidi ya watu walioguswa na madhira ya utawala wa Idd Amin, hivyo ajitokeze mtoto wa Magufuli afanye maridhiano hayo, Kwani Serikali nayo ni muhanga wa awamu ya tano
Hawatokaa wajitokeze na hakuna kitu utafanya.
 
Ni miaka miwili kamili leo hii tangu aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hayati John Pombe Magufuli afariki dunia...
Hakuna Mtanzania anayemchukia JPM ila CHADEMA , CCM na ACT ndio magenge pekee ambayo yametamalaki kumshambulia lakini raia roho kwao kwatu kwa huyo mbabe wa warafi, waonezi na majinuni
 
Bila ya shaka wewe ni miongonj wa waliotumbuliwa na JPM
sijawahi kuwa mfanyakaz serikalin so he was powerless to fire me from my duties hence your statement signfies to be of a person of short knowledge thinking that every person who criticises that stupud person that entered into power by vote theft was sacked by him while not, I urge you and your colleagues who used to benefit from that draconian rule to repent publicly on behalf of that tyrant before 2025, otherwise you will all perish come 2025 if you do not confess.
 
Hakuna Mtanzania anayemchukia JPM ila CDM , CCM na ACT ndio magenge pekee ambayo yametamalaki kumshambulia lakini raia roho kwao kwatu kwa huyo mbabe wa warafi, waonezi na majinuni
Wewe ni mmojawapo wa Genge S, kwanza pole kwa siku siku hii muhimu kwenu. Unajua JPM aliwafanyia watu mambo gani kupitia Genge S na watu waliumia kivipi na wangapi wamepotea hadi leo au kubaki na ulemavu?!
 
Yaani watu wote wanaokosoa ule utawala wa kimbilikimo ni wezi? Watu kundika juu ya ufedhuli wa kile kipindi cha giza ni kupiga kelele? Ukisikia watu kukosa hoja ndiyo hii! Lakini haishangazi kwani hata kipindi kile hakikuwa kipindi cha kupambanisha hoja; kilikuwa kipindi cha hoja kupigwa rungu! Marehemu alibana wezi wa awamu iliyotangulia ili aweze kustawisha wezi wa awamu ya tano ambao kusema kweli walikuwa waporaji na wabaya mara elfu kuliko wa awamu zote zilizotangulia. Ubaya wa wezi wa awamu ya tano ni kwamba walilenga kuua taasisi na vyombo rasmi vya nchi na kuvipora majukumu yake kwa umma na badala yake vyote vikaelekezwa kutumikia genge la uhalifu, wezi na wanyang'anyi! Ofisi ya CAG ni chombo rasmi cha kikatiba cha kuwezesha nchi kusimamia matumizi mazuri ya rasilmali zake. Aidha Prof. Assad alijipambanua kama mzalendo na mwanataaluma mahiri, asiyeyumba, asiyerubunika na aliyekuwa tayari kuisadia nchi hii kudhibiti wizi wa rasilmali za umma. Nini kilimtokea? Si Katiba ya nchi ilivunjwa ilimradi tu aondolewe ofisini? Vyombo vya habari vina nafasi kubwa sana katika kuibua vitendo vya wizi, ufisadi na ubadhirifu na kuisadia nchi kupambana na matendo hayo; alivifanyaje, si alivifungia na kuvinyamazisha? Asasi za kiraia ni washirika wazuru sana wa serikali makini yenye dhamira ya kupambana na maovu katika jamii ikiwa ni pamoja na wizi wa mali ya umma; aliviua!

TAKUKURU ni chombo cha serikali cha kupambana na rushwa; hatua yake ya kwanza alipoingia madarakani ni kumstaafusha Mkurugenzi Mkuu, kwa kuamini kuwa hataweza kukubali kupokea maelekezo yasiyozingatia dhamana ya taasisi hiyo. Badala yake akapeleka Polisi akijua hao wamelelewa kupokea amru tu. Matokeo yake TAKUKURU ikaacha kupambana na rushwa ikafanya kazi kisiasa. Kifupi, marehemu hakuwa na dhamira hata chembe ya kupambana na wizi na ufusadi; alikuwa anafanya hadaa tu ili aweze kufanya mambo yake! Bahati mbaya raia wengi "wanyonge" walidanganyika sana na kauli nyepesi za rais wa wanyonge, nchi hii imechezewa sana na vitendo vya kutumbua watumishi bila kufuata sheria!

Alifanya nini kuhusu 1.5t/= ambazo zilipotelea hazina na kubainishwa na mamlaka ya kikatiba, yaani CAG? Na sasa tunasemaje kuhusu billions za plea bargain zilizofichwa China. Ipo siku haya yote yatafanyiwa kazi.
Wezi ndio Hawa wanatamba Sasa.
 
Jukwaa hili siyo mahali pa kuchambua makosa ya awamu ya tano. Isitoshe, kama mtu mzima, raia wa nchi hii mwenye macho, masikio na akili timamu mpaka sasa hajaona makosa ya kipindi hicho basi hata akitajiwa na kuelezwa hatakubali. Kibinadamu hali hii ipo na ndiyo maana mataifa hujiwekea katiba, sheria, kanuni na miongozo mingine ya kusimika ustaarabu.
Tunaishi kwenye jamii mfu ki fikra 'marginalize community'
 
Huu mtandao wa Jf tusipo jua kutumia kwa faida hakika tutazidi kua maskini wa Akili na Fikra.

Tazama mtu anapoteza muda wake kuanzisha uzi kama huu na watu wanatiririka kuchangia.
This is rubbish.

Umaskini wamaisha na Fikra ni ugonjwa wetu.
Kipimo ni hizi nyuzi za hovyo zinazo anzishwa kila siku majukwaani hapa Jf.
 
Back
Top Bottom