Kuna haja kwa Watanzania kumsamehe hayati Dkt. John Magufuli. Nini kifanyike?

Ni miaka miwili kamili leo hii tangu aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hayati John Pombe Magufuli afariki dunia....
Hakuna jambo lolote kubwa na la maana sana lililofanyika nchini awamu ya tano ya kufanya taifa hili liukumbuke sana uongozi wa kipindi hicho.

Sana sana awamu hiyo ilikuwa imejikita sana katika propaganda na kuwaaminisha raia kuwa inafanya kazi kubwa na ya kipekee tofauti na awamu zote zilizopita. Matokeo yake uongozi wa kipindi kile ulitengeneza makundi ya watu yalifurahishwa sana na kupumbazwa na kauli nyepesi na propaganda nyingi za kujisifia.

Aidha makundi hayo yalitumika pia kuhalalisha matendo ya ubaguzi wa kiitikadi na kijiografia, uporaji wa mali za watu; uonevu dhidi ya watumishi wa umma kuwa ndiyo wanaowasababishia raia hali ngumu ya maisha;

Miradi ya kifahari isiyofuata taratibu na iliyolenga kuujengea uongozi utukufu, nk. Hivyo awamu ya tani itabaki tu kuwa doa jeusi katika historia ya taifa hili.

Changamoto kubwa na jukumu la kipekee la kizazi kilichoshuhudia uovu wa kipindi hicho cha giza ni kuhakikisha kuwa katika muda mfupi sana iwezekavyo hatua zote za kimfumo na kisheria zinachukuliwa kuhakikisha kuwa nafasi ya uovu huo kujirudia inaondolewa kabisa.
 
Ni miaka miwili kamili leo hii tangu aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hayati John Pombe Magufuli afariki dunia...
Hapa ni funzo kwa watanzania kuhusu umuhimu wa katiba inayo kidhi mahitaji ya sasa pengine siyo katiba tu bali jamii yetu iwe ni jamii ya kuhoji na kutoa suluhisho la matatizo yaliyoko kwenye jamii kwa kusikilizwa na kuyachuka 'assimilate' na siyo ya bora liende na kusifu kila kukicha 'marginalize community'
 
Waliopo madarakani kwa Sasa inapaswa watuombe Radhi.
Kuomba radhi lingeweza kuwa jambo jepesi sana na la kiungwana kulifanya, lakini kwa mazingira yetu yaliyotawaliwa na kiburi cha madaraka ni jambo gumu! Hata hivyo, pamoja na ukweli kuwa kwa sehemu kubwa uongozi wa kipindi kile ulikuwa wa mtu mmoja, bado isingewezekana marehemu kutekeleza uovu ule wote peke yake.

Wapo watu wengi walioshiriki kufanikisha uovu ule kwa manufaa yao binafsi kisiasa na kiuchumi. Njia bora ya kushughulikia doa hilo ni tume ya ukweli na usuluhishi.

Wahanga wa dhuluma na uonevu wakajieleze mbele ya tume na pale inapowezekana wataje majina watu waliowaumiza moja kwa moja.

Washiriki wa uonevu na na unyanyasaji nao wafike mbele ya tume kujieleza mazingira ya ushiriki wao. Pale ambapo jinai itabainika waziwazi wahusika wakabidhiwe vyombo vinavyohusika.
 
Washirikina Huwa wapo hivyo.

Wanakua na chuki na marehemu.
Marehemu mwenyewe alikuwa na chuki isiyoelezeka kwa maneno. Hakuna maneno ya kuweza kuelezea kiwango cha chuki yake bali mtu anaweza tu kupata picha kwa kutazama matendo yake na kuyadadavua. Uchaguzi mkuu na ule wa vijiji na mitaa ni jambo takatifu katika jamii inayojipambanua kustaarabika.

Ukiona mtu hathamini jambo hilo linalolenga kuwezesha raia kuwapata vingozi wanaowapenda na kuwaamini ujue kuna tatizo kubwa sana.

Kitendo cha kuvuruga chaguzi za 2019, 2020 na kuwanyima raia nchi nzima haki hiyo ni zaidi hata ya chuki dhidi ya washindani wa kisiasa;

Pengine ni uhayawani wa aina yake. Kwa hakika hata chama chake kilistushwa sana na kitendo hicho na kupata hofu kwamba hatua itakayofuata ni chama hicho tawala nacho kufutwa rasmi baada ya kujimilikisha!
 
Marehemu mwenyewe alikuwa na chuki isiyoelezeka kwa maneno. Hakuna maneno ya kuweza kuelezea kiwango cha chuki yake bali mtu anaweza tu kupata picha kwa kutazama matendo yake na kuyadadavua...
Nani anazijua sifa za mzalendo nambali 'one'
 
Taja makosa yake ili tujue tunaanzia wapi. Achana na tuhuma maana zinaweza kuwa kweli au si za kweli.
Elezea MAKOSA YA DHAHIRI (ya kweli) aliyoyafanya
Jukwaa hili siyo mahali pa kuchambua makosa ya awamu ya tano. Isitoshe, kama mtu mzima, raia wa nchi hii mwenye macho, masikio na akili timamu mpaka sasa hajaona makosa ya kipindi hicho basi hata akitajiwa na kuelezwa hatakubali. Kibinadamu hali hii ipo na ndiyo maana mataifa hujiwekea katiba, sheria, kanuni na miongozo mingine ya kusimika ustaarabu.
 
Kuna kikundi kinamtumia kwa maslahi binafsi yasiyojulikana.

Huwa kinakuja kwa mtindo wa kumchafua au kumtukuza halafu mdahalo unaanza ambao wala hauna maslahi yoyote zaidi ya kumbishania aliyekwisha lala.
 
Jukwaa hili siyo mahali pa kuchambua makosa ya awamu ya tano. Isitoshe, kama mtu mzima, raia wa nchi hii mwenye macho, masikio na akili timamu mpaka sasa hajaona makosa ya kipindi hicho basi hata akitajiwa na kuelezwa hatakubali. Kibinadamu hali hii ipo na ndiyo maana mataifa hujiwekea katiba, sheria, kanuni na miongozo mingine ya kusimika ustaarabu.
Mbona unaandika maelezo marefu lakini unadhindwa kutaja makosa umeambiwa orodhesha makosa? Ilo ndio swali
 
Hayati JPM, alikuwa ni mwanaume halisi asiyeruhusu watu wampande kichwani. He was a really man.
Mtu wa aina hiyo hafai kuwa kiongozi wa kisiasa bali wa familia tu! Ofisi ya umma haihitaji mtu wa aina hii: mwamba asiyekubali kupandwa kichwani!

Badala yake inahitaji mtu mwenye uwezo wa kushawishi watu wamwelewe, wampende na kumfuata; mtu kujibizana kwa hoja badala ya mabavu na bunduki.

Alikuwa hana uwezo wa kushawishi wala kujenga hoja na ndiyo maana alitumia mabavu na vyombo kuwakandamiza na kuwaumiza kimwili washindani wa kisiasa pamoja na raia wengine aliohisi wanao ushawishi kwenye jamii kama matajiri!
 
Siku kama ya leo jioni kuna watu walikuwa wanachoma mbuzi na kugonga glass.

Amini leo watarudia hilo zoezi, pengine ukawa ndio utamaduni wao.
 
Washirikina Huwa wapo hivyo.

Wanakua na chuki na marehemu.
Basi dunia inayowachukia marehemu Adolf Hitler, Emperor Bokassa, Mussolini, Idd Amin Dada, Mobutu, Pol Pot, John Vosta, Magufuli na wengine wote wanao-fit kwenye categories za kimatendo similar to those mentioned it means wote ni washirikina kwani wote hao wameshaenda zao kuzimu.
 
Naona kuwa na chuki iliyopitiliza kwa marehemu ni sawa na aina fulani ya uchizi tu.

Huko ni kujitafutia stress zisizo za lazima mwishowe unakufa mapema kizembe tu.
Unakuta mtu anacommet kwa hasira kama anapigana na simu yake,kumbe anamfokea Marehemu.Kweli huu ni uchizi.
 
Back
Top Bottom