UVCCM Wilaya ya Chato watakiwa kumuenzi Hayati Magufuli kwa kuchapa kazi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

CDE. REUBEN SAGAYIKA AWATAKA UVCCM CHATO KUMUENZI MAGUFULI KWA KUCHAPA KAZI

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Chato wametakiwa kumuenzi Rais wa awamu ya tano, Hayati Dkt. John Magufuli kwa kuchapa kazi na kuiishi slogan yake ya Hapa Kazi Tu.

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka UVCCM Mkoa wa Geita, Reuben Sagayika wakati akihitimisha matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na UVCCM Chato maalum kwa ajili ya kumuenzi Hayati Dkt. Magufuli.

Reuben Sagayika Amesema vijana hawawezi kumuenzi Dk Magufuli kwa kuendekeza tabia za wizi na uharifu pasipo kuwajibika kwenye nafasi zao na hivo maadhimisho ya miaka mitatu ya kifo chake iwe ni chachu ya mabadiliko.

Aidha, Reuben Sagayika amewaomba vijana kuendelea kujitolea kwa ajili ya kukijenga chama ambapo amemushukuru binti wa Hayati Dkt. Magufuli ambaye ni Jesca Magufuli kwa kujitolea baadhi ya vifaa ujenzi kukamilisha ujenzi wa nyumba ya katibu wa UVCCM Chato.

Kwa upande wake, Jesca Magufuli amesema kuwa amewiwa kujitolea baadhi ya vifaa ujenzi vya nyumba ya katibu wa UVCCM kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za vijana wa CCM ambao wameonyesha dira ya uwajibikaji

Naye, Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Chato, Frank Kuzenza amesema viongozi wanapoaminiwa kwenye nafasi zao wanapaswa kufuata nyayo za Hayati Dk Magufuli kwa kuwajibika na siyo kwa maneno.

WhatsApp Image 2024-03-17 at 17.19.33.jpeg

WhatsApp Image 2024-03-17 at 17.19.32(2).jpeg

WhatsApp Image 2024-03-17 at 17.19.32(1).jpeg

WhatsApp Image 2024-03-17 at 17.19.32.jpeg
 
Back
Top Bottom