Kuna haja kwa Watanzania kumsamehe hayati Dkt. John Magufuli. Nini kifanyike?

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,652
18,309
Ni miaka miwili kamili leo hii tangu aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hayati John Pombe Magufuli afariki dunia.

Kifo cha Magufuli kilipokelewa kwa hisia tofauti na watanzania wengi wakionesha kushtushwa na kifo cha ghafla cha rais aliyekuwa madarakani.

Magufuli alifanya mengi yaliyowafurahisha watanzania lakini pia alifanya mengi yaliyowachukiza watanzania. Wapo wanaodai uongozi wa Magufuli uliwaumiza wao binafsi au biashara na ajira zao. Kama taifa kuna watu wanaona uongozi wa Magufuli ulitenda mambo yaliyoliumiza taifa letu kiuchumi na kijamii.

Je, kuna haja ya kufanyika maridhiano kati ya serikali (kwa niaba ya Magufuli) na wananchi ambao wengi wameonesha hasira zao kwa uongozi wa awamu ya tano wa hayati Magufuli?
 
Naona kuwa na chuki iliyopitiliza kwa marehemu ni sawa na aina fulani ya uchizi tu.

Huko ni kujitafutia stress zisizo za lazima mwishowe unakufa mapema kizembe tu.
...na kinyume Chake Ndio hivyohivyo!
 
Ili watu wasahau muacheni msiandike habari zake.
Inaonekana kuna watu wanahasira nae akitajwatu wanalipukwa na hasira na chuki za dhahiri
KWANZA AKIRI DHAMBI ZAKE HADHARANI ALIZOZITENDA NA KUELEZA KILA KITU ALICHOKIFANYA KWA MKONO WAKE KINYWA CHAKE KWA KUWA HAYUPO BASI WAJITOKEZE WANAOMHURUMIA WANAOYAJUA YOTE ALIYOYAFANYA WAMWOMBEE MSAMAHA
 
Ni miaka miwili kamili leo hii tangu aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hayati John Pombe Magufuli afariki dunia...
Taja makosa yake ili tujue tunaanzia wapi. Achana na tuhuma maana zinaweza kuwa kweli au si za kweli.
Elezea MAKOSA YA DHAHIRI (ya kweli) aliyoyafanya
 
Ni miaka miwili kamili leo hii tangu aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hayati John Pombe Magufuli afariki dunia...
Mabadiliko yoyote kuna watakao nufaika na watakao umia. Nchi zetu za kiafrika zina sehemu kuu tatu ambazo ni wananchi wa kawaida, serikali na mabepali.

Wananchi ni kama swala na mabepali ni kama simba, Serikali anakaa katikati kuhakikisha wanamchunga simba asiweze kula swala wote.

Mara zote serikali nyingi huwa zinaegemea upande wa simba na kuruhusu unyonyaji mwingi katika upande wa swala.

Serikali imara lazima ihakikishe simba anasimamia ipasavyo. Kiongozi yeyote ambaye yupo makini na hao simba lazima wataanza kumchukia kwa kubana chakula chao.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom