Kuna faida gani za nchi kuruhusu mataifa kuingia bila VISA?

olimpio

JF-Expert Member
Apr 5, 2023
402
834
Nimeona Rais wa Kenya Ruto amefuta visa entry requirement kwake.

Kuna faida yeyote ya kiuwekezaji?

Je dola 20 au 50 zilikua kikwazo kuingiza watu nchini?

Kwamba kuna wawekezaji serious walishindwa kwenda Kenya kwa kukosa dola 30?

Hii kwangu naiona kama njia ya kukaribisha magaidi nchini Kenya na sio njia au jambo zuri la kuiga Tanzania? ukifanya hivyo, kesho uhamiaji watajaa wasomali maelfu kwa kigezo cha utalii tutaingiza magaidi nchini.
 
Inasaidia kuongeza fedha za kigeni, kwa sababu itatembelewa na watu wengi. Pia inawezekana pia ikaendana na marekebisho chanya katika uwekezaji, na kuweza kuzalisha ajira za kutosha.

Pia wanajiwekea mazingira kwa wananchi wake kukubaliwa huko nje wanakoenda kutafuta fursa; kwa kuimarisha ushirika na nchi za kigeni.​
 
Huhitaji visa ila unahitaji passport. Requirement ya Passport au identification ipo pale pale.

Kenya inajua ina limited opportunities kwa raia wake hapo inalenga nchi zingine zijae nazo ziseme wakenya hamuhitaji visa kuinga kwao ila wakenya wazamie huko. Tayari imepeleka wanajeshi wake Haiti na wakulima Israel. It's a good idea but also to please the white masaa. However you wanna take it.


Update: Raia wamedinda

1000064902.jpg
 
Mchakato wa kupatikana VISA unaweza kua na mlolongo mrefu mpaka ukaleta dosari.

Mfano. Taratibu za kupata VISA ya marekani zinaboa sana kama ulikua una plan kwenda vaccation tu unaweza kata tamaa.

Sijajua taratibu za kupata VISA ya kwetu hapa bongo/Kenya

Mosi, huhitaji visa kwenda Kenya or unapewa at point of entry. Pili, Visa ya Kenya na nchi zinazoendelea haijawahi kuwa issue. Visa za developed countries zitaendelea kuwa issue, maji na mafuta hayapatani.
 
Kwahiyo gaidi hawezi lipa dola 20-50 ili aingie...visa zenyewe zimekuwa kama ni stamp tu..hakuna ukaguzi wowote unaofanyika kabla ya mtu kupewa hiyo visa..its just visa on arrival. Nchi za ulaya ndo wapo serious mpaka kupata hiyo visa wanahitaji alot of proof .siyo hizi visa za Ke ya na Tz
 
Nimeona Rais wa Kenya Ruto amefuta visa entry requirement kwake.
Kuna faida yeyote ya kiuwekezaji?
je dola 20 au 50 zilikua kikwazo kuingiza watu nchini?
kwamba kuna wawekezaji serious walishindwa kwenda kenya kwa kukosa dola 30?

hii kwangu naiona kama njia ya kukaribisha magaidi nchini Kenya na sio njia au jambo zuri la kuiga Tanzania
ukifanya hivyo ,kesho uhamiaji watajaa wasomali maelfu kwa kigezo cha utalii
tutaingiza magaidi nchini
Niujinga wa mtu mweusi ...hakuna faida yoyote zaidi ya kufungua mlango kwa wahalifu
 
Back
Top Bottom