Utoaji wa VISA Duniani unasimamiwa na principle ya Reciprocity; kauli ya Rais wa Kenya imejaa presha ya kisiasa kuwakabili wakosoaji wa sera zake

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Dunia inaendeshwa kwa nipe nikupe, au kwa kauli nyingine nikune nikukune. Visa nayo ipo hivyo; tafsiri nyepesi ni makubaliano ya nchi na nchi kuhusu taratibu za kuingia na kutoka katika mataifa husika.

Rais wa Kenya amekaribisha wageni kuingia Kenya bila visa, lakini hakuna Sehemu kwenye hotuba yake anazungumzia ni Mataifa mangapi kuanzia sasa wakenya wataingia bure? Ni Mataifa gani wakenya watakwenda bila visa wala masharti? Kama bado wananchi wake wanawekewa vikwazo nini malengo yake kwa wakenya?

Anakwenda kufungua wimbi kubwa la watu wasio na ajira kwenda kupata ajira Kenya; anakwenda kufungua milango kwa nchi yake kuingia gharama kubwa kuwaondosha Nchini humo wageni wanaokiuka masharti ya Uhamiaji. Anaenda kutengeneza bomu la wakenya kupokonyana fursa na wageni.

Lakini pia sidhani kama amethibiti mianya ya ukwepaji kodi, means upo uwezekano mkubwa wageni wakachukua Kenya na kupeleka kwao kama remittance huku Kenya ikiwa hainufaiki

South Afrika wanalipisha visa wageni lakini angalia namna wanavyoumizwa na wageni; uchumi unaanza na amani. Leo South Afrika gharama wanazotumia kulinda amani ndani ni kubwa kutokana na wingi wa waalifu hasa kutoka Afrika Magharibi na Ulaya. Kenya wamejiandaa au president katamka akiamini kila mgeni ni fursa?

Leo Uingereza Taifa kubwa linapigana kuwarejesha waafrika wakimbizi wakaishi Rwanda; means wanaelewa athari za wageni kwa wazawa.

Marekani wanakimbiza wageni daily huku wakiwa wamewafilisi......Rais wa Kenya naamini anaweza akawa na nia njema ila athari za kufungua mipaka bila kujiandaa zinaweza kusumbua ukanda wetu.

Lakini kwa Tanzania hii ni fursa kwa sababu wageni wakiongezeka Kenya kama kweli wataongezeka basi na Tanzania wataongezeka. Wageni wakifika Kenya lazima watalipa dola 50 kuingia Tanzania kuona fursa na utalii. Tunakwenda kunufaika moja kwa moja na uamuzi huu. Tumesogezewa fursa karibu tuzidi kukaza.

Naona ni fursa kwa sababu Wakenya , Waganda na Wanyarwanda waliwahi kuunda coalition of the will ndani na Afrika mashariki. Walidhani Tanzania atawaunga Mkono ila tulikaa kimya; hadi sasa hakuna matunda wanayopata ambayo sisi hatupati. Waliwahi kusema tutumie ID tukagoma na bado tukazidi kuwa kimbilio la Wageni.

Walitaka ardhi iwe jambo la Afrika mashariki tukakataa.....hakuna athari tulizopata hadi sasa. Hawa wenzetu maamuzi yao yasije hata siku moja yakawa maamuzi yetu. Kinadharia tunaweza tukadhani wanaona karibu ila kivitendo wanaona mbali.

Mfano wa mwisho, juzi kati hapa magazeti ya Kenya yalitoa makala kuilalamikia Tanzania kukataa mgeni anayeingia Afrika mashariki basi alipe visa kwenye nchi aliyoingilia na baada ya hapo aingie na kutoka kwenye nchi nyingine anavyotaka ...Tanzania tulibaki na msimamo wetu wageni walipe Visa. Hivyo kama unasoma politics za wenzetu wanatafuta namna yakutulegeza watumie fursa ya amani yetu kunufaika.

Nimekaa Ulaya sijawahi kusikia nchi ya Ulaya ikiwaza kunufaisha waafrika. Nimekaa Asia hakuna anayetamani Afrika inyanyuke. Tusipokubali kuwa na wanasiasa wanaosimama na wananchi wao tukawa na wanasiasa wanaotegemea wageni kila siku tutarudi kutawaliwa.

Hakuna Dunia ya wote
 
Kenya is struggling.... visa free ni moja wapo ya namna ya kutapatapa... kwamba iwe rahisi raia wa nchi za nje waingie Kenya walete dola na kuiokoa shilingi yao ambayo ipo matatani.

Kwamba ikiwa wakiweka visa free na nchi nyingine waka reciprocate basi raia wa kenya waende nchi za nje kufanya kazi na kutuma remittances itayoongeza dola inflows na kuokoa shilingi ya kenya.

Haimaanishi na sisi Tanzania tuwaige tuweke visa free itakuwa ni upuuzi. Wana malengo yao, na ni moja wapo ya mipango ya dharura ya Ruto kuokoa jahazi ambalo ni kama limetoboka tayari
 
Focus on your countries policies. Kenyan policies are non of your business.
 
Back
Top Bottom