Kuna faida gani kuwa tajiri?

Kuna faida gani kuwa tajiri?

Utajiri si chanzo cha furaha but Utajiri unakupa Uhuru na machaguo...
Machaguo gani mkuu? Hivi unajua magonjwa mengi ya mifumo ya maisha kama vile kidney failure yanawapata matajiri na chanzo kikuu ni huo uhuru wa machaguo? Ukiwa na ufinyu wa machaguo, hio ndiyo furaha ya maisha hapa duniani mkuu.
 
Utajiri ni utumwa,lakini pia unafuga hela kwa ya watu,wala huzitumii zote
Umemaliza kila kitu mkuu. Utajiri ni kama kutoa huduma kwa jamii (kama vile kutoa ajira kwa watu). Sio kwamba mwenye utajiri ananufaika nao kiviiile. Kwa mfano, mali zote anazomiliki Dangote hatazitumia zote. Mwisho wa siku ataondoka na kuwaacha familia na raia wengine wakifaidi.
 
Machaguo gani mkuu? Hivi unajua magonjwa mengi ya mifumo ya maisha kama vile kidney failure yanawapata matajiri na chanzo kikuu ni huo uhuru wa machaguo? Ukiwa na ufinyu wa machaguo, hio ndiyo furaha ya maisha hapa duniani mkuu.
Umezungumzia magonjwa mfano kidney failure, wagonjwa wengi wa huo ugonjwa ni wa Hali ya chini na wa kipato cha Kati na wengi wanakufa vijana kabisa, nenda hospitali zote Fanya utafiti...Maskini wengi ndio wanaongoza kuumwa siku hizi maana chochote kinachokuja mbele anapita nacho maana Hana kingine kizuri cha kuchagua, mfano Tajiri anaweza kununua chochote kile kwaajili ya afya Yake but maskini ananunua ilimradi maana pesa ni ndogo, angalia ulaji wa watu maskini utagundua Hilo, Leo hii angalia maskini wenye umri kama wa bakhresa wengi walishakufa au wako kitandani kutembea pia hawawezi....
 
Utafiti unaonyesha masikini kila siku anatenga masaa mawili au matatu ya kujifungia chumbani na kuanza kulia huku akimlaumu mungu pamoja na wazazi kwa kumleta duniani🤣🤣🤣🤣🤣
 
Utafiti unaonyesha masikini kila siku anatenga masaa mawili au matatu ya kujifungia chumbani na kuanza kulia huku akimlaumu mungu pamoja na wazazi kwa kumleta duniani🤣🤣🤣🤣🤣
Utafiti wa wapi huu tena mkuu?😂🤣😂🤣
 
MAONI YANGU
Mstari unaotenganisha furaha kati ya maskini na tajiri ni mwembamba sana. Kwa hiyo, hakuna haja ya kujitesa kusaka utajiri hadi ukashindwa kutumia muda mchache ulio nao hapa duniani kufurahia maisha. Ninaposema kufurahia maisha simaanishi kutumia pesa bali namaanisha kuishi stress-free life, hata kama hauna kitu.

Nawasilisha.
​
Umeandika mada yako na mwisho ukajijibu.

Kwamba kuna mstari unaotenganisha furaha ya tajiri na masikini.

Uwepo wa mstari tu ni tofauti kubwa mno. Jitahidi hiyo furaha kidogo uipate wakati una hela.

Hivi unaujua umaskini wewe? Kuna umasikini unaonekana kwa macho ya NYAMA kabsa hakuna haja ya kutumia hesabu.

Katika moslow law kuna stage mbalimbali za binadamu na kote huko ukivuka stage moja kwenda nyingine unahitaji uende zaidi.

Nikuambie tu hakuna sifa ya kuwa masikini.

Na mwisho wa siku tukuulize FURAHA ni nini? Furaha gani inapatikana bila hela?
 
Mkuu umeongea vema lakini hujamaliza. Mm nimesema mstari unaotenganisha umaskini na utajiri ni mwembamba sana. Ni kama vile haupo kabisa. Hebu rudia kunisoma tena.
 
Tajiri ni nani?

Utajiri ni nini?
Utajiri na umaskini ni subjective terms mkuu. Kila mtu anatafsiri umaskini na utajiri kwa vigezo vyake. Hakuna kipimio halisi. Hata MO akijilinganisha na Elon Musk anajiona ni maskini wa kutupwa!
 
Ngoja niingie kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Nikitazama maisha wanayoishi matajiri nikalinganisha na maisha wanayoishi maskini, nashindwa kuona tofauti ya kimsingi iliyopo kati yao.

Fikiria matajiri kama Dangote, MO29 au Bakhressa wanamiliki utajiri uliotapakaa nchi nzima na baadhi ya nchi za Afrika na dunia lakini kila siku wanaamka mapema na kuumiza vichwa kuendelea kukuza utajiri wao. Wakati Dangote tayari yupo kileleni mwa Afrika, akina Bakhressa na wenzake kila siku wanakuna kichwa jinsi ya kuongeza juhudi za kibiashara ili kumfikia na hata kumpita Dangote. Ni kama vile wanakimbia mbio za utajiri na kila mwaka Forbes wanatoa orodha kuonyesha nani kapanda au kushuka kwenye chati ya utajiri.

Na kibaya zaidi hata hawa matajiri sio rahisi kuwasaidia maskini. Mtu anamiliki maghorofa 20 Kariakoo yenye mamia ya vyumba lakini kati ya hayo maghorofa analala ndani chumba kimoja kilichopo kwenye ghorofa moja tu! Bakhressa, kwa mfano, anamiliki magari yametapakaa nchi nzima, hata yeye mwenyewe hajui idadi ya hayo magari. Naye anakutana nayo tu njiani anaona yameandikwa jina lake, wala hajui yalinunuliwa lini na meneja yupi! Lakini kati ya hayo magari yote anatumia gari moja tu, tena la bei ya kawaida.

Ukiangalia ratiba ya matajiri, unagundua kabisa kuwa wanaishi maisha yenye presha na stress kubwa hapa duniani licha ya kuwa wanamiliki mali lukuki. Tajiri anaamka saa 10 usiku kila siku ya juma na kulala saa 8 usiku. Ina maana analala kwa saa 2 tu kila siku! Taabu yote hii anayopata kisa anasaka utajiri. Kwa siku moja tajiri anatengeneza faida sio chini ya Tsh 500,000,000 katika mkusanyiko wa biashara zake zote lakini matumizi yake kwa siku hayapindukii Tsh 200,000, tena kwa kujinyima kweli kweli.

Unamkuta tajiri mkubwa anamiliki utajiri ambao yeye na ukoo wake mzima wanaweza kuutumia kwa miaka 80 bila kufanya kazi yoyote, lakini kila siku yupo busy anakusanya hela zaidi. What for? Kwanini mtu ujitese kiasi hiki kwa sababu ya kutafuta umaarufu kwenye chati ya Forbes wakati unaweza ukalala usifanye kazi na bado mambo yako yako na ukoo wako mzima yakaenda bila shida?

Kwa hali kama hii, ndipo ninaona ni afadhali tu mtu kuishi maisha ya kawaida ya kukuwezesha kupata mahali pa kulala na kupata milo 3 kwa siku badala ya kuumiza kichwa kutafuta utajiri wa sifa. Mtu ana utajiri umetapakaa nchi nzima lakini utakuta ndugu zake wanaishi katika umaskini wa kutupwa! Au utajiri unaambatana na ushetani ndani yake jamani?

MAONI YANGU
Mstari unaotenganisha furaha kati ya maskini na tajiri ni mwembamba sana. Kwa hiyo, hakuna haja ya kujitesa kusaka utajiri hadi ukashindwa kutumia muda mchache ulio nao hapa duniani kufurahia maisha. Ninaposema kufurahia maisha simaanishi kutumia pesa bali namaanisha kuishi stress-free life, hata kama hauna kitu.

Nawasilisha.
​
Dangote ana options nyingi sana ambazo mtu masikini hana. Mambo yote yanayoweza kutatuliwa na pesa Dangote ana options zaidi ya mtu masikini.

Hata hayo maisha ya ku hustle kuongeza utajiri ni option tu. Akiamua anaweza kuuza biashara zake akastaafu na kuishi maisha simple. Au hata maisha yasiyo simple.

Kuna watu hata chakula na sehemu ya kukaa tu ni tabu hao hawana options nyingi alizo nazo Dangote.
 
Maisha yanakuwa rahisi kivipi mkuu? Unadhani matajiri wanaishi maisha ya furaha hapa duniani? Wana stress kama zote mkuu. Tajiri analala kwa saa 2 tu kila siku maisha yake yapo rahisi kivipi?
Yanakuwa rahisi kwamba ukiamua kulala unalala ukiwa na ukwasi.
 
Back
Top Bottom