Kuna faida gani kuwa tajiri?

Kuna faida gani kuwa tajiri?

Sasa ikiwa tajiri kama MO29 hawezi kulala awasubiri mameneja wake wamfanyie kazi na kumletea ripoti, utajiri wake una manufaa gani kwake?
Zile email karibia Mia nne ambazo zinaingia kwa siku ndio report ambazo analetewa yeye huzipitia.

Au wewe unataka matajir walale au wakar nyumbani muda wote?
 
Utajiri ni nini?

Hakuna sifa ya kua masikini umasikini sio sifa sio kitu unaweza kusimama ukawa proud

Utajiri ni sifa
Sifa ya kwanza ni kumiliki kila mtu anatamani kua mmiliki

Tajiri atakula anachotaka sio kilichopatikana

Tajiri ana uhakika wa kutibiwa kama akiumwa huku maskini mda mwingine ikimlazimu kusubiri kifo bila hata jitihada yoyote kufanyika Nk....

Narudia umasikini sio sifa
Umasikini una dhalilisha

Tajiri akiwa na stress atajitoa out atakunywa wine huku anapigwa kiyoyozi
Huku maskini akiwa na majanga analia huku anapuliza moto kuni haziwaki maana zilinyeshwlewa na mvua😢
Kamasi linatililika 😅😅
 
Watu wanaoenjoy zaidi duniani ni upper middle income people
Wana uchumi wa kuhudumia familia zao, kufanya vacation nchi yoyote wakitaka, kwenda restaurants nzuri, hotels na pia responsibilities chache

Pia hata hao mabilionea wapo wanaoenjoy sana. Mfano Lei Jun anayemiliki kampuni ya simu ya Kichina "Xiaomi", alikuwa mtu mwenye interest na computer since kitambo sana, sasahivi amebuild company yake na yeye ndio CEO, mawazo yake yanacome true, ni lazima awe na furaha
 
Suala sio pesa, pesa ni chombo tu cha kuyapata mamlaka. Mamlaka ni ule uwezo wa kuyaathiri maisha ya watu wasiokujua.

Umeelezea aina ya matajiri wanaopenda kushikilia mamlaka. Wanapambana kupanua biashara zao ili wamiliki minyororo mizima ya thamani ambapo watu na hata serikali watawategemea.

Ukiwauliza watasema wana "saidia watu", wana "wekeza", wanajenga "legacy". Wanajipa umuhimu(sio kwa maana mbaya), wanaamini dunia bila wao haiwezekani.

Nafikiri mahusiano yaliyopo kati ya wanadamu na mamlaka ni magumu, yapo kisaikolojia zaidi.

Wapo matajiri ambao wameridhika na walichonacho wanajilia pole pole tena kwa kujificha.
Hakuna faida ila inabidi uwe nao tu!
 
Watu wanaoenjoy zaidi duniani ni upper middle income people
Wana uchumi wa kuhudumia familia zao, kufanya vacation nchi yoyote wakitaka, kwenda restaurants nzuri, hotels na pia responsibilities chache

Pia hata hao mabilionea wapo wanaoenjoy sana. Mfano Lei Jun anayemiliki kampuni ya simu ya Kichina "Xiaomi", alikuwa mtu mwenye interest na computer since kitambo sana, sasahivi amebuild company yake na yeye ndio CEO, mawazo yake yanacome true, ni lazima awe na furaha
Kweli kabisa mkuu. Ndio maana wahenga walisema "too much of something is harmful". Matajiri wakubwa wanaishi kwa taabu sana hapa duniani.
 
Ngoja niingie kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Nikitazama maisha wanayoishi matajiri nikalinganisha na maisha wanayoishi maskini, nashindwa kuona tofauti ya kimsingi iliyopo kati yao.

Fikiria matajiri kama Dangote, MO29 au Bakhressa wanamiliki utajiri uliotapakaa nchi nzima na baadhi ya nchi za Afrika na dunia lakini kila siku wanaamka mapema na kuumiza vichwa kuendelea kukuza utajiri wao. Wakati Dangote tayari yupo kileleni mwa Afrika, akina Bakhressa na wenzake kila siku wanakuna kichwa jinsi ya kuongeza juhudi za kibiashara ili kumfikia na hata kumpita Dangote. Ni kama vile wanakimbia mbio za utajiri na kila mwaka Forbes wanatoa orodha kuonyesha nani kapanda au kushuka kwenye chati ya utajiri.

Na kibaya zaidi hata hawa matajiri sio rahisi kuwasaidia maskini. Mtu anamiliki maghorofa 20 Kariakoo yenye mamia ya vyumba lakini kati ya hayo maghorofa analala ndani chumba kimoja kilichopo kwenye ghorofa moja tu! Bakhressa, kwa mfano, anamiliki magari yametapakaa nchi nzima, hata yeye mwenyewe hajui idadi ya hayo magari. Naye anakutana nayo tu njiani anaona yameandikwa jina lake, wala hajui yalinunuliwa lini na meneja yupi! Lakini kati ya hayo magari yote anatumia gari moja tu, tena la bei ya kawaida.

Ukiangalia ratiba ya matajiri, unagundua kabisa kuwa wanaishi maisha yenye presha na stress kubwa hapa duniani licha ya kuwa wanamiliki mali lukuki. Tajiri anaamka saa 10 usiku kila siku ya juma na kulala saa 8 usiku. Ina maana analala kwa saa 2 tu kila siku! Taabu yote hii anayopata kisa anasaka utajiri. Kwa siku moja tajiri anatengeneza faida sio chini ya Tsh 500,000,000 katika mkusanyiko wa biashara zake zote lakini matumizi yake kwa siku hayapindukii Tsh 200,000, tena kwa kujinyima kweli kweli.

Unamkuta tajiri mkubwa anamiliki utajiri ambao yeye na ukoo wake mzima wanaweza kuutumia kwa miaka 80 bila kufanya kazi yoyote, lakini kila siku yupo busy anakusanya hela zaidi. What for? Kwanini mtu ujitese kiasi hiki kwa sababu ya kutafuta umaarufu kwenye chati ya Forbes wakati unaweza ukalala usifanye kazi na bado mambo yako yako na ukoo wako mzima yakaenda bila shida?

Kwa hali kama hii, ndipo ninaona ni afadhali tu mtu kuishi maisha ya kawaida ya kukuwezesha kupata mahali pa kulala na kupata milo 3 kwa siku badala ya kuumiza kichwa kutafuta utajiri wa sifa. Mtu ana utajiri umetapakaa nchi nzima lakini utakuta ndugu zake wanaishi katika umaskini wa kutupwa! Au utajiri unaambatana na ushetani ndani yake jamani?

MAONI YANGU
Mstari unaotenganisha furaha kati ya maskini na tajiri ni mwembamba sana. Kwa hiyo, hakuna haja ya kujitesa kusaka utajiri hadi ukashindwa kutumia muda mchache ulio nao hapa duniani kufurahia maisha. Ninaposema kufurahia maisha simaanishi kutumia pesa bali namaanisha kuishi stress-free life, hata kama hauna kitu.

Nawasilisha.
​
Fanya kazi kijana upate pesa za kuwa tajiri ,usipofanya kazi unakuwa huna tofauti na nyumbu.

Raha ya Utajiri ni kuajiri watu wanaokutegemea na kukupambania kama wewe.

Kwanza Tajiri anafanyiwa kazi sio yeye kufanya,yeye anafanya maamuzi ni kama Rais alivyo.
 
Maisha yanakuwa rahisi kivipi mkuu? Unadhani matajiri wanaishi maisha ya furaha hapa duniani? Wana stress kama zote mkuu. Tajiri analala kwa saa 2 tu kila siku maisha yake yapo rahisi kivipi?
Tofautisha stress za njaa,ugonjwa au kufiwa na hela huna vs stress za kuogopa hasara au kushuka kiuchumi ukose Heshima.
 
Back
Top Bottom