Kuna faida gani kuwa tajiri?

Kuna faida gani kuwa tajiri?

Suala sio pesa, pesa ni chombo tu cha kuyapata mamlaka. Mamlaka ni ule uwezo wa kuyaathiri maisha ya watu wasiokujua.

Umeelezea aina ya matajiri wanaopenda kushikilia mamlaka. Wanapambana kupanua biashara zao ili wamiliki minyororo mizima ya thamani ambapo watu na hata serikali watawategemea.

Ukiwauliza watasema wana "saidia watu", wana "wekeza", wanajenga "legacy". Wanajipa umuhimu(sio kwa maana mbaya), wanaamini dunia bila wao haiwezekani.

Nafikiri mahusiano yaliyopo kati ya wanadamu na mamlaka ni magumu, yapo kisaikolojia zaidi.

Wapo matajiri ambao wameridhika na walichonacho wanajilia pole pole tena kwa kujificha.
 
Ngoja niingie kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Nikitazama maisha wanayoishi matajiri nikalinganisha na maisha wanayoishi maskini, nashindwa kuona tofauti ya kimsingi iliyopo kati yao.

Fikiria matajiri kama Dangote, MO29 au Bakhressa wanamiliki utajiri uliotapakaa nchi nzima na baadhi ya nchi za Afrika na dunia lakini kila siku wanaamka mapema na kuumiza vichwa kuendelea kukuza utajiri wao. Wakati Dangote tayari yupo kileleni mwa Afrika, akina Bakhressa na wenzake kila siku wanakuna kichwa jinsi ya kuongeza juhudi za kibiashara ili kumfikia na hata kumpita Dangote. Ni kama vile wanakimbia mbio za utajiri na kila mwaka Forbes wanatoa orodha kuonyesha nani kapanda au kushuka kwenye chati ya utajiri.

Na kibaya zaidi hata hawa matajiri sio rahisi kuwasaidia maskini. Mtu anamiliki maghorofa 20 Kariakoo yenye mamia ya vyumba lakini kati ya hayo maghorofa analala ndani chumba kimoja kilichopo kwenye ghorofa moja tu! Bakhressa, kwa mfano, anamiliki magari yametapakaa nchi nzima, hata yeye mwenyewe hajui idadi ya hayo magari. Naye anakutana nayo tu njiani anaona yameandikwa jina lake, wala hajui yalinunuliwa lini na meneja yupi! Lakini kati ya hayo magari yote anatumia gari moja tu, tena la bei ya kawaida.

Ukiangalia ratiba ya matajiri, unagundua kabisa kuwa wanaishi maisha yenye presha na stress kubwa hapa duniani licha ya kuwa wanamiliki mali lukuki. Tajiri anaamka saa 10 usiku kila siku ya juma na kulala saa 8 usiku. Ina maana analala kwa saa 2 tu kila siku! Taabu yote hii anayopata kisa anasaka utajiri. Kwa siku moja tajiri anatengeneza faida sio chini ya Tsh 500,000,000 katika mkusanyiko wa biashara zake zote lakini matumizi yake kwa siku hayapindukii Tsh 200,000, tena kwa kujinyima kweli kweli.

Unamkuta tajiri mkubwa anamiliki utajiri ambao yeye na ukoo wake mzima wanaweza kuutumia kwa miaka 80 bila kufanya kazi yoyote, lakini kila siku yupo busy anakusanya hela zaidi. What for? Kwanini mtu ujitese kiasi hiki kwa sababu ya kutafuta umaarufu kwenye chati ya Forbes wakati unaweza ukalala usifanye kazi na bado mambo yako yako na ukoo wako mzima yakaenda bila shida?

Kwa hali kama hii, ndipo ninaona ni afadhali tu mtu kuishi maisha ya kawaida ya kukuwezesha kupata mahali pa kulala na kupata milo 3 kwa siku badala ya kuumiza kichwa kutafuta utajiri wa sifa. Mtu ana utajiri umetapakaa nchi nzima lakini utakuta ndugu zake wanaishi katika umaskini wa kutupwa! Au utajiri unaambatana na ushetani ndani yake jamani?

MAONI YANGU
Mstari unaotenganisha furaha kati ya maskini na tajiri ni mwembamba sana. Kwa hiyo, hakuna haja ya kujitesa kusaka utajiri hadi ukashindwa kutumia muda mchache ulio nao hapa duniani kufurahia maisha. Ninaposema kufurahia maisha simaanishi kutumia pesa bali namaanisha kuishi stress-free life, hata kama hauna kitu.

Nawasilisha.
​
There is no Nobility in Poverty.
Utajiri una faida kubwa kuliko umasikini, na utajiri siyo kuwa na mapesa mengi na kukosa furaha au muda wa kuenjoy maisha, huo ni umasikni hata kama utakuwa Bilionea.

Utajiri mkubwa kuliko wote ni ule wa kuweza kujikidhi kila kitu unachokihitaji pamoja na kupata mda wa kufurahia maisha.
 
Sio matajiri wote wana shida kama hizo unazozisema,kuna watu tayar wana ukwasi wa kutosha na wao wamekaa pembeni wamewaachia watu wengine wanaendesha makampuni

Kwahiyo hiyo ratiba uliyoisema sio kwamba ndio utaratibu wa matajiri wote

MO huamka asubuhi kuswali na kufanya mazoezi,saa tatu huenda ofisini kama kumbukumbu zangu zipo vizur, sasa sita husoma au hupitia email kama Mia nne hivi,saa tisa huenda kulala for two hours

Huo ni mfano mmoja tu,naamini ukienda kwa Bhakhresa nae atakuwa na ratiba yake

Swala la kusaidia watu au wenye uhitaji ni swala binafsi,sio matajir wote huwa wanatangaza Tema hawa wenye imani zao,hufanya mambo yao kimya kimya
Sasa ikiwa tajiri kama MO29 hawezi kulala awasubiri mameneja wake wamfanyie kazi na kumletea ripoti, utajiri wake una manufaa gani kwake?
 
There is no Nobility in Poverty.
Utajiri una faida kubwa kuliko umasikini, na utajiri siyo kuwa na mapesa mengi na kukosa furaha au muda wa kuenjoy maisha, huo ni umasikni hata kama utakuwa Bilionea.

Utajiri mkubwa kuliko wote ni ule wa kuweza kujikidhi kila kitu unachokihitaji pamoja na kupata mda wa kufurahia maisha.
Tupo pamoja mkuu. Nami hiki ndicho ninachosema. Mtu kama Mengi amefariki akiwa 75 yrs old kwa sababu ya stress za kusaka pesa na kuuacha utajiri wote hapa duniani watu wanagawana. Haina maana kuwa tajiri mkubwa halafu unakosa raha hapa duniani. Ni afadhali kuwa mtu masikini anayeridhika na maisha yoyote anayoishi.
 
Ngoja niingie kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Nikitazama maisha wanayoishi matajiri nikalinganisha na maisha wanayoishi maskini, nashindwa kuona tofauti ya kimsingi iliyopo kati yao.

Fikiria matajiri kama Dangote, MO29 au Bakhressa wanamiliki utajiri uliotapakaa nchi nzima na baadhi ya nchi za Afrika na dunia lakini kila siku wanaamka mapema na kuumiza vichwa kuendelea kukuza utajiri wao. Wakati Dangote tayari yupo kileleni mwa Afrika, akina Bakhressa na wenzake kila siku wanakuna kichwa jinsi ya kuongeza juhudi za kibiashara ili kumfikia na hata kumpita Dangote. Ni kama vile wanakimbia mbio za utajiri na kila mwaka Forbes wanatoa orodha kuonyesha nani kapanda au kushuka kwenye chati ya utajiri.

Na kibaya zaidi hata hawa matajiri sio rahisi kuwasaidia maskini. Mtu anamiliki maghorofa 20 Kariakoo yenye mamia ya vyumba lakini kati ya hayo maghorofa analala ndani chumba kimoja kilichopo kwenye ghorofa moja tu! Bakhressa, kwa mfano, anamiliki magari yametapakaa nchi nzima, hata yeye mwenyewe hajui idadi ya hayo magari. Naye anakutana nayo tu njiani anaona yameandikwa jina lake, wala hajui yalinunuliwa lini na meneja yupi! Lakini kati ya hayo magari yote anatumia gari moja tu, tena la bei ya kawaida.

Ukiangalia ratiba ya matajiri, unagundua kabisa kuwa wanaishi maisha yenye presha na stress kubwa hapa duniani licha ya kuwa wanamiliki mali lukuki. Tajiri anaamka saa 10 usiku kila siku ya juma na kulala saa 8 usiku. Ina maana analala kwa saa 2 tu kila siku! Taabu yote hii anayopata kisa anasaka utajiri. Kwa siku moja tajiri anatengeneza faida sio chini ya Tsh 500,000,000 katika mkusanyiko wa biashara zake zote lakini matumizi yake kwa siku hayapindukii Tsh 200,000, tena kwa kujinyima kweli kweli.

Unamkuta tajiri mkubwa anamiliki utajiri ambao yeye na ukoo wake mzima wanaweza kuutumia kwa miaka 80 bila kufanya kazi yoyote, lakini kila siku yupo busy anakusanya hela zaidi. What for? Kwanini mtu ujitese kiasi hiki kwa sababu ya kutafuta umaarufu kwenye chati ya Forbes wakati unaweza ukalala usifanye kazi na bado mambo yako yako na ukoo wako mzima yakaenda bila shida?

Kwa hali kama hii, ndipo ninaona ni afadhali tu mtu kuishi maisha ya kawaida ya kukuwezesha kupata mahali pa kulala na kupata milo 3 kwa siku badala ya kuumiza kichwa kutafuta utajiri wa sifa. Mtu ana utajiri umetapakaa nchi nzima lakini utakuta ndugu zake wanaishi katika umaskini wa kutupwa! Au utajiri unaambatana na ushetani ndani yake jamani?

MAONI YANGU
Mstari unaotenganisha furaha kati ya maskini na tajiri ni mwembamba sana. Kwa hiyo, hakuna haja ya kujitesa kusaka utajiri hadi ukashindwa kutumia muda mchache ulio nao hapa duniani kufurahia maisha. Ninaposema kufurahia maisha simaanishi kutumia pesa bali namaanisha kuishi stress-free life, hata kama hauna kitu.

Nawasilisha.
​
Umasikini ni laana!
 
Back
Top Bottom