Kuna faida gani kuwa tajiri?

Kuna faida gani kuwa tajiri?

Nilishawah kuwa tajir nikaporomoka kiufup ni stress mikopo bank, wafanyakaz kudai mishahara, majambaz kukuwinda wakuteke, nilinusulika kifo mara tatu kwa kuwekewa sumu na wafanyabiashara wenzangu kisa ushindani,ukipita sehem unataka ununue japo karanga za jero unahofia some time unamiss kukaa kucheza draft unakuta watu wanakuheshimu mpaka nilikuwa naboeka nyie maskin msio wahi miliki hata milion 200 bank hamuwez kumuelewa mtoa mada ila kiufup hakikisha unakula vizur nk hz level za kumilik wafanyakaz hata 50 ni stress sana
Mkuu umemaliza kila kitu. Tusubiri wanazi waje kubisha na kuponda.
 
Maisha yanakuwa rahisi kivipi mkuu? Unadhani matajiri wanaishi maisha ya furaha hapa duniani? Wana stress kama zote mkuu. Tajiri analala kwa saa 2 tu kila siku maisha yake yapo rahisi kivipi?
''Tajiri analala kwa saa 2 tu"
Hapa ndipo uzi wako umegeuka kuwa porojo.
 
''Tajiri analala kwa saa 2 tu"
Hapa ndipo uzi wako umegeuka kuwa porojo.
Kama analala saa 8 anaamka saa 10 hizo ni saa ngapi? Kama hiyo hesabu ni ngumu kwako, tumia calculator mkuu.
 
Ungeongelea umasikini kwakuwa ndo una experience nao ila unapoongelea utajiri hakuna unachoweza kukiongelea kwa usahihi hapo .
 
Maisha yanakuwa rahisi kivipi mkuu? Unadhani matajiri wanaishi maisha ya furaha hapa duniani? Wana stress kama zote mkuu. Tajiri analala kwa saa 2 tu kila siku maisha yake yapo rahisi kivipi?
Nafikiri sio sahihi kusema matajiri wote wana stress. Labda kama ungesema baadhi ningeweza kuelewa
 
Tupo pamoja mkuu. Nami hiki ndicho ninachosema. Mtu kama Mengi amefariki akiwa 75 yrs old kwa sababu ya stress za kusaka pesa na kuuacha utajiri wote hapa duniani watu wanagawana. Haina maana kuwa tajiri mkubwa halafu unakosa raha hapa duniani. Ni afadhali kuwa mtu masikini anayeridhika na maisha yoyote anayoishi.
Absolutely. Na maskini aliyeridhika na kila kitu, na anayepata hitaji la moyo, huyo ndiyo tajiri.
 
Ungeongelea umasikini kwakuwa ndo una experience nao ila unapoongelea utajiri hakuna unachoweza kukiongelea kwa usahihi hapo .
Ndio maana wewe mwenye experience ya utajiri upo ili utupe huo uzoefu mkuu.
 
Maisha yanakuwa rahisi kivipi mkuu? Unadhani matajiri wanaishi maisha ya furaha hapa duniani? Wana stress kama zote mkuu. Tajiri analala kwa saa 2 tu kila siku maisha yake yapo rahisi kivipi?
Thibitisha kuwa kuna tajiri analala saa 2 pekee kwa siku
 
Umesoma uzi au umesoma heading tu ukakurupuka kuja kutoa maoni mkuu?
Nimesoma uzi, unaelezea maisha ya matajiri ambao hujawahi kuishi nao, hujui ratiba zao, hujui vipato vyao n.k.

Wanakutana na kua na access na viongozi wakuu wa nchi wewe hilo huoni, wanauza bidhaa zao kwa uhuru, bila usumbufu, wanasiasa wako mfukoni, malighafi zao zinaingia na kutoka kwa tozo kiduchu wewe huoni, wanalipa mishahara midogo ili wawe matajiri zaidi wewe huoni.

Hawaishi kama masikini, systems zinawafanyia kazi, bila shaka uliamini maneno ya "Mo" kua sijui analala saa 4.

Mkuu makinika hawasemi yote hao, wanaishi maisha ya kifahari mno. Unateswa na kunguni ambao yeye hajui wanafafanaje.

Majuzijuzi Mo kamtambulisha mwanae kinda kabisa ambae bila shaka umemuacha parefu, anasimamia bisahara za familia..

TAFUTA PESA, UMASIKINI SIO SIFA NZURI.
 
Sijakataa kutafuta pesa bali ninachobainisha hapa ni hasara za utajiri mkuu.
 
Ngoja niingie kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Nikitazama maisha wanayoishi matajiri nikalinganisha na maisha wanayoishi maskini, nashindwa kuona tofauti ya kimsingi iliyopo kati yao.

Fikiria matajiri kama Dangote, MO29 au Bakhressa wanamiliki utajiri uliotapakaa nchi nzima na baadhi ya nchi za Afrika na dunia lakini kila siku wanaamka mapema na kuumiza vichwa kuendelea kukuza utajiri wao. Wakati Dangote tayari yupo kileleni mwa Afrika, akina Bakhressa na wenzake kila siku wanakuna kichwa jinsi ya kuongeza juhudi za kibiashara ili kumfikia na hata kumpita Dangote. Ni kama vile wanakimbia mbio za utajiri na kila mwaka Forbes wanatoa orodha kuonyesha nani kapanda au kushuka kwenye chati ya utajiri.

Na kibaya zaidi hata hawa matajiri sio rahisi kuwasaidia maskini. Mtu anamiliki maghorofa 20 Kariakoo yenye mamia ya vyumba lakini kati ya hayo maghorofa analala ndani chumba kimoja kilichopo kwenye ghorofa moja tu! Bakhressa, kwa mfano, anamiliki magari yametapakaa nchi nzima, hata yeye mwenyewe hajui idadi ya hayo magari. Naye anakutana nayo tu njiani anaona yameandikwa jina lake, wala hajui yalinunuliwa lini na meneja yupi! Lakini kati ya hayo magari yote anatumia gari moja tu, tena la bei ya kawaida.

Ukiangalia ratiba ya matajiri, unagundua kabisa kuwa wanaishi maisha yenye presha na stress kubwa hapa duniani licha ya kuwa wanamiliki mali lukuki. Tajiri anaamka saa 10 usiku kila siku ya juma na kulala saa 8 usiku. Ina maana analala kwa saa 2 tu kila siku! Taabu yote hii anayopata kisa anasaka utajiri. Kwa siku moja tajiri anatengeneza faida sio chini ya Tsh 500,000,000 katika mkusanyiko wa biashara zake zote lakini matumizi yake kwa siku hayapindukii Tsh 200,000, tena kwa kujinyima kweli kweli.

Unamkuta tajiri mkubwa anamiliki utajiri ambao yeye na ukoo wake mzima wanaweza kuutumia kwa miaka 80 bila kufanya kazi yoyote, lakini kila siku yupo busy anakusanya hela zaidi. What for? Kwanini mtu ujitese kiasi hiki kwa sababu ya kutafuta umaarufu kwenye chati ya Forbes wakati unaweza ukalala usifanye kazi na bado mambo yako yako na ukoo wako mzima yakaenda bila shida?

Kwa hali kama hii, ndipo ninaona ni afadhali tu mtu kuishi maisha ya kawaida ya kukuwezesha kupata mahali pa kulala na kupata milo 3 kwa siku badala ya kuumiza kichwa kutafuta utajiri wa sifa. Mtu ana utajiri umetapakaa nchi nzima lakini utakuta ndugu zake wanaishi katika umaskini wa kutupwa! Au utajiri unaambatana na ushetani ndani yake jamani?

MAONI YANGU
Mstari unaotenganisha furaha kati ya maskini na tajiri ni mwembamba sana. Kwa hiyo, hakuna haja ya kujitesa kusaka utajiri hadi ukashindwa kutumia muda mchache ulio nao hapa duniani kufurahia maisha. Ninaposema kufurahia maisha simaanishi kutumia pesa bali namaanisha kuishi stress-free life, hata kama hauna kitu.

Nawasilisha.
​
Kuna faida na pia hasara kwasababu roadmap to freedom kwenye maisha huletwa na utajiri.

Kwahiyo utajiri sometimes humpa mtu choices mbalimbali za kwenye maisha tofauti na umaskini ambao effect kubwa ipo kwenye shida.
 
Kivipi mkuu?
 
Back
Top Bottom