Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 21,773
- 57,241
Aliandika Mwanahabari Mkongwe, Edo Kumwembe
“Baada ya kifo Cha Huyu Sir Wicknel Chivayo nimeona baadhi ya watu wakipamba sana utajiri wake huku wengine wakimlinganisha na MO Dewji, aisee Inachekesha sana na pia ni kumvunjia heshima MO.
Mwanzoni mwa mwaka huu Forbes ilimtangaza Mo kufikia utajiri wa Dola Bilioni 2.1 ambayo ni sawa na Trillion 5.55 za kitanzania.
Huyu marehemu Chivayo amefariki akiwa na utajiri wa Dola milioni 100 ambayo ni sawa na Bilioni 264 Yani sawa na Trillion 0.264 (Yani Kwa kifupi alikuwa hajafika hata nusu ya Trillion Moja ya kitanzania)
Kwa lugha rahisi ni kwamba Chivayo utajiri wake wote ulikuwa una ingia mara 21 kwenye utajiri wa MO.
Tatizo watu wakimuona Yuko kwenye Ndege, anamiliki magari yenye majina yake wanamuona ni mtu mwenye pesa sana, ila Mtu kama MO anaye Miliki Range Rover yake Moja kwenda kazini Wana mchukulia rahisi.
Huyu MO utajiri wake unatisha sema siyo mtu wa kujionyesha, ni kumvunjia heshima kumlinganisha na Chivayo.”