Kuna faida gani kuwa tajiri?

Kuna faida gani kuwa tajiri?

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,195
Reaction score
27,811
Ngoja niingie kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Nikitazama maisha wanayoishi matajiri nikalinganisha na maisha wanayoishi maskini, nashindwa kuona tofauti ya kimsingi iliyopo kati yao.

Fikiria matajiri kama Dangote, MO29 au Bakhressa wanamiliki utajiri uliotapakaa nchi nzima na baadhi ya nchi za Afrika na dunia lakini kila siku wanaamka mapema na kuumiza vichwa kuendelea kukuza utajiri wao. Wakati Dangote tayari yupo kileleni mwa Afrika, akina Bakhressa na wenzake kila siku wanakuna kichwa jinsi ya kuongeza juhudi za kibiashara ili kumfikia na hata kumpita Dangote. Ni kama vile wanakimbia mbio za utajiri na kila mwaka Forbes wanatoa orodha kuonyesha nani kapanda au kushuka kwenye chati ya utajiri.

Na kibaya zaidi hata hawa matajiri sio rahisi kuwasaidia maskini. Mtu anamiliki maghorofa 20 Kariakoo yenye mamia ya vyumba lakini kati ya hayo maghorofa analala ndani chumba kimoja kilichopo kwenye ghorofa moja tu! Bakhressa, kwa mfano, anamiliki magari yametapakaa nchi nzima, hata yeye mwenyewe hajui idadi ya hayo magari. Naye anakutana nayo tu njiani anaona yameandikwa jina lake, wala hajui yalinunuliwa lini na meneja yupi! Lakini kati ya hayo magari yote anatumia gari moja tu, tena la bei ya kawaida.

Ukiangalia ratiba ya matajiri, unagundua kabisa kuwa wanaishi maisha yenye presha na stress kubwa hapa duniani licha ya kuwa wanamiliki mali lukuki. Tajiri anaamka saa 10 usiku kila siku ya juma na kulala saa 8 usiku. Ina maana analala kwa saa 2 tu kila siku! Taabu yote hii anayopata kisa anasaka utajiri. Kwa siku moja tajiri anatengeneza faida sio chini ya Tsh 500,000,000 katika mkusanyiko wa biashara zake zote lakini matumizi yake kwa siku hayapindukii Tsh 200,000, tena kwa kujinyima kweli kweli.

Unamkuta tajiri mkubwa anamiliki utajiri ambao yeye na ukoo wake mzima wanaweza kuutumia kwa miaka 80 bila kufanya kazi yoyote, lakini kila siku yupo busy anakusanya hela zaidi. What for? Kwanini mtu ujitese kiasi hiki kwa sababu ya kutafuta umaarufu kwenye chati ya Forbes wakati unaweza ukalala usifanye kazi na bado mambo yako yako na ukoo wako mzima yakaenda bila shida?

Kwa hali kama hii, ndipo ninaona ni afadhali tu mtu kuishi maisha ya kawaida ya kukuwezesha kupata mahali pa kulala na kupata milo 3 kwa siku badala ya kuumiza kichwa kutafuta utajiri wa sifa. Mtu ana utajiri umetapakaa nchi nzima lakini utakuta ndugu zake wanaishi katika umaskini wa kutupwa! Au utajiri unaambatana na ushetani ndani yake jamani?

MAONI YANGU
Mstari unaotenganisha furaha kati ya maskini na tajiri ni mwembamba sana. Kwa hiyo, hakuna haja ya kujitesa kusaka utajiri hadi ukashindwa kutumia muda mchache ulio nao hapa duniani kufurahia maisha. Ninaposema kufurahia maisha simaanishi kutumia pesa bali namaanisha kuishi stress-free life, hata kama hauna kitu.

Nawasilisha.
 
Bora Stress za kuwa tajiri kuliko Stress za Kuwa Masikini.
60c38127d5a48433ebcefcc8ed8e8751dcbf0733_2_476x500.jpeg
 
Sio matajiri wote wana shida kama hizo unazozisema,kuna watu tayar wana ukwasi wa kutosha na wao wamekaa pembeni wamewaachia watu wengine wanaendesha makampuni

Kwahiyo hiyo ratiba uliyoisema sio kwamba ndio utaratibu wa matajiri wote

MO huamka asubuhi kuswali na kufanya mazoezi,saa tatu huenda ofisini kama kumbukumbu zangu zipo vizur, sasa sita husoma au hupitia email kama Mia nne hivi,saa tisa huenda kulala for two hours

Huo ni mfano mmoja tu,naamini ukienda kwa Bhakhresa nae atakuwa na ratiba yake

Swala la kusaidia watu au wenye uhitaji ni swala binafsi,sio matajir wote huwa wanatangaza Tema hawa wenye imani zao,hufanya mambo yao kimya kimya
 
Hao matajiri wanatoa ajira kwa watu ambao bado hawajawa matajiri,

Kila tajiri akisema afunge biashara zake ili atumie hela zake tu mpaka kufa,ni familia ngapi zitateseka kwa kukosa ajira?

Wewe unaonekana una ubinafsi sana,hao matajiri wanatengeneza wealth generation ya vizazi na vizazi,hawajingalii tu wao kama wao.
 
Hao matajiri wanatoa ajira kwa watu ambao bado hawajawa matajiri,

Kila tajiri akisema afunge biashara zake ili atumie hela zake tu mpaka kufa,ni familia ngapi zitateseka kwa kukosa ajira?

Wewe unaonekana una ubinafsi sana,hao matajiri wanatengeneza wealth generation ya vizazi na vizazi,hawajingalii tu wao kama wao.
Ila matajiri wa arabuni ndio wanafaidi thamani ya utajiri wao , kule kuna watu wanaishi kifahari mno ,mpaka vikombe wana tumia vya dhahabu🤔
 
Kunasiku nilirudi nipo tungi.....🍺 basi watoto wangu walikua wamefunga shule wote wapo nyumbani with full of love and joy, sasa nikawa nawasimulia kwamba mimi sitamani kuwa tajiri lakini naomba Mungu anijaalie nisikose wala nisipungukiwe...🤗
 
Nilishawah kuwa tajir nikaporomoka kiufup ni stress mikopo bank, wafanyakaz kudai mishahara, majambaz kukuwinda wakuteke, nilinusulika kifo mara tatu kwa kuwekewa sumu na wafanyabiashara wenzangu kisa ushindani,ukipita sehem unataka ununue japo karanga za jero unahofia some time unamiss kukaa kucheza draft unakuta watu wanakuheshimu mpaka nilikuwa naboeka nyie maskin msio wahi miliki hata milion 200 bank hamuwez kumuelewa mtoa mada ila kiufup hakikisha unakula vizur nk hz level za kumilik wafanyakaz hata 50 ni stress sana
 
Back
Top Bottom