Kuna anaeutesa moyo wangu JF!

Kuna anaeutesa moyo wangu JF!

Pole binti,
Bora kajisemea ukweli lakini
Kuliko kukurusha rusha kama mpira wa kona.

Habari zenu waungwana ,Ni siku nyingine tena imeanza nikiwa na huzuni tele hasa baada ya kuuufunua moyo wangu na kupata haya majibu toka kwa mhusika ...(Niseme tu Kabila lake ni mchagga)
Nimepokea majibu kutoka kwa mhusika ,na ameomba sana nisimtaje ,kwani yeye na ubavu wake wote wako JF na PM wife anachungulia .
Anashukuru sana nimeweza kumwambia jambo hili,Anasikitika sana kwani nafasi yake iko full ingawa kasema amejisikia faraja kuona anapendeka yeye kama mwanaume ,anasikitika kwa hili na amesema hana uwezo wa kunisaidia ,nisife moyo kwani haya mambo hutokea katika maisha na mwisho wa siku nitamsahau ,otherwise ananitakia mafanikio mema katika maisha yangu ya Uraiani na JF kwa ujumla.
Mwisho wa kunukuu.
Nawashukuru wote mlionipa ,
Nalog off till further notice ..:A S embarassed:
 
Mdogo wangu mpendwa amani yamoyo aijua mwenye kuiona, najua inawezekana usemayo ni kweli kabisa wala si kuchangamsha jf lkn muombe Mungu pia kwani sukari ni tamu sana lkn ukiila sana inaleta ugonjwa mbaya wa kisukari, mithiri ya ukimwi utalazimika kuiacha kwahiyo kama yupo unaedhani anadondosha moyo wako basi mpe habari nakama na yy kamdondokea mwingine basi akikubali ajipange kusepa aliye mpenda muendelee na maisha, kwani amani huletwa na uvumilivu, kisha huja saburi na kazi ya saburi nibusara nakujua kumweka mwezio mbele kabla yako ili ajuekweli unampenda.
Be Blessed.
 
Mie nitapenda japo apite kwenye thread hii aone tu kama kuna mtu anahangaika kimawazo juu yake ...
nahisi nikimtumia PM anaweza kukaa kimya asiijibu ...

hebu kuwa mwanamke wa kweli mrembo and talk to him!sio lazima utafute pa kumweka ila just to let him know love is in the air.may be he feels the same bana!!
 
maneno matamu haya hakika mwente kuangukiwa laiti angejijua ingekuwa faraja ya moyo wake...
 
Sasa utaendelea kuumia mpaka lini jamani?? si bora umueleze ukweli ili ujue kama utampata au utamkosa kuliko kuutesa moyo wako. U neva know pengine na yeye anakupenda ila anaogopa kukueleza
 
Inaonesha umesharidhika na uwepo wake. Hii ni ile aina ya mapenzi inaitwa "Platonic love", yaani unapenda wewe tu wakati anayependwa masikin hata hajui. Pata ujasiri wa kufunguka zaidi kwake kama ambavyo wengine wamefunguka mwaka huu.
 
Usiniambie umekata tamaa bana! Vipi vigezo na masharti yake umefikisha? lol

Unajua kuna shida fulani ipo siku hizi, unapomuapproach mtu ni ngumu kuweza kujua kama yupo fully occupied kama hana pete ya ndoa au ana mtu ambaye hawezi kumpiga chini.

Tatizo linakujaje? Kila unapopiga sound hata mashairi yako yatakuwa na vina kiasi gani ni lazima afanye reflection na mtu aliyenaye kama umemzidi au laaah halafu ndiyo aje atoe maamuzi ya nifanye au laaah.

Kitu kingine naheshimu maamuzi ya mtu anapojieleza kwa hisia au kwa msisitizo kuwa jambo hilo unalolitaka halipo katika programe zake hata baada ya kumueleza. Haimanishi ana dharau kwa kukuambia hivyo bali huo ndiyo msimamo wake. Inabidi kama mstaarabu uvute pumzi kama kutatokea majaaliwa mbele ya safari ni Mungu ajuaye lakini score board itakuwa inasoma 2 - 1 mpaka 90min na kipyenga kinakaribia kupulizwa kuashiria mpambano kuisha.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom