Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,694
- 40,720
Sasa msianze kunirukia na kunishadadia kwa kusema mtu ana sura ya kiatu wakati kiatu chenyewe ninachokizungumzia wala hamkijui. Labda chaweza kuwa kile cha ‘ko-ko-ko' au vile vya ngozi vyenye shingo ndefu ambavyo dada mwenye "usafiri" mzuri akivitinga anaonekana kama Bi. Condi Rice akiteremka kwenye lile jigede la Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani! Hapana si hivyo ninavyovizungumzia. Na siyo vile vya kuchomeka ambavyo vinaonesha mguu mzima isipokuwa vidole, nyayo na kisigino.
Dada ninayemzungumzia sura yake ilikuwa kama Kandambili. Sasa kuna kandambili nyingi nzuri, za rangi rangi, na zinapendeza. Hapana, yeye sura yake ilikuwa siyo ya kandambili tulizozizoea. Sura yake hasa ilikuwa ni kama ya malapa. Sasa malapa yenyewe ninayoyazungumzia ambayo yamefanana na sura ya dada huyo kwa kweli siyo yale unayoweza kwenda kwenye duka la Mwarabu au hata duka la "Viatu Bora" ukayapata. Hapana. Sura yake imefanana na viatu aina ya kandambili ambazo hujulikana kama malapa, na malapa yenyewe yanaitwa Makubanzi!
Kwa wale ambao hamjui makubanzi ni viatu vya aina gani nitawasaidia kidogo. Makubanzi huvaliwa sana na Wamasai na watu wa bara zaidi na miaka ile ya hali ngumu ya uchumi, wakati wa dona la Yanga! Yalikuwa yanavaliwa na watanzania wengi bila ya kujali vyeo vyao na hadhi yao ya maisha. Makubanzi hutengenezwa kutokana na mabaki ya magurudumu ya gari ambayo hukatwa kwa mtindo wa kandambili na hugongelewa vimisumari vidogo vidogo na hutengenezwa kwa kila aina ya mtindo.
Sifa kubwa ya makubanzi ni kuwa hudumu kwa muda mrefu sana. Wewe ukichakaza makubanzi basi wewe ni mtembezi kweli. Tatizo kubwa hata hivyo la makubanzi ni kuwa, kukiwa na jua kali, havifai kwani vinaunguza utadhani umeweka miguu kwenye mafiga ya moto wa kuni. Licha ya sifa zake nzuri, makubanzi hayaangaliki. Ni meusi, yanatisha, na wakati mwingine ukiyaangalia sana utadhani yanakukodelea macho. Kwa vile makubanzi hayana rangi nyingine isipokuwa nyeusi, basi yanaficha mambo mengi sana. Hata hivyo, wakati wa shida na raha, makubanzi ni rafiki wa watu wengi sana. Irena, sura yake ilikuwa kama ya makubanzi kwani ukiingalia unapatwa na ganzi ya macho, na kigugumizi cha akili.
Najua una hamu ya kujua kwanini naandika kuhusu Irena. Ukweli ni kuwa katika maisha yangu yote (na mvi zinashuhudia kuwa nimeishi kwingi) sijawahi kumpenda mwanamke kama nilivyowahi kumpenda Irena kwa muda mfupi tuliowahi kuwa pamoja. Bila ya shaka umekenua meno, na taya lako limedongoka, huku ute ukining'inia kunishangaa iweje mimi Mwanakijiji nimpende mwanamke mwenye sura ya kiatu kilichojaa kunyanzi kama makubanzi.
Nitakupa jibu, ila kwanza chukua kigoda, keti pembeni, acha kuparua huo mtandao, na sikiliza kwa makini kisa changu na Irena. Kama una kiu, karibu togwa, na kama si mpenzi wa togwa basi karibu mirinda na fanta (ulanzi umeisha) na kama huviwezi hivyo kwani ni laini kwako, basi karibu Konyagi ya Kinyumbani (wenyewe twaiita Gongo). Nitakusimulia kisa chenyewe basi ukiacha kucheka cheka kwa vile nimekukumbusha nyumbani karibu na kwa yule mama muuza Gongo, mwenye mtambo wa gongo uliobuniwa, kuundwa, na kutengenezwa na mlevi mmoja hivi toka JWTZ!
Nilikutana na Irena mwaka 2001 wakati naenda nyumbani likizo ya Krismasi. Mimi niliunganisha ndege pale Heathrow Uingereza. Niliingia kwenye ndege hiyo ya KLM Lufthansa nikiwa nimechoka, mkononi nikiwa nimebeba kikompyuta changu kwenye begi lake. Nilipoketi kwenye ile seti hakukuwa na mtu mwingine, nikashukuru Mungu kuwa nitapata nafasi ya kujisomea angalau kitabu kimoja na kusinzia vizuri bila mtu kunikoromea. Wala sikupata nafasi ya kufurahia mawazo hayo, kwani yalikatishwa na mtu ambaye aliketi kwenye ile nafasi ya kulia iliyokuwa wazi.
Kwa kuangalia kwa haraka sikujua kama alikuwa ni mwanamme au mwanamme, kwani alikuwa amevalia koti, shati, suruali na kofia. Huyo mtu alikuwa mweusi wa mpingo. Kwa vile hakusema kitu, na mimi sikusema kitu, nilidhania labda jamaa ni mjaluo au Mnigeria fulani anayeenda pande za Afrika ya Mashariki.
Baada ya kama saa moja ya safari, yule mtu ndipo alipovua kofia yake ili aweze kujilaza vizuri kwenye kiti chake. Hata alipovua kofia sikuweza kujua kama ni mwanamke au mwanamme. Nilijisikia vibaya kweli kwani udadisi ulianza kunizidia. Nikaamua kumsemesha kwa kimombo na kumuuliza hali yake. Aliponijibu ndipo nilijikuta nimepigwa na bumbuwazi. Sijawahi kusikia sauti nyororo kama ya dada huyo, ilikuwa ni sauti ya chiriku masikioni mwangu, naapa ningeweza kubembelezwa hadi kulala nikimsikiliza dada huyo akinisomea hadithi za Bulicheka na zile za Alfu Lela Ulela!
"Where are you heading" Nilimuuliza nikidadisi safari yake ni kwenda wapi ili kuvunja ubaridi na ukimya uliokuwa kati yetu.
"I'm going home to Tanzania" Alinijibu kwa furaha huku macho yake meupe yaliyojificha kwenye uso mweusi utadhania mtu aneyechungulia gizani yakingara kwa hamasa. Kama umewahi kuona paka mweusi akichungulia gizani, basi ndo dada huyo alivyoonekana.
Ndipo nilipogundua kuwa yeye ni Mtanzania, na tukaamua kubadili lugha na kuanza kutumia Kiswahili. Tulizungumza mambo mbalimbali, huku nikijikuta siwezi kumuangalia usoni, ila sikutamani aache kuzungumza kwani sauti yake ilikuwa ni kama ya malaika!! Vionjo na hisia zangu vilikuwa vimechanganyikiwa utadhania mtu amenizungusha kama pia na kuniachilia nisijue wapi pa kuelekea bali nikabakia kuyumba yumba utadhani mlevi pale Mgandini. Upande mmoja nilijisikia vibaya sana kumuona ana sura mbaya, upande mwingine nilijua navutiwa na dada huyo kuliko nilivyowahi kuvutiwa na mwanamke yoyote kabla yake. Hicho ndio waswahili wanakiita kisongombingo na wengine wanasema ni kasheshe.
Kwa vile nimewahi kuona mengi humu duniani, basi nilijikaza kisabuni na nikaamua kuyavulia maji nguo. Tuliendelea kuzungumza mambo mengi, alinijulisha kuwa alikuwa anarudi nyumbani toka Uswisi alikokuwa akifanya kazi katika Shirika la Afya la Dunia (WHO) na mkataba wake umeisha na anarudi kimoja. Pole pole nilianza kumzoea lakini kabla hatujazungumza sana tulishakuwa angani kwa karibu masaa matatu na watu walianza kupiga usingizi.
Irena, alianza kupiga miayo na kufikicha macho, na haikumchukua muda mrefu na yeye akasinzia. Aliniacha nikiwa na mawazo kweli. Nilimuangalia kwa karibu zaidi, na kila nilivyomuangalia sura yake ilikuwa inanichanganya. Alionekana ana uzuri fulani uliofichika lakinu huwezi kuuona hadi uwe kwenye upande fulani ndipo unaweza kuuona. Kama mnakumbuka zile rula za plastiki zenye vimichorochoro vya Mickey Mouse (vile vikatuni vya Disney) na vimefichwa fichwa hadi ugeuze geuze ile rula ndiyo unaweza kuona. Nadhani kulikuwa kuwa na vichongeo kama hivyo pia. Ndiyo uzuri wa Irena ulivyofichika.
Kwa mbali sura yake ilikuwa kama makubanzi, lakini kwa karibu sura yake ilificha uzuri wa binti wa kiafrika aliyejaliwa, umbo zuri, na akili iliyopevuka. Nilianza kukubali mawazoni mwangu kuwa nilikosa mbele za Mungu kumhukumu dada huyo namna hiyo kwa kuangalia sura yake tu, nilijikuta joto likianza kunipanda mwilini, huku viungo nyeti vikianza kushangalia na kukubaliana na mawazo yangu hayo mapya. Niliuma mdogo wangu wa chini nikaguna. Irena alishtuka.
"Nini tena M?." aliniuliza na bila kufikiri aliniita kwa jina langu la kwanza.
"Hapana matatizo, nilikuwa naota tu" nilimjibu kama mtu aliyeshikwa akifanya jambo asilopaswa huku nikicheka kwani nilikumbuka tangazo la zamani la biashara kwenye redio Tanzania ambalo mwisho wake jamaa alikuwa akisema "Nilikuwa naota tu".
Tuliwasili kwenye jiji la Salama karibu masaa saba baadaye na kabla ya kuagana tulipeana anuani zetu za barua pepe ili kabla ya Krismasi tukutane kwa moja moto moja baridi.
"Nitafurahi kukuona kabla ya Krismasi M." Aliniambia huku akinyosha mkono wake kuniaga. Kwa mbali niliona aibu ya kike iliyofichika na soni ya mtoto wa kike.
"Angalia email yako basi baada ya kama wiki hivi, Ok?" Nilimuambia huku nikiuvuta mkono wake wa kulia uliokuwa laini kama pamba karibu na mdomo wangu na kwa heshima zote kama niliyekuwa mbele ya binti mfalme niliubusu, nikilishindilia busu hilo kwa sekunde chache huku macho yangu nikiyakaza kwenye uso wake mpole. Irena alifumba macho na kuachia mdomo wake wazi, kwani hakutarajia mimi kuonesha heshima kwake mbele ya kadamnasi ya watu hapo nje "Kipawa".
Tulipoachana siku hiyo, nilimuweka mawazoni kwa muda mfupii lakini siku mbili baadaye alinitoka kabisa mawazoni. Baada ya kutulia nyumbani kwa siku kadhaa nikisalimia ndugu jamaa na marafiki ambao niliwamiss kwa muda mrefu, nilijikuta nikianza kumfikiria tena Irena. Kwa kadiri Krismasi ilivyokaribia ndivyo nilivyozidi kumfikiria yule binti, hata sijui ni kwanini.
Ilikuwa ni siku ya Jumatano kabla ya Krismasi nilipoamua kwenda katika moja ya vicafe ambako kuna huduma ya mtandao kwa malipo. Lengo langu ilikuwa kumtumia barua pepe Irena ili nitimize ahadi yangu ya kuonana naye kabla ya Krismasi (katika maisha yangu najitahidi kwa udi na uvumba kutimiza ahadi zangu). Haikunichukua muda nikaingia kwenye mtandao nikitumia anuani yangu ya MwanaKJJ@hotmail.com na bila ya kuchelewa kulikuwa na shehena ya ujumbe kutoka marafiki zangu, mashabiki, na maadui kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Sikuziangalia hizo zote, nilikuwa natafuta anuani ya Irena. Mara nikaona mfululizo wa vibarua pepe vyote vikiwa na kichwa cha habari kisemacho "Irena has sent you a card". Nilianza kuhisi viganja vya mikono yangu ikilowa jasho kidogo, nilipoanza kubofyoa viunganishi hivyo vya mtandao na kuzifungua hizo kadi. Niliishiwa pumzi, kwani Irena alikuwa amejaliwa maneno mazuri. Kubwa aliloniambia ni kuwa angependa sana tuonane kabla ya Krismasi kwani ameniandalia surprise. Akaniachia namba ya simu nimpigie wakati wowote. Kila kadi ilifungwa kwa maneno mazuri ya urafiki wa karibu. Na mimi niliamua kumjibu kwa kadi moja ambayo ndani yake niliandika ifuatavyo.
Mpendwa Irena,
Tangu tukutane wiki chache zilizopita kwa mipango ya Mungu, nimekuwa nikikuwaza kila zaidi kuliko siku iliyopita. Sijui ni nini kimenikumba lakini umekuwa kama nyota ya heri iliyofunuliwa mbele yangu, kama uwa waridi lililozuka mbugani, na kama tausi katikati ya viboko! Kwa kadiri ninavyokufikiria ndivyo moyo wangu unavyozidi kuyeyuka mbele yako. Natamani kukuona sana kuliko unavyoweza kufikiri. Samahani kwa kuchelewa kujibu kadi zako, nimezipenda hadi najisikia aibu ya mtoto wa kiume! I hope to c u soon!
Nilimalizia kwa kuambatanisha na kadi yenye maua ya waridi thenashara. Katika mojawapo ya email zake Irena alinipa anuani yake ya kazini kwenye ofisi za WHO Tanzania alikokuwa anafanya kazi kama Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha Utafiti wa Magonjwa ya Watoto. Moyoni, nilifurahia sana. Sikuchelewa baada ya kutoka hapo tu kwenye huo mgahawa nikaamua kumpigia simu kazini. Irena alikuwa ametoka lunch tu.
"Habari yako Irena" Nilimuuliza kwa sauti ya upole.
"Nzuri tu, nani mwenzangu" Alijibu kwa heshima lakini akiwa na udadisi.
"Hahaah, kwani una wenzako wangapi?" Nilimuuliza kwa kicheko cha kijanja.
"is this M?" Aliuliza kwa shauku huku akishikilia pumzi yake. Nilisita kidogo kuacha ukimya upite kati yetu.
"The only one baby" Nilimwambia kwa majigambo ya mtoto wa Kinyakyusa.
"Oh, my God, sikutegemea utanipigia simu, asante sana.. yaani you just made my day" Alisema akichanganya kiingereza na Kiswahili huku akionesha shauku kama mtoto wa kike aliyepevuka hivi karibuni.
"Haya sema, samahani kwa kuchelewa kuwasiliana nawe" Nilimwomba radhi.
"Hamna tatizo, sikutegemea kama ungenijibu anyway" Alisema huku akificha katika maneno yake hali ya kukata tamaa.
"Kwa nini? Si nilikuahidi tutaonana kabla ya Krismasi" Nilimuuliza.
"Wewe! Hivi unajua wanaume wangapi wameniambia watanipigia simu au watataka tuonane tena na kamwe haikuwa hivyo? Nilidhania na wewe ni mmoja wao" Alisema kwa sauti yake nyororo ambayo kwa hakika hata kama nyota ni chatu, basi angetoka huko pangoni.
"Irena, mimi si kama wanaume wengine" Nilimjibu nikimhakikishia.
"Umewahi kufika Kunduchi Beach?" Aliniuliza.
"Hapana, vipi kwani?" Nilimjibu bila haya. Ni kweli sijawahi kufika Kunduchi Beach licha ya kusikia sifa zake kutoka kwa watu wengi.
"Leo ni Jumatano, unaweza kupata nafasi Ijumaa tukutane huko tuzungumze, kuna sehemu nzuri za kuketi na kupunga upepo" Alisema Irena akisubiri jibu langu kwa hamu.
"Of course, saa ngapi" Nilikubali na kumrushia swali papo hapo.
"Baada ya kazi, nipigie simu ukiwa njiani kuja basi" Alijibu na kunipa maelekekezo. Basi tuliagana kukutana siku ya Ijumaa kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach iliyoko kwenye ufuko wa bahari ya Hindi nje kidogo ya Jiji la Dar.
* * *
Niliona Ijumaa imechelewa kufika, na ilipofika niliona masaa yanaenda taratibu utadhani yamepanga njama dhidi yangu. Majira ya saa tisa za adhuhuri nilianza kujiandaa, nilisafisha gari langu la kukodi na kuhakikisha lina mafuta ya kutosha, na nikavalia suruali yangu ya jeans ya bluu iliyopauka, na miguuni nikiwa nimevalia viatu vya raba za Jordani vya rangi nyeupe vyenye mchirizi wa rangi nyekundu wa nembo ya Nike. Nilivalia shati la jepesi la mauaua ya rangi ya machungwa na hudhurungi kama vile niko Visiwa Hawaii, niliachia kifua changu wazi kidogo kikionesha fulana yangu yenye matundu tundu huku shingoni mwangu ukining'inia mkufu wangu wa bahati. Nilijiangalia mara moja tu kwenye kioo na kugundua kuwa niko bomba, nikajisemea "Aloha"!
Ilinichukua karibu masaa mawili kufika Kunduchi kupitia barabara ya Mwenge. Moyo nusura unitoke kwani nashukuru nilikuwa sijawahi kufika hoteli hiyo kabla ya hapo. Hoteli ilikuwa imefanyiwa matengenezo makubwa na kurejeshewa sifa yake. Kwa mbali ilionekana kama jumba la kifalme! Sikuamini kuwa katika Tanzania kuna majengo mazuri kama hilo la hoteli ya Kunduchi. Hoteli ilikuwa na maudhui ya Kiarabu na Kiswahili. Kwa kweli ilipendeza kweli, na nikajua kuwa Irena alikuwa anajua kuchagua vitu vizuri.
Nilipofika kwenye meza ya mapokezi nililakiwa na mwanadada mrembo ambaye alikuwa amevalia batiki la rangi ya kijani inayong'ara na nikamwambia kuwa mimi ni mgeni wa Irena. Akanielekeza kuwa Irena yuko upande wa bahari kwenye majawapo ya vibanda vya kupungia upepo, ananisubiri. Huku nikipiga mluzi na kuchezea ufunguo wa gari mkononi, nielekea alikokuwepo Irena.
"Hi M" Sauti ilinishtua baada ya kumpita dada mmoja aliyekuwa ameketi kwenye kiti cha uvivu.
Alikuwa Irena. Jamani dada likuwa ni mweusi, lakini ni weusi wa kupendeza. Alikuwa amevalia pia tisheti ya mikono mifupi inayobana na kakaptula kafupi kabisa kalikoishia chini kidoto tu ya ****** yake. Alikuwa ametunisha kifuani na kiunoni na kuonekana mrembo kweli. Nilishauzoea uso wake, na kwa hakika nilijua tu kuwa hakuwa na sura mbaya kiasi hicho, ni mtazamo tu. Sisemi uongo, hakuwa na sura ya Halle Berry au Jessica Alba au mmoja wa warembo wetu wa kibongo, lakini hakuwa na sura ya Idi Amin pia.
Niliketi karibu yake huku macho yangu yakimvinjari mwili wake mzima.
"Hali yako Irena, nimekumiss kichizi" nilimwambia.
"Miye mzima, ila naona nimekumiss zaidi" Alisema huku akidondosha macho yake chini kwa aibu ya binti wa Kitanzania.
Tuliendelea kuzungumza na kuhadithiana tuliyoyaona Bongo tangu turudi nyumbani na kupeana michapo ya huko tulikotoka. Tukiwa tumezama kwenye gumzo, tulikuta kagiza kamenyemelea taratibu. Sauti ya mawimbi ilisikika kwa nguvu huku upepo mwanana ukipuliza na kutuletea harufu ya chumvi. Hoteli ya Kunduchi iliangazwa kwa taa nyingi zilizopangwa vizuri.
"Unataka twende ndani?" Irena aliniuliza.
"Kuna mahali pazuri pa kuketi hapo ndani?" Nilimuuliza.
"No, nimepanga chumba hapa kwa muda wote niko hapa hadi nitakapopata nyumba yangu" Aliniambia huku akinyanyuka na kuchukua kanga yake na mkoba wake na kuongoza njia. Kama simba aliyeona mawindo, nilimfuata nyuma, huku macho yangu yakikodolea wowowo lake lililokuwa likitingishika kwa mtindo wa "Singida Dodoma, Singida Dodoma"! Nilihisi beberu aliyelala zizini akiamshwa usingizini. Moyo ulianza kunidunda!
Chumba alichokuwa amepanga Irena kilikuwa kikubwa, chenye sebule na baa yake. Kilipambwa vizuri. Kitanda chake kilikuwa kikubwa na cha kuvutia, kilichotandikwa mashuka meupe ya hariri. Nilijikuta natabasamu. Nilikuwa bado nimesimama kwenye zuria zuri la Kichina karibu tu na mlango na Irena alikuwa mbele yangu akiwa amenipa mgongo. Jinsi Irena alivyosimama ndani ya chumba hicho na jinsi kilivyopambwa ilikuwa ni kama kumuangalia malkia ndani ya Kasri yake. Irena aligeuka taratibu, huku akiniangalia, macho yake yalipogongana na yangu miguu yangu ilikosa nguvu. Alitabasamu akinisogelea taratibu.
"Mwanakijiji, najua sina sura ya kuvutia kama mademu wengine" alisimama mbele yangu.
Sikujua niseme nini, nilishikwa na kigugumizi cha ghafla. Nilijua kumuambia alikuwa ni mzuri wa sura ilikuwa ni kumdanganya, lakini neno "mbaya" halikuingia akilini mwangu.
"Irena, binadamu wote tuna mapungufu na kasoro fulani, lakini sote tunastahili kupewa nafasi ya kupenda na kupendwa" Nilimuambia kwa sauti ya upole kama nambembeleza simba jike. Macho yake yalimulika kama nyota ya alfajiri. Alitabasabamu, na macho yake meupe yaling'aa na hivyo kuupamba uso wake uliokuwa mweusi wa mpingo wa kimakonde!
Kwa kutumia mikono yake yote miwili, Irena alianza kuivuta tsheti yake kuanzia kiunoni kuelekea kichwani kuivua. Jinsi ilivyombana, basi matiti yake yalichoropoka kwenye sidiria ya Victoria Secret yenye rangi nyekundu na ya kichandarua, chuchu zake nyeusi zilizokuwa zimesimama kwa hamu zilinichungulia kana kwamba kuniita "karibu". Nilianza kuhema taratibu.
Nilimsogelea Irena wakati bado anavuta tsheti yake usoni na kuufunika uso wangu kwenye matiti yake. Harufu ya poda iliingia puani mwangu na kunifanya nijisikia ka' mtoto mdogo. Nilizungusha mikono yangu na taratibu nilikinasua kifungo cha sidiria n kuidosha sakafuni. Kabla Irena hajamaliza kuitoa tsheti kichwani, mikono yae ikiwa bado iko juu, mdomo wangu uliibugia chuchu ya kulia kama nimepagawa mashetani! Aliguna kwa mfadhaiko wa ghafla na nusura adondoke.
"EM..EM" Aliita kwa taratibu.
"Tulia Irena...na wewe unastahili kupendwa" Nilisema huku ulimi wangu ukiendelea kumvinjari mwili wake. Nilimvuta karibu na kumpandikizia busu la nguvu, la taratibu, la upole, lakini lililojaa kila aina ya mahaba ndani yake. Kwa karibu sekunde thelathini nilimbusu midomo yake kwa mapenzi. Alikuwa ananukia vizuri kweli.
Nilizungusha mikono yangu nyuma yake na kama nimeshika bakuli kubwa la maji niliishika wowowo lake lililojaa mikononi mwangu. Nilimnyanyua. Na yeye hakusita kuzungusha mikono yake mgongoni kwangu huku kichwa chake akikilaza kwenye bega langu upande wa kushoto wa shingo yangu. Nilimchukua taratibu na kumlaza kwenye kitanda cha hariri! Kwa mbali niliweza kusikia sauti ya upepo ukivuma na ukipiga mluzi kama wimbo wa mapenzi!
Nilimfungua vifungo vya kakaptula kake na pole pole niliivuta chini taratibu nikionyesha chupi nyingine nyekundu ya nyavunyavu iliyoyabana mapaja yake vilivyo na kumfanya aonekane kama yule dada mrembo mweusi sana kutoka Uganda. Weusi wake na rangi nyekundu ya chupi hiyo, viliwiana vyema. Kiuoni alikuwa amejaza shanga za rangi mbalimbali ambazo zilikuwa ni kama viungio vya mboga, bila ya shaka ndo maana hivyo vyaitwa chachandu! Nilianza kumbusu taratibu kuanzia mapajani, tumboni, kifuani na nilibusu kila chuchu taratibu.
Irena alikuwa amefumba macho huku mikono yake ameiweka nyuma ya kichwa chake juu ya mito. Baada ya kupeana mahaba ya mwanzo, taratibu nilimwingia huku nikimuangalia sura yake nyeusi ambayo ilikuwa iking'ara kwa mapenzi. Tulifanya mapenzi kwa karibu nusu saa kwa raundi ya kwanza. Irena alikuwa ana machozi usoni kwake yaliyoendelea kuupamba uso wake. Tulifanya mara nyingine nne usiku huo.
Kesho yake ilikuwa ni usiku wa Krismasi na sikutaka kuila Krismasi hiyo na mtu mwingine yeyote isipokuwa Irena. Tulienda pamoja kanisa la Mt. Petro Oysterbay, karibu na ninakoishi eneo la Msasani. Sikujali watu waliokuwa wanatuangalia, na yeye hakujali!! Tulikuwa kama watu wa ile hadithi ya "Ua Jekundu" lakini wahusika wakiwa wamegeuzwa. Irena alikuwa ni binti mwenye tabia nzuri ambayo katika maisha yangu sijawahi kukutana na binti kama huyo. Mwishoni mwa mwaka tuliagana mimi nikirudi na yeye akibakia nyumbani. Tuliendelea kuwasiliana mara kwa mara lakini kutokana na sababu zisizoweza kuelezeka hatukuweza kupata nafasi ya kukutana tena.
* * *
Mwezi wa August mwaka huu Irena alinitumia barua pepe kuniambia kuwa amepata nafasi ya kuja kusoma Marekani shahada ya Udaktari katika chuo kikuu cha Minnesota kuanzia mwezi wa kwanza mwakani. Nilifurahi sana, kwani nilijua wakati wa mimi kutulia umefika kwani licha ya bahati ya kukutana na mabinti wengi katika kila kona ya dunia, ukweli ni kuwa sijawahi kupenda kama nilivyompenda Irena wangu, dada mwenye sura kwatu, isiyo na kutu, na isiyo na utukutu! Ni yeye aliyebadili mawazo yangu kabisa kuwa uzuri ni kwa yule anayetazama, na kuwa hata tunaowadhania wana sura mbaya, nao wanajua kupenda na wanastahili kupendwa.
Ni yeye aliyenifanya niamini ya kuwa mwenye kupenda haoni, ingawa macho anayo! Ni huyo Irena wangu, ambaye katika maisha yangu yote, ningetamani awe ubavuni kwangu na pembezoni mwangu kama msaidizi na rafiki yangu wa karibu. Kama ningepewa nafasi moja tu kupenda na kupendwa, ningemuomba Mungu anipe nafasi tena na Irena.
Ninapoandika kisa hiki, machozi yananitiririka, na fundo la uchungu limekaba koo langu, na najisikia kutetemeka kwani nikimkumbuka Irena namshukuru Mungu kwa kumleta kwenye maisha yangu namna hiyo. Hata hivyo, uwezekano wa mimi kukutana naye tena haupo. Unakumbuka ile ajali ya Basi iliyotokea Kibaha hivi karibuni na kuua watu kumi na sita?.... .... ndiyo....Irena alikuwa ni mmoja wao.
M. W. I. S. H. O..