Kumekucha Pemba, Wanawake watatu wapewa talaka kwa sababu za kisiasa

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
677
1,000
Wakinamama takribani watatu wamethibitika kupewa talaka baada ya hekaheka za uchaguzi. Wete katika jimbo la Gando mume ametoa talaka kwa bi. Zawadi Ally Haji

"Niliachwa kipindi hicho cha siasa, mume aliniambia nikienda kupiga kura ndio talaka yangu na mimi nikaenda, nilivyorudi jioni ndio nikawa nishaachika. Nilipokwenda nikamchagua Rais ninaemtaka mie, Hussein na Salim Mussa, kwa sababu ndio yeye hakuwataka sikumfuata upande wake atakao, kwa sababu nimefata upande wangu ninaoutaka" Alisema Bi. Zawadi, mke alieachika.

Mzazi wa Bi. Zawadi, Zadi Hamad Iddy amesema kwa masikitiko binti yake huyo amerejea nyumbani akiwa na mtoto wake mdogo.

"Sijapokea uzuri kwa sababu alipoanza kumposa huyu ni mwali na mama yake alikuwa ni mwana CCM na alipokuja tulimwambia unakuja tuolea mwenetu lakini yuko upande wa CCM na huyu mwanaume alikuwa ni CCM, baada ya kukaa na kugombana na wazazi wake akatoka CCM akajifanya CUF kwanza, baadae ndio akaja ATC lakini wakati wote huo hawana ugomvi lakini ikifika wakati wa siasa tu!

Safari hii anamtilia tena usiende kupiga kura kwa sababu ajua ni against na yeye, huyu ni CCM, yeye ni ATC. Kwao hatuwaingilii lakini hii kuacha sasa, kamuacha kweli na sasa hivi yuko nyumbani kama unavyomuona wala hajaja kusema anamrejea, kajizuia na sisi tumejizuia. Si jambo zuri, huu ni mchezo tu ingawa twawania dola sio kama mchezo wa mpira"

Nae Jaffari Suleiman amesema binti yake ameachwa kwa habari ya siasa, alienda akakaa PO Shezamwe, aliporudi mume akamtaliki hivyo amerudi nyumbani na watoto wawili bila ya kumshughulikia mke aliemuacha na watoto wake. Jaffari anasema hatua aliyochukua ni kulifikisha suala hilo kwenye chama na Serikali.

 

Abuu Kauthar

JF-Expert Member
Jul 10, 2011
3,662
2,000
Jamii za waswahili zina mambo mengi ya kiswahili swahili tu.

Pwani, Tanga, Mtwara,Lindi, Tabora na Dodoma NDIPO JAMII HIZI ZINAPOPATIKANA, KUNA UMASIKINI ULIOTOPEA.

Mwarabu kapota.

Bora hao waswahili wanaachana fresh kila mtu anaendelea na maisha yake. Lakini hao wabara mwanaume kazi kuua, kutesa, kuvunja, kuwaharibu wanawake tena kwa sababu za kijinga kabsa. Eti hajapika ugali...mara eti hajapiga magoti. Lakini hao waswahil fresh tu wanaachana. Na kuhusu umasikini Tanzania karibia yote masikini sehemu na watu wachache tu. Hivyo punguza wivu
 

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,529
2,000
Kwa maumivu tuliyosababishiwa na CCM kwenye uchaguzi huu hata mimi ningekuwa na mume ambaye ni CCM tungeachana tu.

Huyo jamaa aliyeacha mke anajielewa sana, ningekuwa single ningemtafuta lol
Maumivu gani!!!!!! Wazanzibar hawawezi kutawaliwa na yule babu, marais wazee wabaki huko Ulaya na Marekani ambako hawazaani, wamebaki kuf...na tuu
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,596
2,000
Jamii za waswahili zina mambo mengi ya kiswahili swahili tu.

Pwani, Tanga, Mtwara, Lindi, Tabora na Dodoma NDIPO JAMII HIZI ZINAPOPATIKANA, KUNA UMASIKINI ULIOTOPEA.

Mwarabu kapota.

Siyo kweli, kwanza hao unaowaita ,,Waswahili'' wana maisha bora yaliyostaarabika na ya juu kuliko huko kwenu ambako haujakutaja, hata ustaarabu tu wa Tanzania yote kama upo hata kidogo ni wa Kiswahili kuanzia Lugha, mapishi, mavazi mpaka kuishi pamoja, hivyo umasikini utakuwa huko kwenu kwa maana hamna ustaarabu wowote kama upo utaje hapa, ...
 

Compton

Senior Member
Aug 12, 2016
117
250
Hao watu wa Pwani hata Vyoo hawana wanajisaidia baharini, unasema wamestaarabika?
Siyo kweli, kwanza hao unaowaita ,,Waswahili'' wana maisha bora yaliyostaarabika na ya juu kuliko huko kwenu ambako haujakutaja, hata ustaarabu tu wa Tanzania yote kama upo hata kidogo ni wa Kiswahili kuanzia Lugha, mapishi, mavazi mpaka kuishi pamoja, hivyo umasikini utakuwa huko kwenu kwa maana hamna ustaarabu wowote kama upo utaje hapa, ...
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,596
2,000
Hao watu wa pwani hata Vyoo hawana wanajisaidia baharini, unasema wamestaarabika?

Taja kwenu halafu tulinganishe, nitajie ustaarabu wowote mlionao aidha wa mavazi au hata chakula tu, umeshataja wa Pwani sasa taja kwenu, tuone huo ustaaraubu mlio nao, ...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom