Mbunge Nicodemus Maganga: Siasa Zisitugombanishe - Uchaguzi wa Diwani katika Kata ya Isebya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

Mbunge Nicodemus Maganga: Siasa Zisitugombanishe - Uchaguzi wa Diwani katika Kata ya Isebya

Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Mkoani Geita Mhe. Nicodemus Maganga amewataka wananchi wa Kata ya Isebya kujiepusha na maneno ya uchonganishi yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Mhe. Maganga ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Diwani wa Kata hiyo ambapo amesema,

"Sheria na taratibu za Serikali kila panapotokea mambo kama haya ni lazima uchaguzi ufanyike tena, asiwepo mtu atumie nafasi hii kuleta uchonganishi kwamba mambo yaliotokea kuna kitu kimefayika niwaombe sana wana Isebya msigombane kwa ajili ya vyama"

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa Fadhil Maganya amewataka Wananchi hao kuwa watulivu kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi huo bila kusababisha uvunjifu wa amani.

"Huu ni Uchaguzi wa Kisiasa wala hatuna sababu yoyoyte ya kuumizana, kwasababu yoyoyte ile, tufanye uchaguzi wenye ustaarabu lakini pia tukumbuke sisi ni jamii moja" amesema Maganya.

Awali akiomba kura kwa Wananchi Mgombea huyo, George Mbapula amesema anatambua changamoto wanazozipitia wananchi wa Kata hiyo ikiwemo ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji hivyo akipewa nafasi hiyo atahikikisha changamoto hizo zinatatuliwa.

Uchaguzi mdogo wa Nafasi ya Diwani katika Kata ya Isebya Jimboni Mbogwe unafanyika baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo kufariki.
 
Attachments

  • Untitledaqwsazx.jpg
    Untitledaqwsazx.jpg
    7.7 KB · Views: 2
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa Fadhil Maganya amewataka Wananchi hao kuwa watulivu kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi huo bila kusababisha uvunjifu wa amani.

"Huu ni Uchaguzi wa Kisiasa wala hatuna sababu yoyoyte ya kuumizana, kwasababu yoyoyte ile, tufanye uchaguzi wenye ustaarabu lakini pia tukumbuke sisi ni jamii moja" amesema Maganya.
Wanafiki tu. Sasa wanagomba na nani?
 
Back
Top Bottom