Kumekucha Pemba, Wanawake watatu wapewa talaka kwa sababu za kisiasa

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,269
2,000
Kwa maumivu tuliyosababishiwa na CCM kwenye uchaguzi huu hata mimi ningekuwa na mume ambaye ni CCM tungeachana tu.

Huyo jamaa aliyeacha mke anajielewa sana, ningekuwa single ningemtafuta lol
Hivi ikatokea ndugu yangu ameuawa na askari wa CCM kwa sababu tu ndugu zangu ni wapinzani, najua kabisa ndugu yangu kauawa na CCM, halafu mke wangu akawashabikia wauaji, bado nitakuwa na upendo na mwanamke wa namna hiyo? Lazima niseme wazi, HAPANA.

Kwa kilichofanyika safari hii, kuishabikia CCM ni kushabikia mauaji ya watu wasio na hatia, ni kushabikia mateso ya watu waliowekwa kwenye mahabusu za polisi bila hatia, ni kushabikia siasa za kishenzi zisizokubalika katika jamii yoyote ya watu waliostarabika.

Mimi siwezi kuwa na mahusiano zaidi ya yale ya kawaida na wanCCM wanaoshabikia matendo ya kishenzi dhidi ya watanzania wenzao. Wapo wanaCCM ambao nao hawakujua kama chama chao kingeishia kuwa genge la wahuni dhidi ya raia. Hawa naendelea kuwa karibu nao maana wanatambua kuwa mbele ya itikadi za vyama kuna ubinadamu wetu, utu wetu na Taifa letu.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,269
2,000
Sijajua kama kuna watu wapumbavu na wapo wanaoshabikia upumbavu, huwezi kulazimisha mtu achague chama anachotaka matokeo yake anamuadhibu hata mtoto asiye na hatia.
Nadhani hapa siyo suala la itikadi bali ni mwenzi wako kushangilia au kushikamana na wauaji (CCM). Maana kwa sasa CCM siyo chama bali ni genge la wauaji, wavuruga demokrasia, na wavunjaji wa haki za raia.
 

fundinaizer

JF-Expert Member
Dec 15, 2016
1,516
2,000
Kwa hiyo mama akiwa CCM na Mzee ACT wazalendo - mambo ya unyumba inakuwa hakuna tena ili msikwazane, maana unaweza kusaula ukakutana na guo la ndani la rangi ya kijana limeandikwa Hapa kazi tu - munkari wote unakata ghafla...
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
50,077
2,000
Kwa hiyo mama akiwa CCM na Mzee ACT wazalendo - mambo ya unyumba inakuwa hakuna tena ili msikwazane, maana usiku unaweza kumsaula ze wife ukakutana na guo la ndani la rangi ya kijana limeandikwa Hapa kazi tu - munkari wote unakata ghafla...
Aolewe na CCM wenzake
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,301
2,000
Sijajua kama kuna watu wapumbavu na wapo wanaoshabikia upumbavu, huwezi kulazimisha mtu achague chama anachotaka matokeo yake anamuadhibu hata mtoto asiye na hatia.
Naye hajalazimisha abaki naye, kampa uhuru aende huko atakapokwenda kiroho safi!

Hata mimi ningeishi zama za Hitler halafu mke wangu akawa anaunga mkono chama cha NAZI nahisi ningempa talaka!
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,664
2,000
Mawakili wana CCM mburuzeni hicho kidume kimpe mali mahakamni huyo mwanamke kiliyemuacha hakuna cha msikitini ni mahakamani tu
 

Laface77

JF-Expert Member
Jul 9, 2008
2,116
2,000
Wakaolewe na Slowslow na kama ni weupe Jiwe/Kichaa anaweza kuwaoa. Mimi hata angekua bab yangu au mama yangu kaipigia kura CCM ningemkana siku hiyohiyo!
 

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
29,112
2,000
Maumivu gani!!!!!! Wazanzibar hawawezi kutawaliwa na yule babu, marais wazee wabaki huko Ulaya na Marekani ambako hawazaani, wamebaki kuf...na tuu
Wala wazanzibari hawawezi kutawaliwa na wezi na wauwaji . AINGIAYE KWA UPANGA ATATOKA KWA UPANGA
 

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
29,112
2,000
Sijajua kama kuna watu wapumbavu na wapo wanaoshabikia upumbavu, huwezi kulazimisha mtu achague chama anachotaka matokeo yake anamuadhibu hata mtoto asiye na hatia.

Tatizo matatizo yanasababishwa na hawa madhalimu, wakati wa serikali ile tunayoambiwa ni ya waarabu kulikuwa hakuna haya mambo
 

kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
3,673
2,000
Mwaka huu, CCM ilijuwa janja ya wapinzani Pemba. Kule watu wa CUF enzi hizo walikuwa wakiwashikia panga wanaCCM wasiende kupiga kura. Na ndiyo ilikuwa janja ya CUF kukomba majimbo yote.

Mwaka huu, kwanza wana jeshi na polisi wakapiga kura siku moja kabla! Hivyo siku ya uchaguzi wakawalinda wanaCCM wasizulike na CUF. Matokeo mmeyaona. Hizo za kutaliki ni hasira maana wanaCCM walipewa jeuri safari hii ya kupiga kura.

Utafiti hoyeee
 

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
12,305
2,000
Wanawake watatu wamethibitika kupewa talaka na Waue zao baada ya hekaheka za uchaguzi, huko katika Jimbo la Wete mume amemuacha Mkewe Bi. Zawadi Ally Haji.

“Niliachwa kipindi hicho cha siasa, Mume aliniambia nikienda kupiga kura ndio talaka yangu na mimi nikaenda, nilivyorudi jioni ndio nikawa nishaachika, nilipokwenda nikamchagua Rais ninaemtaka mie” Bi Zawadi

“Hussein na Salim Mussa, kwa sababu ndio yeye hakuwataka sikumfuata upande wake atakao, kwa sababu nimefata upande wangu ninaoutaka” Bi. Zawadi, mke alieachika


Mzazi wa Bi. Zawadi, Zadi Hamad Iddy amesema kwa masikitiko binti yake huyo amerejea nyumbani akiwa na mtoto wake mdogo.

“Sijapokea uzuri kwa sababu alipoanza kumposa huyu ni mwali na mama yake alikuwa ni mwana CCM na alipokuja tulimwambia unakuja tuolea mwenetu lakini yuko upande wa CCM na huyu mwanaume alikuwa ni CCM”Zadi Hamad

“Baada ya kukaa na kugombana na wazazi wake akatoka CCM akajifanya CUF kwanza, baadae ndio akaja ATC lakini wakati wote huo hawana ugomvi lakini ikifika wakati wa siasa tu” Zadi Hamad
Credit: Milard Ayo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom