Yesu alitoa muongozo na majibu ya maswali ya taratibu za talaka kwenye ndoa, kwa nini watawa wa kanisa katoliki hawaoi?

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,734
10,041
Kwenye Suala la kutoa talaka:

Yesu aliwajibu wafarisayo walipomjaribu;

Wakamuuliza: “Basi, kwa nini Musa aliagiza kutoa cheti cha kumfukuza na kumtaliki?”

8 Akawajibu: “Musa aliwaruhusu kuwataliki wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo. Ninawaambia kwamba mtu yeyote anayemtaliki mke wake isipokuwa kwa sababu ya uasherati, na kumwoa mwingine, anafanya uzinzi.

~Kwa hiyo talaka zinaruhusiwa kama mke au mume atakuwa amemchit mwenzi wake na mtu mwingine nje ya ndoa.

Kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na kashfa nyingi sana ndani ya kanisa la katoliki kuhusu, ubakaji, kutokuweza kujizuia hali za kiubinadamu miongoni mwa watumishi wa kanisa. Hali hii imeleta kejeli nyingi sana. Ila Hayo yote yalishajilikana na Biblia inafafanua



Yesu aliwajibu kuhusu swala la kutokuoa kuwa;

Yesu akawaambia: “Si watu wote wanaolipa nafasi jambo hilo, ila tu wale walio na zawadi. 12 Kwa maana kuna wale waliozaliwa wakiwa matowashi, wengine wamefanywa matowashi na watu, na wengine wamejifanya wenyewe kuwa matowashi kwa ajili ya Ufalme wa mbinguni. Yule anayeweza kulipa nafasi jambo hilo na afanye hivyo.

(MATOWASHI): Matowashi ni watu waliojitoa wakfu kwa Mungu, wasiojihusisha na mambo ya wanawake,(yaani kuwa na mke au watoto), mfano wa matowashi katika biblia ni Bwana wetu Yesu, Mtume Paulo,Barnaba, n huwenda pia Yohana mbatizaji, Danieli na Eliya.

Kwa nini "matowashi" wetu wachache wanashindwa kuishi viapo vyao? Sababu inaweza kuwa

A) Labda aliingia katika utumwe kwa msukumo wa watu wake wa karibu labda mfano; familia.

B) Tamaa binafsi na msukumo binafsi alizochochewa nazo baada ya kuona hali fulani ya maisha wanayoishi hao mapadri au masista. Mwisho wa siku anapoingia huko anakuta uhalisia uko vipi.
 
Back
Top Bottom