Kumbe Uturuki hamna Christmas!..

Kumbe Uturuki hamna Christmas!..

Wacha mrusi awaadabishe tu ndio maana nyerere alikataa udini katika nchi ila kueshimu sikukuu za watu ni muhimu sana ukawapa watu mapunziko kwa kua uislam uturuki ni asilimia 70 tu 30% sio waislam vipi Zanzibar hapo asilimia 90 ni waislam na 10 ni wakristo?
 
Sio uturuki tu, nenda eastern Europe uone kama utakuta mtu akisherehekea leo.
Russia, Belarus, Latvia, Ukraine na nyingine nyingi tu hawana Christmas, wao husherehekea sikukuu yao 7th January, kanisa na waumini wa orthodox church hawana Christmas.
 
Hivi marekani taifa kubwa kabisa duniani wanasherehekea Eid ? Na je Uingereza? Ulishawahi kushangaa na hivi? Kila nchi ina taratibu zake kama vipi chukuwa off pika pilau yako na nguruwe ule uburudike!
 
Niko Oman since 2012. Mara ya mwisho kusherekea xmass, pasaka na mwaka mpya ilikua 2011 toka nilivyokuja huku imebidi tu nisahau hizo mambo kwa kweli....narudia tena Sio xmass na pasaka tuu, hata mwaka mpya no off except ule wa kiislam/hijra
 
Siku nyingine kabla ya kuandika mada au kulaumu kitu jaribu kujitafakari kwanza,

Hivi unafikiri kila nchi Duniani wanafuata utaratibu wa Sikukuu zote kama ilivyo Bongo?

Nafikiri nia yako kubwa ya kuanzisha hii thread ilikuwa ni kujitangaza kuwa na wewe upo Turkey kikazi.

Hahhahhahahahaah sentensi yako ya mwisho mi hoi
 
Nch km hzo hazifai kabisa...anyway vp musuala dada poa wapo lakini.isije wakawa wanabana pia
 
Ni utaratibu tu wa nchi husika. Ndio maana unaambiwa ukienda kwa watu ishi kama ulivyokuta wanaishi usianze kutaka kuingiza utaratibu wako. Sio kila mtu ana amini unacho amini wewe
 
nimesikitika kuona baadhi ya nchi wanaendekeza udini kupita maelezo. nipo uturuki kwa mda kama mwezi kikazi. nimeshangaa kuona leo dunia inaadhimisha sikuku ya kuzaliwa yesu lakini kwa hii nchi tofauti kidogo. watu wameenda kazini, vyuoni, shule na shughuli zote za maendeleo zinaendelea kama kawaida. nimemuuliza dogo mmoja ananiambia ndo ilivo kwa kawaida hakuna mapumziko ya chrismas wala pasaka. mapumziko ni siku za eid tu. nimesikitika kwa kweli nimekumbuka tanzania yangu. sikutegemea kama udini upo juu kiasi hiki kwa nchi kama uturuki!!!

Waturuki wengi Ni waislam
 
Ndio mahaana mkuu rahaana zinawatafuna plus majanga ni sawa kila nchi inataratibu zake lakin kumbuka waliopo wote c Islamic mfano huko turkey kuna ifesso wanahamin kuwa bikra maria alihishi pale na watalii wengi uwenda pale nakuchukuwa maji ya balaka wanawezaje kutoamin kuzaliwa kwa mfalme Wa wayaudi pumba kabisa
 
kila nchi ina taratibu zake na hilo nadhani unalifaham isipokuwa umeleta huu uzi ilia watu tujue kama uko uturuki ....fikiria broh kabla ya kuandika
 
Sweden,Norway na Denmark nao wabaguzi kwa sababu Idd hamna mapumziko? Tembea kijana wacha uvivu wa kufikiri.
 
Ukienda NorthKorea kule ndo hakuna cha uislam wala ukristo..kule usishangae kukawa nasikukuu ya kusherehekea bomu la nuclear au ballistic missile festivals
 
nimesikitika kuona baadhi ya nchi wanaendekeza udini kupita maelezo. nipo uturuki kwa mda kama mwezi kikazi. nimeshangaa kuona leo dunia inaadhimisha sikuku ya kuzaliwa yesu lakini kwa hii nchi tofauti kidogo. watu wameenda kazini, vyuoni, shule na shughuli zote za maendeleo zinaendelea kama kawaida. nimemuuliza dogo mmoja ananiambia ndo ilivo kwa kawaida hakuna mapumziko ya chrismas wala pasaka. mapumziko ni siku za eid tu. nimesikitika kwa kweli nimekumbuka tanzania yangu. sikutegemea kama udini upo juu kiasi hiki kwa nchi kama uturuki!!!

Mbona Vatican hakuna sikukuu ya Idd elfitri,Hajji wala mubarakka......
 
Back
Top Bottom