Haya Hapa Mahesabu Yanayoonesha Yesu Hakuzaliwa 25 Dec. Huu Ndio Mwezi Na Mwaka Aliozaliwa (Hatupingi Christmas, Kujifunza Tu)

Raphael Mtui

Member
Nov 26, 2024
68
190
Iko hivi: kwenye Biblia kuna viashiria kadhaa vya kuaminika vinavyoweza kutupatia mwaka na mwezi Yesu aliozaliwa.

Pia, vipo viashiria kutoka kwenye Biblia vinavyotuwezesha kujua mwaka Yesu aliozaliwa.

Kwa habari ya siku yenyewe kabisa, hatuwezi kuipata maana hakuna reliable source/chanzo cha kuaminika hata kimoja cha kuweza kutupa tarehe kamili.

Lakini kabla hatujaenda mbali, ni vyema ukajua mapema kwamba Kalenda hii tunayoitumia, hii inayotuambia huu ni mwaka 2024, sio kalenda ile tunayoiona kwenye Biblia.

NGOJA TUKUPE SOMO LA KALENDA KIDOGO.

Kalenda hii tunayoitumia inaitwa Gregorian Calendar, kwa majina mengine ni Western Calendar na pengine huitwa Christian Calendar maana ndio inatumika na Wakristo wa leo.

Ina jina la Gregory kwa sababu ilitangazwa na kuidhinishwa kwamba inafaa kutumika na aliyekuwa kiongozi wa kanisa la Kirumi Katoliki, Papa Gregory XIII mwaka 1582.

Kuna kalenda nyingi sana duniani, lakini hii ndiyo iliyojizolea umaarufu kuliko zote.

Waislamu hutumia calendar yao iitwayo Islamic Calendar na inategemea position ya mwezi tu. Ni pure Lunar Calendar (kalenda ya mwezi). Kwa sasa wako kwenye miaka ya 1400.

Gregorian Kalenda ni kalenda ya jua kabisa (Solar Calendar).

Lakini kalenda iliyopo kwenye Biblia ile Mungu aliyoianzisha kwenye Kutoka 12:1-2, inaitwa Hebrew Calendar. Ina mwaka wenye siku 360 tu. Hii ndiyo Ecclesiastical calendar (kalenda ya kidini).

Kalenda ya Kiebrania huzingatia mwezi na jua kwa pamoja ndio maana ipo kwenye kundi la Luni-Solar Calendars.

Hii calendar kwa sasa iko kwenye miaka ya 5700. Kwenye Biblia, tunaona siku na miezi ikitajwa, lakini mtu asidhani ni tarehe za kalenda yetu hii ya Gregorian.

Sasa, ni muhimu tujifunze miezi ya Kalenda ya Kiebrania ili tuweze kuelewa kirahisi mahesabu yetu hapo mbele.

Ifutatayo ni miezi ya Kiebrania ya kalenda hii ya Biblia, Hebrew Calendar.

(Nitazihusishanisha na siku na miezi ya kalenda yetu.)

I) Nissan/Abibu (Kutoka 13:4, 23:15, 34:18 Kumb 16:1 na Ester 3:7)--- Ni baadhi ya siku za miezi ya March na baadhi ya siku za April.

2) Iyar/Zivu (1Falme 6:1, 37). Ni baadhi ya siku za April na baadhi ya siku za May)

3) Sivani (Ester 8:9). Ni baadhi ya siku za May na baadhi ya siku za June.

4) Tammuz (Ezekiel 8:14). Ni baadhi ya siku za June na baadhi ya siku za July.

5) Abu/Av (Hesabu 33:38). Ni baadhi ya siku za mwezi July na August.

6) Elul (Nehemia 6:15). Ni baadhi ya siku za mwezi August na baadhi ya siku za September.

7) Tishrei/Ethanimu (1Falme 8:2). Ni baadhi ya siku za mwezi September na baadhi ya siku za October.

8) Cheshvan (1Falme 6:38). Ni baadhi ya siku za October na baadhi ya siku za November.

9) Kisleu (Zekaria 7:1). Ni baadhi ya siku za November na baadhi ya siku za December.

I0) Tevet (Ester 2:16). Ni baadhi ya siku za December na baadhi ya siku za Januari.

II) Shevati (Zekaria 1:7). Ni baadhi ya siku za Januari na baadhi ya siku za February.

12) Adar (Ester 9:15, 17na 19). Ni baadhi ya siku za February na baadhi ya siku za March.

SASA, TURUDI KWENYE MADA:

VIFUATAVYO NI VIASHIRIA VINAVYOWEZA KUTUPA KUJUA MWAKA YESU ALIOZALIWA.

1) KIFO CHA HERODE THE GREAT.

Mathayo 2:19-20
Hata ALIPOFARIKI HERODE, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri,

akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto.

Kifo cha Herode Mkubwa (Herode the Great) kilitokea mwaka 4BC.

Wakati huyu mzee anakufa (alifia kule Yeriko Judea), bado kina Yusufu na Maria walikuwa wamekimbilia barani Afrika pale nchini Misri kumficha mtoto Yesu asiuawe kutokana na tamko la mfalme huyo.

Hatutegemei kwamba Yesu alikuwa amezaliwa muda mrefu sana uliokuwa umepita hadi mfalme huyu anapokufa.

Kingine hapa utajiuliza: "Mbona Yesu amezaliwa miaka inayoangukia BC yaani Before Christ? Yesu azaliweje tena mwaka ambao ni KABLA YA KRISTO?"

Umeelewa hilo swali? Maana wengi hudhani siku ile Yesu aliyozaliwa ilikuwa tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka wa kwanza.

Ni kweli kwamba waliotengeneza hii kalenda yetu ya Gregorian Calendar, kina Aloysius Lilius, walitarajia kutumia kuzaliwa kwa Yesu ndio kuwe mwanzo wa kuhesabu siku za kalenda hii.

IKUMBUKWE KWAMBA HAKUNA KALENDA HATA MOJA DUNIANI INAYOWEZA KUHESABU KUANZIA ILE TAREHE KAMILI MUNGU ALIPOUMBA SIKU YA KWANZA KABISA. HUWA KILA KALENDA INAAMUA NI WAPI IANZIE KUHESABIA HASA KWENYE TUKIO KUBWA.

HATA HII KALENDA YA MUNGU (HEBREW CALENDAR) ALIYOWAPA WAISRAELI, MUNGU ALIYOITOA KWENYE KUTOKA 12:1- ALIAMUA IANZIE PALE MWISHO WA UTUMWA WA ISRAELI NCHINI MISRI NA NDIO HUWA WANAANZIA KUHESABIA HAPO NDIO MAANA WAPO MIAKA YA 5780.

Lakini kalenda yetu iliamua kuhesabu kuanzia kuzaliwa kwa Yesu japo mahesabu yake YALISHINDIKANA ku-pin-point kabisa siku ile ile Yesu aliyozaliwa.

Kwa hiyo USIDHANI KUWA SIKU ILE YESU ALIYOZALIWA NDIO HAPOHAPO KALENDA HII YA GREGORI ILIANZA KUHESABU TAREHE MOJA MWEZI WA KWANZA MWAKA WA KWANZA.

Kalenda yetu ni matokeo tu ya Julian Reformation tena yaliyofanywa baadaye sana miaka ya 1580 baada ya kuzaliwa kwa Yesu.

Kuna ambaye amedhani kwamba kabla ya kuzaliwa Yesu miaka ilikuwa inahesabiwa kunyume-nyume!!!

Hata mie niliwahi kuwaza hivyo kwa sababu ya jinsi kalenda yetu inavyohesabu ule upande BC, yaani miaka iliyo nyuma kabla ya kuzaliwa kwa Yesu.

'Kikalenda chetu' kinatulazimu kufanya hivyo maana tumetumia kuzaliwa kwa Yesu kama chanzo cha kuhesabu miaka na tarehe zetu.

Hivyo inabidi, miaka ya nyumba kabla ya Yesu (BC), tuihesabu kwa kurudi nyuma, LAKINI HIYO HAIMAANISHI WATU WALIOISHI SIKU HIZO WALIHESABU KINYUMENYUME.

Kalenda yetu ilikuwa bado hata haijazaliwa.

Kalenda za wakati huo ikiwemo hii ya Hebrew Calendar hazikuwa zikihesabu kinyume-nyume.

Tangu Kutoka 12:1-2, hadi leo wameshafika miaka ya 5780 wakati sisi bado tupo 2024.

Au nikutwange kaswali:

Kama walihesabu kuja kinyume-nyume walihesabu kuanzia wapi? Walichagua waanzie mwaka gani ndio waanze kushuka nao? Na namba hiyo ya miaka ingeshuka hadi mwaka sifuri ingekuwaje?

Tuache hayo.

Hiki hapa kiashiria kingine kinachoonesha Yesu alizaliwa around 6-4BC

2)SENSA (ORODHA) YA MFALME AUGUSTO

Tunafahamu kwamba wakati Yesu anazaliwa kulikuwa kuna zoezi kubwa la sensa ambalo lilikuwa linafanyika kwenye dunia yote iliyokuwa ikitawaliwa na Ngome au Dola ya Kirumi (Roman Empire).

Luka 2:1-7
Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.

Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu.

Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao.

Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;

ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.

Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,

akamzaa mwanawe, kifungua mimba,..

Kulingana na historia sahihi, sensa hii ilifanyika miaka kati ya 6-4BC.

Sensa hii ndio ya kwanza wakati Kirenio akiwa ameshateuliwa na Mfalme wa Dola ya Kirumi awe governor (liwali) wa jimbo la Syria (Shamu).

Kiashiria kingine.

3) KIRENIO ALIKUWA LIWALI WA SHAMU WAKATI YESU ANAZALIWA.

Kirenio (Quirinius) anatajwa hapo kwenye Luka 2:2

Huyu jamaa alikuwa anaitwa Publius Sulpicius Quirinius.

Kulingana na historia sahihi, huyu Kirenio alipewa cheo hiki mwaka 6BC, na ni kipindi hiki cha mwaka 6-4BC ambacho sensa ilifanyika mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa liwali (governor) wa Shamu (Syria).

Sensa hii iliwafanya kina Yusufu wasafiri kutoka Galilaya waje kwenye ukoo wao wa Daudi kule Bethlehemu ili wapate kuhesabiwa, kwa maana kipindi hicho kila mtu alitakiwa kuhesabiwa akiwa eneo la nyumbani alikozaliwa.

SASA TUANGALIE VIASHIRIA AMBAVYO VINAWEZA KUTUSAIDIA KUJUA YESU ALIZALIWA MWEZI GANI.

I) ZAMU YA ABIYA (THE COURSE OF ABIJAH)

Luka 1:5, 8-9
Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, WA ZAMU YA ABIYA, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti.
Basi ikawa, alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani KATIKA TARATIBU YA ZAMU YAKE mbele za Mungu.
KAMA ILIVYOKUWA DESTURI YA UKUHANI, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba.

Kama Zakaria alikuwa zamu ya Abiya, tutafute kwanza zamu hii ilikuwa ikiangukia mwezi gani, hii itatusaidia sana huko mbeleni kujua kwa karibu mwezi Yesu aliozaliwa.

KULIKUWA NA JUMLA YA ZAMU 24 ZA VIKUNDI AU KOO ZA KIKUHANI ZILIZOPEWA KUSHIKA ZAMU KILA KIMOJA KWA WIKI MOJA, NA ZIKIISHA, WALIANZA TENA MZUNGUKO HADI MWAKA UISHE.

1Nyakati 24:1-19 ndio tunaona mpangilio wa zamu hizo.

Kwenye mstari wa kumi, ndio zamu ya kina Abiya, yaani ule ukoo wa kina Zakaria ndio unatajwa na kuwa kwenye ZAMU YA NANE.

Tukumbuke, zamu hizi zilizingatiwa sana sana bila kuvunjwa, na hakukuwahi kuzuka sababu ya msingi ya kuvunja utaratibu wa zamu hizo.

1Nyakati 28:13, tunaona Daudi akimkabidhi Sulemani zamu hizo zitunzwe na kuzingatiwa akishamaliza ujenzi wa hekalu.

Yehoiyada naye alizizingatia na hakuwaza kuzifumua hizo zamu.

1Nyakati 23:8
..kwa maana Yehoiyada kuhani HAKUZIFUMUA ZAMU.

Hapo kwenye Luka amesema KAMA ILIVYOKUWA DESTURI YA UKUHANI.. maana yake bado zamu (courses) zilizingatiwa kama zilivyokuwa zimepangwa miaka ya nyuma kabisa enzi za Daudi. Ndio maana hadi wakati huu wanajua ni zamu ya ukoo wa Abiya.

Sasa tuendelee..

Zamu ya kina Zekaria ilikuwa ikiangukia wiki ya kumi ya mwaka. Hii ina maana ilikuwa kwenye mwezi wa tatu wa kalenda yao yaani Tammuz, na hiyo ni sawa na mwezi wa June au wa July kikwetu.

Japo kina Abia ni zamu ya nane, zamu yao haiangukii wiki ya nane kwa sababu kuna wiki mbili ambapo MAKUHANI WOTE WATASHIKA ZAMU BILA KUJALI NI ZAMU YA KINA NANI. Ni wiki ya sikukuu ya pasaka mwezi wao wa kwanza (Aviv/Abibu) kila tarehe 15-21, na wiki ya sikukuu ya Pentekoste kwenye mwezi wa Siwani/Sivan. Sikukuu hizi ni kubwa na makuhani wote walikuwa wakihudumu bila kujali zamu.

Sikukuu hizi ndio zinaisukuma mbele kidogo zamu ya Abia na kuingia kwenye wiki ya kumi ya mwaka, yaani mwezi wa Siwani sawa na May au June.

Hapa ndipo Zekaria anahudumu hekaluni maana ukoo wake umempigia kura kwamba yeye ndio aingie kuhudumu na kufukiza uvumba. Akiwa kule ndani, malaika anamtokea, na anamweleza yote kuhusu mke wake kubeba mimba na kuzaa mtoto wa kiume kwa jina la Yohana.

Sasa kumbuka unabii huu haukumaliza muda mrefu bila kutimia maana Biblia inasema "siku zile" yaani baada tu ya siku zile zile alipomaliza tu zamu yake na kurudi nyumbani.

Luka 1:24
Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba akatawa miezi mitano,...

Kwa hiyo tunaweza na ni sahihi kwamba baada kama ya wiki moja au mbili tu tangu Zakaria arudi nyumbani baada ya kumaliza ukuhani, vipimo vika-test mke wa Zekaria ni mjamzito.

Ni kwenye huo huo mwezi wa Sivan au huo uliofuata wa Tammuz sawasawa na mwezi wa June au July.

Elizabeth akatawa (akajificha/akajitenga) kwa miezi mitano, hakuonekana mtaani kirahisi.

Mwezi wa sita (Luka 1:26) wa ujauzito wake, Maria huko Nazareth anatokewa na Malaika na anaelezwa habari za kubeba mimba ya Yesu, na anapewa taarifa kwamba ndugu yake kule Yudea Elizabeth ana mimba pamoja na uzee wake, na ina miezi sita sasa.

Luka 1:36 Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa;

Wakati Elizabeth ana mimba ya miezi sita, ni kwenye mwezi wa Kislev yaani kwenye kalenda yetu ni mwezi November ama December.

Ni kipindi hicho Mimba ya mwili wa Yesu inatungwa kwenye tumbo la Mariamu maana maneno ya malaika hayakuchukua muda hata kidogo.

Yohana Mbatizaji alimzidi Yesu kiumri kwa miezi sita tu.

Kumbuka ilikuwa ni wakati ule ule wa uchumba, Yusufu anagundua Maria ni mjamzito.

Kwa vile umri wa mimba ya mwanadamu ni miezi tisa, Yesu anazaliwa kwenye mwezi wa sita wa Hebrew calendar, yaani Eluli, sawa na August au September.

Wengine husogeza mbele kidogo na kusema Yesu alizaliwa mwezi wa saba Tishrei kwenye wiki ya sikukuu ya vibanda (Sukkot) sawa na September ama October. Haina shida, ni makadirio mazuri tu.

2) WACHUNGAJI MALISHONI:

Tukumbuke, Yesu alizaliwa kipindi ambacho wachungaji (pastoralists) yaani wafugaji walikuwa wakilala na wanyama wao huko malishoni.

Ndio hao baadhi yao walitokewa kuelezwa habari za kuzaliwa kwa Yesu.

Luka 2:8-11
Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.
Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.

Kwa mwezi wa sita na saba wa kalenda yao, yaani Elul na Tishrei, ilikuwa ni kipindi cha hali ya hewa iliyo rafiki kuweza kulala na mifugo huko malishoni.

Kwa mwezi December, yaani Kislevu na Teveti, kunakuwa na baridi na hata barafu, wasingeweza kulala na mifugo nje mashambani na malishoni.

TAREHE 25 DEC ILITOKA WAPI?

Tarehe hii ina stori ndefu kweli kweli!

Tujue tu kwamba hatuna amri ya kushika au kutokushika sherehe ya birthday ya Yesu.

Kanisa la kwanza halikuwahi kuisherehekea na hakuna sikukuu hii ya Christmas kwenye Biblia.

Hatuna AGIZO la kufanya kumbukumbu hiyo, wala hatuna KATAZO la kufanya kumbukumbu hiyo.

Hatuna dhambi tusipoifanya, wala hakuna dhambi tukiifanya.

Ni jambo neutral.

Tunaweza kutenda dhambi kama tutaiadhimisha vibaya kama wapagani wafanyavyo.

Pia tukiikataa, tunaweza kutenda dhambi kutokana na njia tutakazotumia kuikataa.

Kuhusu tarehe, hatuna tarehe takatifu wala tarehe najisi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu.

Hakuna tarehe takatifu iliyoagizwa wala hakuna tarehe chafu iliyokatazwa.

Kwetu sisi Wakristo tunaungana na tarehe hii ila hatuungani na upagani wowote ulioambatanishwa na adhimisho hili la kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu.

Kuna umuhimu mkubwa sana sisi kusherehekea, ni fursa kwetu.

Dunia inaposeti tarehe kwa ajili ya Bwana wetu Yesu, tusikatae tukasema haipo kwenye Biblia.

Tuipokee, muhimu tuwe waangalifu tusitende dhambi kwa kigezo cha kuburudikia sikukuu isiyo hata kwenye Biblia.

Tuwe rohoni zaidi kuliko mwilini, tukiwaza, tukitafakari na kuhubiri umuhimu wa Yesu kuzaliwa kwetu kwa lengo la wokovu wetu.

Ni muda wa kuhubiri wokovu huu mkuu, si kufanya maovu kama wapagani wafanyavyo, kulewa, kufanya kila uchafu kwa kutumia jina la Christmas.

Christmas kwetu ni hiyo, kuhubiri maana ya ujio wa Kristo katika mwili kwa ajili ya mission ya kumkomboa mwanadamu ili apate wokovu.

USIACHE KUJIPATIA VITABU VYETU VIWILI AMBAVYO VIMEKUSANYA ZILE HABARI ZA KUSISIMUA AMBAZO BIBLIA HAIKUPATA FURSA YA KUZIANDIKA, INGAWA NI NZURI NA ZINA MAFUNZO MEMA YASIYOPINGANA NA BIBLIA. WOTE TUNAJUA KWAMBA BIBLIA ISINGEWEZA KUANDIKA KILA KITU HATA KAMA NI KIZURI.

Katika vitabu hivyo:

Utapata kuijua stori ya kweli ambayo wengi hawajawahi kukutana nayo ya Simoni, yule mchawi anayetajwa kwenye Biblia Matendo 8. Huyu twaweza kusema ndiye mchawi mtenda miujiza wa kutisha zaidi kuwahi kutokea na kuutikisa Ukristo kwa matendo yake!

Mtume Petro na Paulo walivyomshughulikia mbele ya umati wote wa jiji la Roma wakati akiwa anapaa, ni tukio tukufu la kupaswa kuhadithia vizazi vyetu, ingawa anguko lake lilisababisha visasi vibaya ikiwemo kuuawa kwa Mtume Petro na Paulo, na tumekueleza kwa kina jinsi walivyouawa na miujiza iliyotokea siku hiyo walipouawa.

Katika vitabu hivyo utapata pia zile nyaraka za mambo ya kale yaliyogundulika hivi karibuni nchini Uturuki, Israeli pamoja na Italia, kuhusiana na habari za Yesu zilizokuwa zimefichwa na wale waliomchukia. Moja ya nyaraka muhimu iliyopatikana ni pamoja na hii yenye mahojiano waliyowahi kufanyiwa enzi hizo Mariamu mama yake Yesu, Josefu baba yake, Martha na Maria dada zake Lazaro, na mtu aitwaye Masaliani.

Utamfahamu Yesu kiundani tangu utoto wake, maisha yake ya kawaida na tabia zake akiwa nyumbani, na alichokuwa akifanya nyumbani hasa kukitokea ugomvi. Pia utafahamu kuhusu tabia ya ajabu aliyokuwa nayo kwenye kula kwake na kuvaa kwake.

Utamwona Mariamu alivyokuwa akiudhika kwa vile Yesu alivyokuwa hahangaiki kutafuta utajiri, mke, umaarufu, wala kujijenga kisiasa, akiamini Yesu angekuwa mfalme wa siasa za kidunia.

Utamwona pia Martha dada yake Lazaro alivyokiri kutamani kuwa mke wa Yesu, lakini soma uone jinsi Yesu alivyokuwa akiishi dhidi ya wadada, hadi watoto wadogo wa kike.

Pia, utayajua maisha ya Yohana Mbatizaji ambayo Biblia haikuandika. Biblia imetuacha na maswali kadhaa kumhusu Yohana Mbatizaji: Mfano, Yohana aliweza vipi kuishi ndani ya jangwa lile hatari la Yudea, tena tangu akiwa mtoto mdogo? Alifikishwaje katikati ya milima hatari ya jangwa lile? Soma utapata majibu na pia utaona jinsi malaika walivyomlea Yohana tangu akiwa mtoto mdogo hadi alipokuwa mtu mzima na kuanza huduma rasmi.

Hatukuacha kukupa vile visa vya kusisimua vya jinsi Pontio Pilato pamoja na Kuhani Mkuu Kayafa walivyokuja kuupojea Ukristo baada ya kushiriki kumtoa Yesu asulibiwe.

Kama unasumbuliwa na yale mawazo kwamba una matatizo magumu sana kiasi kwamba Mungu hawezi kukutoa hapo, tafadhali hakikisha kwa nguvu zako zote unasoma ushuhuda wa maisha ya Bernard kwenye kitabu hiki. Mwone Bernard kutoka Ghana, mtoto wa kahaba aliyekulia majalalani, akaugua ya kufa, akamjua Mungu, hadi kualikwa White House na Rais wa Marekani, leo akiwa ni mtu aliyefanikiwa sana duniani.

Stori ya wale majitu wanefili waliotajwa kwenye Mwanzo sita hatukuiacha, utawajua kwa undani na visa vyao vya kutisha vilivyomfanya Mungu afute dunia kwa mafuriko ya enzi za Nuhu na kuanza upya uumbaji.

Mwisho, tumekupa stori yote kuhusu lile sanduku la Agano, tangu kutengenezwa kwake, miujiza yake, na mambo ya ajabu yaliyotokea siku ile lilipopotea hadi leo.

Kitabu kimoja kina kurasa 92, kingine kina kurasa 104.

Vyote vinapatikana kwa shilingi 20,000 pekee.

Kama unataka hard copy utafikishiwa ulipo. Kama unataka soft copy utazipata kupitia whatsapp.

Wasiliana nasi kwa namba 0762731869.

Hiyo ni namba ya whatsapp na kupiga pia.
 
Hiyo biashara yako hatuitaki kwa ufupi.
Yesu amezaliwa Machi 20 .
Tunasherehekea siku ya 25 December kwakuwa hiyo ilikuwa siku maalumu ya miungu ya kipagani , hivyo Yesu kavunja ngome zote za Wapagani na ibada zao.
Tumemshinda ibilisi
 
Msingi wa dini ni kuungaunga uongo mpaka uaminike kuwa ukweli.

Ukishangaa tarehe ya kuzakiwa Yesu wakati mpaka leo hakuna aliyethibitisha Mungu yupo na watu wanaamini yupo, nitakuona unapoteza thamani ya kushangaa bure.

Yani watu wamejidanganya Mungu yupo, wakati hayupo.

Halafu wewe unashangaa wakijiundia tarehe tu na kuadhimisha kuzaliwa Mungu?

Hawa watu wameacha mantiki, wanaungaunga tu wanavyojitakia kiimani.

Kwa nini unataka kuingiza mantiki kwenye imani yao?
 
  • Masikitiko
Reactions: K11

Usingeweka matangazo ya vitabu vyako ningekupongeza sana kwa Analysis yako. Lakini pia hujahitimisha mada. Mimi nikipata nafasi nitakuelezeni Yesu kazaliwa lini.
 
Kama ndio Ili mkristo ajue kuwa Yesu hakuzaliwa 25 December inabidi asome huo Uzi wote ni Bora tu aendelee kuamini kuwa Yesu alizaliwa 25 December
 
Laiti maelezo, haya marefu yangekuwa ni maelezo jinsi ya kutumia tekinolojia kutatua tatizo la ajira kwa vijana, kuboresha kilimo, kukuza viwanda, ingekuwa jwmbo la maana Sana, no body cares about exact date ya Yesu alizaliwa lini, we just celebrate him, that's all, haya Mambo ya kuchambua vitu vinavyokuzidi umri kwa miaka 2000+! It's wasting of time, leta mada za kufundisha ili kuboresha maisha ya watu, how to think properly, uwekezaji, malezi,sio Mambo ya vumbi la Kongo, na upuuzi mwingine
 
  • Thanks
Reactions: K11

Similar Discussions

Back
Top Bottom