kijanamtanashati
JF-Expert Member
- Aug 22, 2014
- 523
- 916
nimesikitika kuona baadhi ya nchi wanaendekeza udini kupita maelezo. nipo uturuki kwa mda kama mwezi kikazi. nimeshangaa kuona leo dunia inaadhimisha sikuku ya kuzaliwa yesu lakini kwa hii nchi tofauti kidogo. watu wameenda kazini, vyuoni, shule na shughuli zote za maendeleo zinaendelea kama kawaida. nimemuuliza dogo mmoja ananiambia ndo ilivo kwa kawaida hakuna mapumziko ya chrismas wala pasaka. mapumziko ni siku za eid tu. nimesikitika kwa kweli nimekumbuka tanzania yangu. sikutegemea kama udini upo juu kiasi hiki kwa nchi kama uturuki!!!