~**~ kumbatio la mwenye makosa ~**~

~**~ kumbatio la mwenye makosa ~**~

DOOOOOONE!!!!

Asanteni kwa uvumilivu wenu, kwa baada ya miaka minne nimeweza kumaliza kisa kizima. Mmenisukumua kurudi na kuandika kidogo na kuamsha mizimu iliyokuwa imelala. Natumaini imekuwa burudani tosha kwa wengi wenu na hamtasita kuniunga mkono kiukweli - siyo kugonga senksi tu! kwenye kisa na visa vingine vya huko mbeleni. You never know.. mnaweza kuwa sehemu ya kitu kikubwa zaidi kama alivyonidokeza mshikaji wangu mmoja leo ambaye alitaka kunichapa vibao kwanini sijaandika visa hivi muda mrefu!!
 
Sura ya Saba na ya mwisho wa kisa hiki cha kusisimua inakuja ndani sasa hivi.... zingatieni onyo.. nililotoa jana. Msichape mkaweka karibu na watoto.

Mwanakijiji mie na MJ1 tuko same boat ...hiyo sehemu ya saba naona PM zitajaa kwenye mail box yako ..
 
Sasa MMM nimwangukie character wa kwenye hadith jamani kivuli hicho ndugu yangu na enzi zile za kumfia Willy Gamba ilikuwa zamani bwana. But of course ninaheshimu utashi wako mpenzi you are not reachable ..... so najiweka pembeni nile kwa macho tu.... ntafanyaje sasa nami kukuteka siwezi.... lol.

nashukuru kwa kuelewa.. ur a sport and a scholar!
 
mwanakijiji mie nataka nije na ukosoaji wa kiuandishi ................ninaruhusiwa?
 
Mwanakijiji asante sana kwa burudani,ila hii sehemu ya mwisho.....mie simo!
 
1. seriously mwanakijiji unatumia brackets kwenye story book...............seriously!
 
Aksante MMM kwa burudani. Nimefurahi kuwa at the end dada yangu Clementina akili yake imerudi haraka. Jamani ni kweli kabisa sometimes wanandoa tunajidanganya kutafuta faraja nje ya mahusiano yetu ya halali lakini huwa si suluhisho hata kidogo. Mambo yote yako kwa wenzi wetu wa halali.

Ila MMM ungemfunua kidooooogo Freddy kwa maswali alokuwa akijiuliza Clementina ningefurahi yaani tujue kama Freddy ni mtoto wa mjini au lah maana umetuacha na kiu shemeji.
 
I salute you Mwanakijiji well well done utunzi mzuri umefanikiwa kuteka mawazo yetu
ThankYouBlueSparkle.gif
 
Aksante MMM kwa burudani. Nimefurahi kuwa at the end dada yangu Clementina akili yake imerudi haraka. Jamani ni kweli kabisa sometimes wanandoa tunajidanganya kutafuta faraja nje ya mahusiano yetu ya halali lakini huwa si suluhisho hata kidogo. Mambo yote yako kwa wenzi wetu wa halali.

Ila MMM ungemfunua kidooooogo Freddy kwa maswali alokuwa akijiuliza Clementina ningefurahi yaani tujue kama Freddy ni mtoto wa mjini au lah maana umetuacha na kiu shemeji.

of course lazima kuna part 2...
 
Aksante shemeji sasaaa.............duh sijui ntaambiwa nina kimuhemuhe? ah naliza tu bana

Sasa MMM baba lini tutegemee Part 2 ya hii Kumbatio la Mwenye Makosa?

mbona nimedokeza...? watakaopata "Uso kwa Uso" watashangaa suprise iliyomo...LOL
 
mwanakijiji .........sie wengine tuna masuali au tunataka kutoa critism kwenye uandishi, twaruhusiwa?
 
mwanakijiji kwa vile umetoa ruhusa mie nitakuja na ukosoaji wa kiuandishi

1. Matumizi ya Mabano (brackets)
Sijawahi kuona kitabu cha hadithi kuwa na bracket ndani yake. It doesnt sit well when u read. Kama maelezo hayo ya ndani ya Bracket ni muhimu basi ni bora kama ungeyatafutia njia ya kuyaandika nje ya bracket.

2. Kuelezea kwa undani vitu ambavyo havina athari kwenye plot moja kwa moja
Umeelezea vizuri sana na kwa kina kuhusu sherehe za muungano (zaidi ya nusu ya kurasa moja) ambayo haikuwa na haja hata kidogo kwa kuwa unamtoa msomaji wako kwenye maudhui yenyewe unampeleka kwenye kitu ambacho hakina athari kwenye hadithi yenyewe.

3. Kufananisha kitu kimoja na chengine mno kwenye hadithi
sijui ndo inaitwaje kwa kiswahili ........lakini mfano umesema something like 'akitizama paja langu lililonona kama punda milia wa serengeti' au 'kumsimamia mbele bila nguo sawa na panya kusimama mbele ya paka na kumshikia kiuono' na kadhalika na kadhalika.
Unapokuwa na hizi nyingi kwanza moja unampunguzia msomaji wako uhuru wa kufikiri
pili nafikiri pia zinamtoa msomaji kutoka hadithi yenyewe...............maana do u want us to think of the ugomvi baina ya hawa wawili au about panya kashika kiuono!

4: italics
Kwa kweli i didnt get the way you used italics. mwishowe nilihisi labda ni kwa ajili ya kushadidia jambo......but sometimes it felt like it wasnt the case. Sikuelewa matumizi yako ya italics katika hadithi hii..............naomba ufafanuzi
 
Chief! kama kawa naipeleka home tukaisome kwa pamoja...............ahahahahaha! ukifululiza hadithi kama hizi tatu nyingine nakwambia jnr atapata mdogowe sasa hivi!:target::target::target:

Thank you chief!
 
mwanakijiji kwa vile umetoa ruhusa mie nitakuja na ukosoaji wa kiuandishi

1. Matumizi ya Mabano (brackets)
Sijawahi kuona kitabu cha hadithi kuwa na bracket ndani yake. It doesnt sit well when u read. Kama maelezo hayo ya ndani ya Bracket ni muhimu basi ni bora kama ungeyatafutia njia ya kuyaandika nje ya bracket.

true and point well taken.

2. Kuelezea kwa undani vitu ambavyo havina athari kwenye plot moja kwa moja
Umeelezea vizuri sana na kwa kina kuhusu sherehe za muungano (zaidi ya nusu ya kurasa moja) ambayo haikuwa na haja hata kidogo kwa kuwa unamtoa msomaji wako kwenye maudhui yenyewe unampeleka kwenye kitu ambacho hakina athari kwenye hadithi yenyewe.

Ni kweli, wakati mwingine hata hivyo nafanya makusudi (na waandishi wengine hufanya vile vile) kutengeneza mazingira nje ya tukio na hivyo kwa makusudi kabisa unamtoa mtu kwenye stori line na kumrudisha tena. Labda haitakiwi kwa undani hivyo kama huko nje hakuhusiani sana na kilichokuwa kinaendelea.

3. Kufananisha kitu kimoja na chengine mno kwenye hadithi
sijui ndo inaitwaje kwa kiswahili ........lakini mfano umesema something like 'akitizama paja langu lililonona kama punda milia wa serengeti' au 'kumsimamia mbele bila nguo sawa na panya kusimama mbele ya paka na kumshikia kiuono' na kadhalika na kadhalika.
Unapokuwa na hizi nyingi kwanza moja unampunguzia msomaji wako uhuru wa kufikiri
pili nafikiri pia zinamtoa msomaji kutoka hadithi yenyewe...............maana do u want us to think of the ugomvi baina ya hawa wawili au about panya kashika kiuono!

Hii ni kweli, nikiwa na muda mzuri wa kuhariri najua ningepunguza hivi sana. Ni mojawapo ya mambo mwandishi unatakiwa kuwa mwangalifu sana. Matumizi ya simile..

4: italics
Kwa kweli i didnt get the way you used italics. mwishowe nilihisi labda ni kwa ajili ya kushadidia jambo......but sometimes it felt like it wasnt the case. Sikuelewa matumizi yako ya italics katika hadithi hii..............naomba ufafanuzi

Kama umefuatilia vizuri utaona italiki zinatumika humu aidha kuashiria mawazo ya kile ambacho anakifikiria kimoyomoyo au kitu anachokisema akiwa na maana zaidi ya kinachotamkwa.

Asante sana.
 
Back
Top Bottom