Mke wangu ana kadi mbili za kliniki, moja jina langu, lingine la bwana mwingine!

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
609
Habari wanajamvi,

Nimeamini usemi usemao usione watu wanaangua vicheko barabarani na wakati mwingine hadi machozi yanawamwagika kutokana na sababu mbalimbali, Ni kweli kwamba yapo machozi ya furaha lakini pia machozi mengine ni uchungu unaoonekana kama aina fulani ya furaha.

Mtu anaweza kucheka lakini siyo kweli anacheka kutoka moyoni bali anajaribu kuficha yanayomkera lakini katika kujipa moyo anashiriki kicheko pale anapozungumza na jamaa au rafiki yake.Huo ni ukweli.

Ushiriki huu wa kicheko, hakika humpunguzia mawazo fulani kwani vile nijuavyo mimi kicheko ni afya. Hufanya hata makunyanzi kwenye uso kupotea kwa muda.

Lakini pia kipo kicheko cha ukweli kinachotokana na jambo fulani la kufurahisha alilokujulisha mwenzako na katika kuonyesha wingi wa furaha, chozi nalo hujikuta likimwagika. Je, imewahi kukutokea hivyo? Mimi Yes!mara nyingi tu.

Naam, nimeanza hivyo ili kukuweka sawa kwa kile tutakachojadili hapa chini kwamba usione watu wanapita barabarani, wako maofisini wakichapa kazi ukadhani wana furaha tele moyoni.

Pale kazini wanajitahidi au niseme wanajitutumua tu kutimiza wajibu lakini baadhi wanapofikiria kule majumbani wanakotoka, mapigo ya moyo huenda mbio na afadhali kama angeambiwa apige mbio lakini yanamdunda wakati katulia tuli. Kisa amekumbuka vitimbi vya nyumbani kwake.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28, nimejaliwa kufunga ndoa na mke wangu miaka 4 iliyopita, ingawa tumechelewa kupata mtoto lakini ndoa yetu ina upendo na amani ninaishi Dar.

Mwezi wa Machi mwaka huu, mke wangu alifanikiwa kupata ujauzito kitu ambacho kimeongeza upendo ndani ya nyumba yetu na mimi najitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha mke wangu anapata mahitaji yake yote muhimu kiasi kwamba hakuna kitu anachokikosa.

Hata hivyo, kilichonifanya niombe ushauri kutoka kwenu wana JF kwa ujumla, ni kwamba hivi karibuni nimemfuma mke wangu kwenye kabati lake la nguo nimekuta ana kadi mbili za kliniki, moja ina jina langu na ya pili ina jina la bwana mwingine hizo kadi zote kaziandikisha vituo tofauti vya Afya (Majina ya yule bwana mwingine ninayo).

Angalia Mungu alivyo mwema, amenielekeza hadi nikaziona kadi zile kunidhihirishia kuwa mke wangu siyo mwaminifu na lipo au yapo mambo mengi labda bado ananificha.

Kwa kweli baada ya kuzifuma kadi hizo nilichokifanya nilizirudisha nilipozikuta na mpaka hivi sasa mke wangu hajui chochote kinachoendelea.

Ndugu wanajamvi Madam B, Watu8, @KakaKiiza, KakaJambzi, FROWIN, Tutor, ASHUA, na wengineo, mwenzenu yamenikuta nimebaki njia panda kiasi kwamba nashindwa la kufanya. Naombeni ushauri wenu kabla sijachukua uamuzi wowote.

Wasalaam.
 
Tembelea vituo vya afya ukachunguze afya yako hasa uzazi pengine mkeo alipona mnakaa ndani ya ndoa pasipo mafanikio ya ujauzito akauza mechi sasa yupo njia panda ajui mimba yako au ya jamaa maana wote mlikuwa mnamtumia
 
Mkuu shikamoo. Maana wewe ni mkubwa tayari kwangu.
Cha kwanza kabisa ujue Mungu anakupenda na ndio maana hayo mambo yamefunuka kwako.
Pili kuwa mpole usiwe na papara kutoa uamuzi na usipunguze upendo kwa mkeo kwa namna yoyote ile.
Tatu anza sasa kufanya uchunguzi kwa makini..kuna maswali unaweza jiuliza ili kupata pa kuanzia kwa mfano
1. Nini msingi wa ndoa yenu? je ni upendo? pesa?....nk
2. Mlipitia nini wakati wa uchumba? alishawahi kukusaliti ai wewe ulimsaliti?
3. Rejea afya yako ya uzazi...unatatizo lolote? Ulishaonana na daktari akakupima?
Mkuu ukijibu hayo maswali tayari utakuwa na uamuzi mkononi. Lakini mwisho wa yote...mwenye kujua ukweli ni huyo mkeo hivyo basi pamoja na tafiti zote ulizo fanya hakikisha unambana mkeo pia akupe ukweli.
Jioni njema mkuu. Pia pole sana maaana najua hapo kichwa kiko na mawazo mengi na yasiyo na majibu.
 
Huyo mtoto usikute ni wako umebambikiwa. Hizo kadi mbili huwezi jua ya bwana gani anachunwa.
Kafanye DNA upate cha kuongea na mke wako.
 
Toa copy tena ya rangi kadi zote mbili au uzifanyie scan na uzisave kama soft copy, ndio ufanye subra na uchunguzi wako kiasi kwamba akiziharibu hizo kadi basi wewe unakuwa na backup

Chukua ushauri huu ndugu atakuja kukukana huyo hadharani kuna uwezejano hata huyo mtoto sio wako!
 
Huyo mtoto usikute ni wako umebambikiwa. Hizo kadi mbili huwezi jua ya bwana gani anachunwa.
Kafanye DNA upate cha kuongea na mke wako.

Mkuu shikamoo. Maana wewe ni mkubwa tayari kwangu.
Cha kwanza kabisa ujue Mungu anakupenda na ndio maana hayo mambo yamefunuka kwako.
Pili kuwa mpole usiwe na papara kutoa uamuzi na usipunguze upendo kwa mkeo kwa namna yoyote ile.

3. Rejea afya yako ya uzazi...unatatizo lolote? Ulishaonana na daktari akakupima?

Nawashukuru wakuu ila hatujawahi kuchelewa kupata mtoto pale tulipohitaji kuzaa, pia nawashukuru kwa ushauri kwamaana yawezekana nina matatizo bila kujijua japokuwa awali tulikuwa tunaangalia siku ya kufanya mapenzi kuwa iko salama au la hadi pale tulipoamua kuwa na mtoto.
 
Mkuu jua kabisa wewe si babakijacho .... miaka minne ya ndoa bila mtoto... na hapa mach 2015 ujauzito ukapatikana na baada ya hapo Mungu alivyo mwema kakuonyesha baba mwenzio...

So ushaur hapo ni kushirikisha ndugu zako wa karibu wakushauri zaid... binafs mie tafuta kipimo cha DNA then uchukue maamuz baada ya results zake kutoka
 
Hahahaaaa, hii noma sana lakini kumbuka kuna baadhi ya wanasiasa wanamiliki na wanaendelea kulipia kadi za vyama viwili tofauti hali wana cheo kikubwa tu ndani ya chama kimojawapo kati ya hivyo.
 
Back
Top Bottom