Kukosekana kwa machinjio rasmi ya mifugo Rufiji, Pwani ni kero na hatari kwa afya

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Kwa sisi wakazi wa Wilaya ya Rufiji iliyopo Mkoa wa Pwani tangu nchi ipate uhuru hapajawahi kujengwa machinjio rasmi ya kuchinjia nyama kama zilivyo wilaya nyingine.

Pamoja na kuwa wafanyabiashara wanalipa ushuru wa ng’ombe minadani, vizuizi vya njiani (mageti ya ushuru) na kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), hatujui hizo hela zinafanyiwa kitu gani mpaka leo.

Wamiliki wa mabucha wanachinjia mifugo sehemu zisizo rasmi, kitendo kinachohatarisha afya zetu sisi wananchi (walaji), hususani mji wa Ikwiriri.
 
Back
Top Bottom