KWELI Kukimbia au kufanya Mazoezi katika Barabara zinazotumiwa na Vyombo vya Moto ni hatari kwa Afya

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Licha ya kuwa Mazoezi husaidia kujenga na kulinda Afya, kuna masuala muhimu ya kuzingatia kabla ya kuanza mazoezi ikiwemo kuchagua eneo la kufanyia mazoezi ambalo litakuwa salama kimiundombinu na kimazingira.

Katika siku za hivi karibuni watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi katika maeneo ya jirani au pembezoni mwa Barabara zinazotumiwa na Vyombo vya Moto (Magari, Pikipiki Bajaj na Mitambo mbalimbali) hali inayodaiwa kuwa watu hao huvuta hewa chafu.

Je kuna ukweli wowote hapo?

1690100123344.png
 
Tunachokijua
Mazoezi ya mwili ni njia bora ya kuongeza utimamu wa mwili pamoja na kujikinga na magonjwa. Mazoezi ya mara kwa mara ya kimwili yanaweza kuongeza uzalishaji wa homoni zinazokufanya uhisi furaha na kukusaidia kulala vizuri.

Yanaweza pia kuboresha mwonekano wa ngozi, kupunguza uzito wa mwili, kupunguza hatari ya kuugua magonjwa sugu pamoja na kuboresha ufanisi katika kushiriki tendo la ndoa.

Shirika la Afya Duniani (WHO) hushauri walau kila mtu mwenye umri wa kati ya miaka 18-64 kufanya mazoezi kwa jumla ya dakika 150 kwa wiki ili kuimarisha afya ya mwili.

Kufanya mazoezi pembezoni mwa barabara
Tafiti nyingi zimegundua kuwa kufanya mazoezi karibu na mazingira tenye uchafuzi wa hewa unaohusiana na vyombo vya usafiri huathiri vibaya Mfumo wa upumuaji. Madhara ya muda mfupi ni kusababisha kukohoa, kubana kwa kifua, na kupumua.

Ushahidi pia unaonyesha kuwa inaweza kuongeza mapigo ya moyo na kupumua kwa wanariadha.

Madhara ya kiafya ya muda mrefu ya kufanya mazoezi karibu na kwenye mazingira haya hayako wazi sana. Hata hivyo, ushahidi tulionao juu ya uchafuzi wa hewa kwa ujumla unaonyesha kwamba baada ya muda, hewa chafu inaweza kudhoofisha mfumo wa kinga na utafiti unahusisha na hatari ya kuongezeka kwa hali ya afya kama magonjwa wa moyo, pumu, kupungua kwa utambuzi, na magonjwa ya mfumo wa upumuaji.

Wakati huo huo, mazoezi huja na manufaa makubwa kiafya na inajulikana kupunguza hatari yetu ya kupata hali nyingi sawa, ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa moyo , matatizo ya mapafu, na vifo kwa ujumla. Ni mlinzi bora wa afya na takwimu inaonesha mara kwa mara kuwa mazoezi ya kawaida ya mwili yanaweza kupunguza baadhi ya athari mbaya za kiafya zinazosababishwa na uchafuzi wa hewa.

Kwa hivyo, tunaendelea kufanya mazoezi nje na karibu na barabara kuu? Au ikiwa kukimbia barabarani ndio chaguo letu pekee, Je, tunapaswa kuacha? Haya ndiyo unayohitaji kujua kabla ya kukimbia kwenye barabara yenye shughuli nyingi zaidi katika mtaa wako.

Jinsi moshi wa Magari unavyoathiri afya zetu
Kwa mujibu wa Dr. Mary Prunicki , MD, Ph.D, mkurugenzi wa uchafuzi wa hewa na utafiti wa afya katika Kituo cha Sean N. Parker cha Utafiti wa mzio (Allergy), Stanford Medicine, miji mingi mikubwa huwa na kiwango kikubwa cha hewa chafu ambayo ni mchanganyiko wa nitrogen dioxide, benzene na kemikali nyingine mbaya.

Mara baada ya kuvuta pumzi yenye hewa hii, chembechembe ndogo zinaweza kuingia kwenye njia ya upumuaji na kusababisha kuwasha kwa koo, kikohozi au kusababisha maumivu ya kifua.

Utafiti unaoangazia matokeo ya kiafya ya watu wanaoishi karibu na barabara zenye shughuli nyingi umehusisha mazingira haya na kuongezeka kwa wagonjwa wa pumu, kupungua kwa utendaji wa mapafu na matatizo ya moyo na mishipa ya damu. Wale walio na hali za kiafya, kama vile pumu au ugonjwa wa moyo, huwa na hisia kali zaidi kwa mazingira haya.

Tunapofanya kazi, tunapumua hewa zaidi. Utafiti unaonyesha kwamba mtu anayekimbia katika eneo lenye uchafu atavuta chembe nyingi zaidi ikilinganishwa na mtu anayetembea au ameketi kwenye gari lake.

Utafiti mwingine uligundua kuwa mbio za marathon zinazofanyika kwenye miji iliyo na uchafuzi mkubwa wa hewa huongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya chembe zinazoingia kwenye njia ya upumuaji, ikizingatiwa wakimbiaji wanapumua kwa bidii kwa muda mrefu.

Uwepo wa Ajali
Pamoja na athari tajwa kwa afya zinazosababishwa na upumuaji wa hewa chafu pembezoni mwa barabara kuu, watu wengi pia wamekuwa wanapatwa na ajali nyingi zinazoondoa uhai wao, au hata kuwaachia ulemavu wa kudumu.

Mathalani, Julai 22, 2023, tukio moja lilitokea Mwanza ambapo watu 6 walipoteza maisha kwa kugongwa na gari wakati wakifanya mazoezi barabarani.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hii, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya alisema watu wengine 16 waliokuwepo kwenye mazoezi hayo walijeruhiwa pia.

Mtumiaji wa Twitter anayefahamika kwa jina la Ginimbi, Julai 22, 2023 alitoa pia ushuhuda wake kuhusu hatari ya kufanya mazoezi barabarani. Aliandika;

"Nakumbuka tarehe 01/03/2022 niliwahi kugongwa na pikipiki saa 12 alfajiri nikiwa nafanya mazoezi ya kukimbia kutoka Mazimbu kuelekea Mzumbe University eneo la Kasanga. Ni hatari sana kukimbia barabarani! MUNGU alininusuru lakini bodaboda alifariki papo hapo. R. I. P Bro"

Mtumiaji mwingine wa Mtandao wa Twitter, Januari 30, 2023 alitoa angalizo kwa watu wanaofanya mazoezi pembezoni mwa barabara.

"Epuka kuvaa headphone wakati wa kufanya mazoezi ya kukimbia pembezoni mwa barabara yenye vyombo vya moto vingii hii uenda ikakuepusha na ajali mbaya ambayo pengine ikaweka historia kwenye maisha yako"

Ajali za aina hizi zimekuwepo kwa muda mrefu na zinaendelea kutokea hadi sasa.

Ushauri
Pamoja na uwepo wa faida nyingi za mazoezi katika kuimarisha afya ya binadamu, ni muhimu kuyafanya kwenye sehemu ambazo hazihatarishi maisha.

Maeneo ya pembezoni mwa barabara huwa na kiasi kikubwa cha hewa chafu, pia vyombo vya usafiri vinavyopita maeneno hayo ni hatari kwa usalama wako.
Ndiyo ni hatari kiafya na pia kiusalama ,jana wafanya jogging 10 mwanza wamefariki kwa kugongwa na gari.
 
mazoez n afya,yanatujenga,yanatupa utulivu na furaha..na kimsingi ukishazoea mazoez n ngumu kuacha.

Hoja yangu n kusaidiana namna bora ya kuweza kufanya mazoezi haya kulingana na mazingira yetu…nmeona taarifa ya ajali ilyotokea 22 july mwanza ilyokua wanariadha 6 na wengne kujeruhiwa baada ya gari kupoteza mwelekeo

Tushauriane nn chakufanya,mana viwanja n vichache na vibovu sana,kukimbia ndio zoez muhmu kulko yote huwez kufaAAAA au aa wa aaq forget asante AAA
 
Ndiyo ni hatari kiafya na pia kiusalama ,jana wafanya jogging 10 mwanza wamefariki kwa kugongwa na gari.
Kukimbia barabarani ni adventurous tofauti na kukimbia kuuzunguka uwanja.
Tatizo barabara zetu nyingi si salama si tu kwa wakimbiaji bali watembea kwa miguu. Kiufupi si salama kwa mijongeo.

Hadhari ni muhimu unapokimbia kuwa upande sahihi, kutovaa earphone, na kubana pumzi pindi vyombo vya moto vinapotoa hewa chafu ili kujizuia kuivuta hewa chafu kwa sekunde kadhaa. Na hili si tu kwa wakimbiaji bali hata watu wengine watumiaji wa barabara.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom