Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,755
Nikiwasalimu itikieni
Enzi za Mwalimu, Ikulu ya Dar ilikuwa na uzio wa michongoma na maua sambamba na uzio wa wavu eneo lenye wanyamapori wanaofugwa Ikulu. Enzi hizo tuliweza kuona uzuri na umaridadi wa Ikulu yetu. Wapita njia hususan wageni waliweza kutembea pembeni ya uzio wa Ikulu bila kusumbuliwa
Alipokuja mzee Mwinyi alijenga ukuta kuzunguka ikulu, lakini haukuwa ukuta wa kumnyima mpitanjia kujionea umaridadi wa jengo letu linaloendeshwa na kutunzwa na kodi zetu.
Alikuja mzee Mkapa ambaye hakukuwa na heka heka nyingi bali aliruhusu wapitanjia kutembea pembezoni mwa uzio huku wakijionea ufahari wa Ikulu yetu.
Ukarabati mkubwa wa Ikulu (badala ya kuanza ujenzi wa Dodoma) ulifanyika chini ya Jakaya, tukaanza kuona mabadiluko machache, upande wa barabara ya Barack Obama ilianza kufungwa usiku kuzuia magari kupita. Lakini wapitanjia waliruhusiwa kupita. Upande wa Wanyama wanaofugwa Ikulu ukawekwa Uzio kuziba wanyama wasionekane na wapitanjia. Tulianza kupata mashaka labda wameuzwa kwa sababu wale wanyama walipungua sana kabla hakujazibwa kabisa wasionekane....
Kasheshe alipokuja mpendwa wetu JPM, barabara ya Barack Obama ikafungwa kabisa hakuna raia kupita, na hata wapita njia walizuiwa, kibaya zaidi hadi sasa raia anayetembea nje ya ukuta wa Ikulu anashughulikiwa kikatili na wale walinzi waliovaa makirikiri. Hali hii imedumu hadi kwa rais wa sasa. Tunachojiuliza Watanzania kadhaa ni kwamba, kuna tishio gani la usalama kiasi ya kuwekwa makatazo hayo? Au kuna biashara gani zinaendelea Ikulu kiasi kwamba wapitanjia wanaweza kuiba siri?
Inaonesha kuwa Serikali imeweka alert dhidi ya raia wake na haina imani nao na kibaya zaidi, vyombo vya dola vimejimilikisha jengo na mandhari ya Ikulu huku vikijua wazi kabisa kuwa ile ni kodi za wananchi.
Kama endapo lengo ni ulinzi. Watafakari uwezo wao wa kulinda lile jengo bila kujenga hofu kwa wapitanjia .
Lakini, kitu muhimu ni kwamba, kadiri wanavyoiweka Ikulu mbali na wananchi ndivyo wwnavyomjengea mazingira magumu sana mkazi namba moja pale Ikulu hadi kupelekea kupoteza umaarufu. Kusimika mabango na public mentioning ya rais ni utamaduni uliobuniwa kuhakikisha anapata umaarufu wa LAZIMA badala ya kufanya mambo ya msingi zaidi.
Natoa rai kwa wwhusika, wasipore ama kuitenganisha Ikulu na Tanzania. Kama wanaona ni muhimu kufanya hivyo basi wabuni miradi ya uwekezaji ya kuiendesha Ikulu na wasitegemee kodi zetu.
Jambo la kuzingatia. Ikulu ya Chamwino ina privacy nzuri na maridhawa kwa rais, itoshe kwa yeye kufanyiakazi na kuishi kule na aruhusu barabara zilizokuwa zinapitika zamani kuelekea na kutoka Kivukoni kutumika.