Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,988
Mhe. Sagini ametoa maagizo hayo Novemba 25, 2023 katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua Miradi mbalimbali ya Ujenzi inayotekelezwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi hiyo
"Niwatake wakandarasi kuongeza nguvu kazi ili kuwahisha utekelezaji wa miradi kwa kuzingatia ubora unaotakiwa na ikiwezekana ongezeni muda wa kufanya kazi na hakikisheni vifaa vyote vimenunuliwa ili kurahisisha Ujenzi," Amesema Mhe. Sagini
Aidha Mhe. Sagini ametembelea na kukagua Ujenzi wa Kituo cha Polisi, Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Nyumba Sita za Askari Polisi, Mradi wa Ufyatuaji tofali wa Gereza Geita.