Kujiajiri/Ujasiriamali ni homa ambayo ikikushika haitoki, ila wahitimu wengi vyuo vikuu wana chanjo tayari!

RAFA_01

Senior Member
Aug 10, 2022
104
169
Graduates wengi tunachanganywa na vyeti vyetu na zile picha za majoho kwamba tukimaliza tunategemea kwenda kufanya kazki katika shining new office, tupige picha na kupost kuonyesha colleagues kwamba tumefanikiwa.

Hii inatokeo kwa baadhi ya watu wanabahatika wanapata kazi mapema na wengine ndio wanachelewa hawapati/hawajapata Mpaka leo.

Unafanya nini sasa kama umekosa kazi?
Ntazungumzia mimi sababu najua humu hamna graduates kihivyo, wengi wenu ni watu wazima. Ila mimi nimesaidiwa na mtu ambae hata leo simkumbuki kwa jina alikuwa jamaa tu alidai ana njaa akaniuzia kitabu Njiani “Cashflow Quadrant by Robert Kiyosaki” Kwa Buku (1000 Tsh/=). Kile kitabu sikukisoma right away... nilikiacha nkakiweka lakin baadae nikapata mda nkakisoma kimenifungua akili sana. Baada ya hapo nkasoma “The Small Business Bible”- by Steven D. Strauss

Nipo na small retail shop ambayo haifanyi vizuri kivile mpaka sasa ila nna furaha sababu nafanya vitu navyovipenda. kutokana na hayo mauzo madogo ili kuboost nmeongeza online presence kwahiyo nna official website ya kuhuzu hizo electronics accessories, Kama nilivyosema biashara haiko booming ila nna furaha Sababu inaniumiza kichwa ku operate kila kitu finance, sales, Marketing kila kitu nafanya mwenyewe inatesa asikwambie mtu ila at the same time it’s fun.

Tatizo linakuja kwa Wazazi, Marafiki na Colleagues linapokuja swala la Interviews. Nili apply for jobs kipindi hiko sasa siku hizi siendi na nisipoenda naulizwa simu kibao. kiukweli niko kwenye safari mpya nna degree ila bado naona sina maarifa ya kutosha bado ni mgeni sijui kitu, though nna degree field ya business. Kwa kusema ukweli elimu ya chuo inansaidia kwa kiasi chake watu wasidharau elimu.

Wazazi wanafikia kusema kua “una matatizo gani kusoma umesoma kazi hautaki?” Hawajui kuwa interview sio guarantee ya kazi. Mind you nimegraduate with honors sio kwamba nna cheti kibaya hapana.

Kweli labda napoteza maana nlkuwa nakaa kwangu ila sasa hivi niko kwa wazazi nimerudi kupunguza matumizi ya kodi, najikusanya nafanya Delivery kwa wateja wa online pamoja Freelancing Remotely kwa ujuzi nliioupata shulen japo wateja ndio changamoto, Marketing inahitajika paid ads hapo pesa tena. kule Kuna mtu ana operate Brick & Mortar kwenye kale ka store napata faraja atleast nimerahisisha maisha ya mtu mmoja.

Sema hii safari ni ngumu maana kila mtu anakwambia biashara ngumu, biashara ngumu... Kuanzia wazazi wako, familia na Marafiki wote.

Nasoma vitabu nasikiliza podcasts nafanya kazi still bado earnings inasua sua... wenzangu walio kwenye kazi wanaflex nilisema sitaangaika na 9-5 Job...nikisema nianze kuangaika ntakuwa narudi nyuma...(You can quit anytime, why Now?) niko na deal na computer na simu always reading...mpaka macho naona yanaanza kuuma natafuta Anti-Blue ray glasses huku nikiamini mambo yatakuwa sawa.

Kujiajiri sio rahisi kama inavyosemwa, Kwahiyo vijana wengi wanavyolalamika ukosefu wa ajira ni kwamba wanaogopa hii safari sababu sio rahisi.

Mungu akisaidia nkiweza toboa nataka ntafute njia ya kuwasaidia vijana wenzangu kutoka katika hili tatizo. Na document kila kitu ili ntumie kama learning tools kwa wengine.

Kwa yeyote mwenye Marketing Tips au ushauri ningefurahi kusikia kutoka kwenu wazoefu.

Ahsante.
 
Kitu wasichojua vijana wengi ni kuwa mafanikio si kazi rahisi na inahitaji muda mwingi sana. Labda kwa wale wanaorithi biashara za wazazi hapo inaweza kuwa rahisi. Ila kwa anayeanza from the scratch, si masihara Mzee. Funga mkanda kabisa Sheikh wangu. Hii ndo dunia halisi sasa.

Motivational speakers watakwambia kila kitu kinawezekana tena kwa haraka, ila ukweli ni kuwa wanachosema si relevant kabisa. Not that easy bro..! Mie nina jamaa yangu alikuwa motivational speaker, alikuwa anawa-motivate watu ukumbini weee, akitoka hapo anapiga mzinga wa nauli. Nikawa nacheka kweli. Sasa ufanye nini? Mie sina ushauri specifically kwa biashara yako ila nitasema mambo kiujumla sana.

Kwanza jipe muda wa kutosha. Ukweli ni kuwa itakuchukuwa muda karibia miaka 10 tangu umalize chuo ili uweze kuwa stable kiuchumi. Na hapo siyo stable enough ila angalu unaweza kuona mwanga uko hapo mbele yako.

Katika hiyo plan yako ya miaka 10 jipe malengo ya muda mrefu na mfupi. Malengo ya muda mrefu inaweza kuwa mfano kumiliki kampuni flani, kisha uanze kufatilia jambo moja baada ya lingine. Tengeneza plan inayokufanya kutekeleza jambo moja baada ya lingine kwa muda flani na uweke plan yako iwe realistic kulingana na uwezo ulionao.

Katika malengo ya muda mfupi inaweza husisha jambo unaloweza kufanya for a living na kuwezesha achievement ya plan zako za muda mrefu. Sahau kabisa sijui mambo ya ujenzi wala gari wala gheto la maana kwa sasa. Stick kwenye plan yako and remain consistent. Usikate kabisa tamaa na ondoa kabisa tamaa za mafanikio ya muda wa sijui miaka miwili au mitatu.

Ukifanya hivyo, baada ya miaka 10 ndio utaona mafanikio taratibu yanakuja. Siwezi kuwa spefic zaidi kuwa ufanye nini ila kwakuwa unasema wewe ni graduate mwenye outstanding performance, basi shughulisha huo ubongo wako kung'amua jambo gani ufanye.

Usitegemee kabisa kupatiwa msaada sijui na ndugu wala nani. Hii duni kwa sasa imehama kutoka kwenye socialism mode of life kwenye kwenye capitalism. Kumbuka kwenye Capitalism kuna kitu inaitwa Individualism, hii kitu inakuwa-embaraced sana kwenye capitalism. Yaani maisha ya ubinafsi, umimi mimi. Unakuta ndugu yako ana miliki nyumba hata 5 na viwanja 10 na bado anampango wa kupanua wigo aongeze vingine, meanwhile mtu huyo ana ndugu ambao wanahitaji mtaji wa hata 100K tu na hajawahi kuwasaidia hata senti moja. Huu ndo mfumo tulionao sasa wa maisha.

Nikutakie kila la kheri. Mwisho kabisa, kwenye huo usomaji wako wa vitabu, siyo kila jambo ni relevant na maisha yetu ya kibongo. Kwahiyo fanya ku-digest vizuri kila unapokuwa unasooma. Unakuta vitabu vingi vimeandikwa na watu wa Marekani au Ulaya ambako mfumo wa maisha ni completely diffrent na tulionao bongo. Vingi vina mambo mazuri, ila kuwa makini usiige kila jambo. Mafano unakuta unaambiwa kwa kila sh 100 unayopata hakikisha unaweka 50 kama akiba na 30 uwekeze na 20 ufanye kama matumizi. Sasa kwetu huku vipato ni vidogo sana kiasi cha hata hiyo pesa unayopata haiwezi hata kulipia kodi ya nyumba na kununua chakula. Je hiyo saving unaitoa wapi? Ila Ulaya na Marekani hayo mambo yanawezekana maana wao malipo anayopata mtu yanawezesha kutoa gharama za kuishi na kubakisha savings.

Aluta continua...
 
Fuata moyo wako na usimsikilize mtu yeyote.

Tafuta na hivi vitabu usome

1.Change your thinking change your life by Brian Tracy

2.Millionaire nextdoor

3. Secrets mind of millionaire by T harv Eker
 
Ahsante sana mkuu nimekuelewa vizuri sana.
Kwahiyo hapa njiandae for a decade, Sawa
 
Back
Top Bottom