Elimu ya chuo kikuu ni muhimu lakini karama ya kuzalisha pesa ni muhimu zaidi.
Average age ya kuhitimu ama kumaliza digrii ya kwanza Tanzania ni miaka 24. Vijana wengi waliohitimu chuo wana msongo mkubwa wa mawazo sababu ajira hakuna. Na pia elimu imewaweka daraja la juu hawawezi kufanya kazi za chini.
mentality ya wahitimu wa vyuo vikuu huwa wanaaminishwa wao ni special , ndio magenious wana deserve kazi za juu.
vijana wenye elimu ndogo walishakubaliana na hali, they know wasipo hustle hawafiki mahali, so wame build in mind kukubaliana na hali, na ku fight. They simply have no ego. Wasomi in the other side they have ego
Mfano hai kijana Misso Misondo ana miaka 24 na amenunua gari yake ya kwanza.
Mfano wa pili binti Nice Moshi konda maarufu Tilisho ana miaka 24 amenunua gari yake ya kwanza.
Sometimes ujivuni ya kusoma chuoni ni mzigo, vijana wengi wanaohitimu vyuo wanachelewa sana kustuka kwamba tunaishi mara moja tu na miaka hairudi
Kijana kamaliza degree yake akiwa na 24, mindset yake imekuwa tuned kujiona yeye ni special keki kwamba inabidi asubiri kazi za ofisini zenye ulaji mnono, ujinga huu huwa wanajazana sana vyuoni.
kijana anamaliza chuo yupo kitaa anazungusha barua kwa kutafsiri msemo "one day yes" ndivyo sivyo kudhani kuna njia moja tu ya kutoboa, muda unaenda akiwa anazurura mtaani, anaweza kupata kazi ya fani yake ila akaishia kujitolea bila mshahara kwa muda mrefu.
Miaka inaenda haraka mnooo anagonga 30, kidogo anaanza kujitambua anafungua duka la kawaida kwa kuwa anona kazi ya kuchoma mishkaki, kuchoma mahindi, kuuza nyanya, kuwa mama ntilie, kuwa kinyozi, SIO HADHI YAKE YA MHITIMU, hapo dukani unakuta anafanya biashara aliyoiga ili kumaintain satus yake ya kuwa mhitimu, na kwa vile bado ana mindset ya kichuo na kutaka kuendana na wenzake wachache walioajiriwa sehemu zenye ulaji, anajikuta anatumia mpaka mtaji ku keep up.
Ubao unasoma 35 III !!! ndio anakuja justuka kwamba yupo tayari kufanya chochote halali bila kujali hadhi yake wala atavyosemwa, hapo ndo unakuta mtu anaanza kujua kwamba hata kazi alizozidharau zinaweza kumtunza, anajilaumu kwamba alichelewa sana.
Wakati huo wale wa darasa la saba na form 4 walishastuka zamani sana