Vijana Wasomi wakimbilia fursa mlima Kilimanjaro

Jun 20, 2023
54
51
Kama unadhani vijana wanaojihusisha na kazi ya kubeba mizigo ya watalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimajnjaro(KINAPA) maarufu kwa jina la 'wagumu' ni vijana wasijiotambua na ambao hawajaenda shule,pole yako.

Sasa unaambiwa miongoni mwa wanaobeba mizigo ya watalii ni wasomi wa vyuo vikuu nchini waliohitimu katika kada mbali mbali na wengine wangali wakiendelea na masomo yao na kazi wanayoifanya ni katika kutafuta fedha kwa ajili ya kulipia ada na mahitaji mengine muhimu .

Miongoni mwao wapo kwenye kampuni ya Altezaa Travel,hii ni kampuni ya kijamii ambayo imewasajili vijana zaidi ya 1,500 kwa ajili ya kazi hiyo ya kubeba mizigo ya watalii ikiwamo vyakula,majiko ya gesi ya kupikia chakula,mitungi ya Oksijeni kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza pale mgeni anapokutana na changamoto ya kiafya kule mlimani.

Dickson Mugisha meneja wa Altezza Travel anasema wasomi hao wamo waliomaliza vtuo na wako kwenye ajira wakiwamo madereva lakini wapo wanaoendelea na masomo lakini kutokana na hali ya kiuchumi wasomi hawa wakaamua kuchapa kazi ili kusaka fedha za kulipia masomo yao.

"Suala la haki za porters ni suala ambalo unatakiwa kulijadili kwa mapana saana maana humo wapo porters wa kada mbali mbali,na sisi kama Altezza tunao porters ambao wako kwenye masomo vyuo vikuu na kuna wakati anakuambia kaka nisaidie nimalizie ada yangu"

"Altezza ni kampuni ya kijamii lazima tuwekeze kwenye jamii na porters ni familia yetu lazima tuwekeze kwao na hili sisi tumeliwekea mkazo ,tunalipa mishara yao kwa wakati kwa mujibu wa GN 22 ya mwaka 2008 ambayo ni dola kumi kwa siku na si hivyo tu tunawalipia hadi matibabu"

Mavazi ya kujikinga na baridi kali mlimani ni moja ya changamoto kubwa ambayo imekuwa ikiwakabili wagumu hawa licha ya kufanya kazi ngumu wakibeba mizigo yenye ujazo wakilo 20 na hii ni kutokana na makampuni mengi kutowekeza kwa vijana hawa kwa maana ya kuwapatia mahitaji kama hayo.

Mugisha anasema suala hilo ni moja ya mambo wanayopewa kipaumbele na kampuni yao na hufanya ukaguzi siku moja kabla yakuponda mlima lengo ni kuhakikisha kila porters anayo mavazi stahiki kwa ajili ya kupandia mlima.

Anasema mgumu akipata changamoto za kiafya kutokana na kutokuwa na mavazi stahiki anayepata hasara ni wao kutokana nakuingia gharama za kumtibu hivyo ni lazima wawatunze ili kuepuka gharama kubwa za kuwahudumia pindi wanakutana na changamoto za kiafya huko mlimani.

"Wengi hawajui tu ila kiukweli Porters ndiyo wasaidizi wa wageni,hawa ndiyo wanobeba vitu vyote vya mgeni kuanzia vyakula,gesi ya kupikia,Okisijeni na vitu vingine,sasa lazima huyo mtu umtunze na usipomtunza maana yake ujiandae kuingia gharama za kumtibu na hapa anayepata hasara ni kampuni"

Anasema kwa mazingira ya sasa wanahitajika porters wasomi wataoweza kuwahudumia vyema wageni pale wanapokutana na changamoto za kiafya wawapo mlimani hasa pale mgeni anapohitaji hewa ya okisijeni ni lazima porters wawe na elimu juu ya matumizi sahihi ya mitungi ya okisijeni

Kwa sasa Altezza imeanzisha programu maalumu ya kuwapeleka waongoza wageni(Guides) nje ya nchi kwenye milima kama Nepal kwa lengo la kujifunza zaidi na kupata uzoefu wa namna Guides wenzao wanaovyofanya kazi.

Kwa mujibu wa Mugisha Programu hiyo ilianza Novemba mwaka jana ambako kundi ya Guides wapatao 13 walienda ziara ya mafunzo huko Nepal ambako walijifunza mambo kadhaa pamoja na kubadilisha mazingira wakiongozana na mpanda milima nguli duniani Nims Dai.

Ukitaka kujua mengi zaidi juu ya Altezza wafuate kwenye web yao www.altezza.travel

WAGUMU 1.jpg
WAGUMU 2.jpg
 
Taratiiibu naona wasomi wanaanza kutokuchagua kazi , pigeni kazi ndugu zangu tulienda kusoma ili tupate ujuzi wa kutatua matatizo yetu!!!
 
Shida ya Pale ni Udulumaji unakuta Mzungu anatoa $1000 ya wabeba mizigo mpaka iwafikie unakuta mtu anapewa $35
 
Shida ya Pale ni Udulumaji unakuta Mzungu anatoa $1000 ya wabeba mizigo mpaka iwafikie unakuta mtu anapewa $35

Daktari au mwalimu anayefundisha serikali kwa siku anazalisha kiasi gani na analipwa bei gani?

Ukitaka usidhulumiwe jiajiri au anzisha biashara yako.
Kwenye hiyo Usd 1k walipe lipa USD 500 kwa wafanyakazi ili usitende dhulma
 
Back
Top Bottom