Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,101
- 2,344
Kabla sijasema lolote kila mmoja asome huu ujumbe wa mstaafu mmoja wa jeshi la polisi akigugumilia maumivu ya kikokotoo alioutuma kwa aliyekuwa mbunge mstaafu wa Jimbo la Tarime vijijini (CHADEMA) ndugu John Heche na kuuposti Instagram page yake...
Mimi umeniumiza sana na nimeamua kuuleta kwenye jukwaa hili ili tujadili.
✍️Ujumbe huu uko very clear kuwa unahusu kikokotoo cha 33.33% cha mafao ya watumishi umma wastaafu..
✍️Ni wazi pia kuwa kikokotoo hiki, hakiwahusu watumishi wa kada za kisiasa kama;
√ Rais wa nchi.
√ Makamu wa Rais.
√ Waziri Mkuu.
√ Spika wa bunge.
√ Jaji Mkuu
√ Mawaziri.
√ Makatibu wakuu wa wizara..
√ Wabunge nk nk.
✍️Lakini ni ajabu kuwa hili kundi la watu (wanasiasa) hao hapo ☝️☝️juu ndio wanajipangia wajilipe mafao kiasi gani na kwa kanuni ipi. Na pia ndio wanaowapangia wengine kama walimu, makaktari, manesi, makarani nk nk walipwe vipi na kwa kanuni ipi.
Mpaka hapo, unaweza kuona kuwa, kwa utaratibu na mfumo huu, basi kamwe hakuwezi kuwa na fairness yoyote ktk kugawana keki hii ya taifa!!
✍️Hebu sasa tumjadili huyo polisi hapo juu. Kafanya kazi kuitumikia nchi hii kwa miaka 32. Hivi kweli ni sahihi kumpa mafao ya kustaafu ya Tshs. 18,000,000 tu? Hivi huyu hata mshahara wake unaweza kuwa ulikuwa shilingi ngapi eti?
✍️Hebu endelea kufikiri zaidi. Kuwa, usawa uko wapi iwapo mtu mmoja mwanasiasa mwenye cheo cha ubunge tu. Tena aliyepata ubunge huo kwa rushwa au kuiba kura.
Huyu anakaa bungeni miaka mitano halafu siku hiyo hiyo bunge linapovunjwa bila jacho wala kuhangaishwa kuambiwa leta nyaraka hii au ile ili ulipwe mafao lakini jioni anakuta kwenye Bank A/C yake TZS 350,000,000 kama mafao yake ya ubunge kwa miaka 5 tu???
Hivi hii inaingia akilini kweli hii?
✍️Hebu Rais Samia Suluhu Hassan na serikali kwa ujumla na hususani CCM yako oneni hata aibu kidogo basi. Wote tuna akili na tunaona. Hii haiko sawa!!
Hii siyo sera nzuri hata kidogo. Ni sera iliyoleta utaratibu wa kikandamizaji na kinyonyaji usiokubalika hata kidogo ktk jamii iliyostaarabika...
Hebu rudisheni kikokotoo cha zamani japo hata hicho nacho kilikuwa hakifai vilevile..