Vijana hamna pesa, ubunge ni wa matajiri wafanyabiashara na wabunge wastaafu wenye mafao yao

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,278
2,041
Kipenga cha UCHAGUZI MKUU kitakuwa kimepulizwa kimya kimya dalili za kuchukuliana FOMU tumeziona.

TAHADHALI kwa VIJANA wataka UBUNGE
Kuna aina 2 za wataka Ubunge ambao watawatesa Vijana Wasomi wasio na PESA
1.Wabunge wanaomaliza Muda wao Wenye Mamilioni ya Mafao
2.Wafanyabiashara Wenye Pesa na Mikopo ya Benki.

Haya Makundi Mawili ni Mwiba mkali kwa Vijana Wasomi Masikini. Wapiga kura wetu ni Masikini kiasi ambacho UMASIKINI wao Unanunulika na WABUNGE wastaafu na Wafanyabiashara.

Hitimisho kwa VIJANA Wasomi wataka Ubunge kwa kuwa hamna PESA achaneni na Mawazo ya Ubunge jikiteni kwenye KILIMO cha Jembe la Mkono, Bodaboda, Kubet na Umachinga UBUNGE waachie Wabunge wastaafu Matajiri na Wafanyabiashara ili Wakiipata WAZINUFAISHE Familia zao.

CCM hii sio ya WAKULIMA na Wafanya kazi bali ni Wafanyabiashara na Matajiri.
 
Back
Top Bottom