Kuelekea Mei Mosi 2022: Rais Samia, Waokoe Watumishi wako Dhidi ya Dhulma Kali ya Makato ya Lazima ya Mshahara kutoka kwa Vyama vya Wafanyakazi

Wanachama wa vyama husika nao hawajui wajibu wao! Ni wale wale walalamishi wa pembeni!
 
Hili jambo tumelipigia sana kelele huko nyuma, lakini utekelezaji wake 0! Yaani mpaka leo huwa sipati majibu ya sababu hasa za kuwakata wafanyakazi 2% ya basic salary kila mwezi kwa ajili eti ya ada ya uanachama!

Huu ni wizi wa wazi kabisa kwa sababu mishahara ya hao wanachama hutofautiana, huku madai yao/ haki zao kwa mwajiri yakifanana/zikifanana.
Ifikie wakati serikali ya ccm iachane na hii tabia ya kulea mafisadi/majambazi kwenye jamii, wakiwemo hawa viongozi wa vyama vya wafanyakazi.

Waziri mwenye dhamana apeleke muswada bungeni. Hii sheria kandamizi ibadilishwe, na hivyo wafanyakazi wote walipe kiwango sawa cha ada kila mwezi! Badala ya huu utaratibu wa kifisadi wa kulipishana kwa % ya mshahara, halafu unakuta hela zenyewe zinatumika kulipana tu posho na kuendeshea vikao vya kipuuzi puuzi tu.
 
Muhimu Ni kuendelea kupiga kelele zaidi zaidi kwasababu bila hivyo hali itakuwa mbaya zaidi.
 
Namaanisha kuwa wanachama dhaifu huzaa mifumo dhaifu inayoleta viongozi miungu watu!
Vyama ni vya kwao. So inategewa wao ndo wawe mstari wa mbele kufanya maamuzi magumu.
Wawe very #disruptive waache kuishi kwa mazoea!
Sidhani kama unajua unachozungumza.

Anyway, Hapa nazungumzia Makato ya Lazima ya Mshahara yanayofanywa na Vyama vya wafanyakazi Tanzania hasa kwa Watumishi wasio wanachama wao.

Haya makato yanaiywa Ada ya UWAKALA na yanafanywa kwasababu za kisheria ( Sheria ya ajira na mahusiano kazini ( 2004).

Kwahiyo, hapa utaona Sheria ilitungwa na Bunge na anayepitisha Makato haya kwa mtumishi Ni Mwajiri.

Na ndio maana hapa mwenye uwezo na nguvu ya kutatua suala hili "Once and For All" Ni Mwajiri mwenyewe.
 
Mjinga mwache aendelee kufanyiwa ujinga.
Mimi huu ni mwaka wa saba sijawahi kukatwa na hivyo vyama vya kijinga.
Nililetewa form ya TUGHE nikaitupa kidizaini.
Hii mifuko haimkati mtu kwa lazima.
Huo ndio ukweli, sema unapoanza kazi wanakuja wapumbavu kuwapigia promo nyingi ndipo mnaingia kingi. Kutoka pia mnatishwa.
Walimu mpaka mifuko ya hifadhi ya jamii walikuwa wanachaguliwa na mabwenyenye waliolamba 10%.
 
Hataweza kuongeza mishahara kama alivyoahidi maana hazina inavuja atakuja na sababu zingine mtabaki macho wazi
Uchumi unapanda kwenye majukwaa ya siasa ila likija suala la maslahi ya walioupandisha huo uchumi(Wafanyakazi/watumishi utaambiwa subirini uchumi ukue.
Wenye akili hung'amua fumbo mapema na mchezo ndiyo huo huo kila bajeti/mwaka.
Watanzania tumekuwa wepesi mno.Haki hakuna kote kote,wakulima,wafugaji,wavuvi,wakwezi,watumishi,wajasiriamali nk wote wanaisoma namba na hakuna nafuu isipokuwa wanasiasa na wateule wao.
 
Safi sana... MoseKing umeona? Kumbe matendo yanawezekana. Chukueni hatua stahiki. Acheni visingizio au kuhamishia matatizo yenu kwenye mamlaka nyingine!
Mnanyonywa!
 
Naunga mkono hoja makato yawe fla
Naunga mkono hoja makato yawe flatrate kwa sababu makato kwa asilimia ni uonevu kwani hakuna huduma ya ziada anayoipata anayekatwa fedha nyingi ukilinganisha na yule anayekatwa kdgo
 
Kama hukatwi basi shukuru Mungu, na kaa ukijua kuwa lazima watakuja kukukata tu whether wewe Ni Mwanachama au siyo Mwanachama.

Na hapa nazungumzia zaidi kuhusu Makato ya Lazima ya Ada ya UWAKALA na siyo Makato ya uanachama.

Mwanachama hawezi kulalamika kwasababu Makato yanakuwa Ni kwa hiari yake mwenyewe.
 
Kama hukatwi basi shukuru Mungu, na kaa ukijua kuwa lazima watakuja kukukata tu whether wewe Ni Mwanachama au siyo Mwanachama as long as Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini itaendelea kuwa kama ilivyo sasa hivi.

Na hapa nazungumzia zaidi kuhusu Makato ya Lazima ya Ada ya UWAKALA na siyo Makato ya uanachama.

Mwanachama hawezi kulalamika kwasababu Makato yanakuwa Ni kwa hiari yake mwenyewe.
 
Kujiunga na chama cha wafanyakazi ni HIYARI kwaio unaweza kujitoa.

Mi nliunganishwa TUGE nikakatwa miezi4 nikaandika barua ya kujitoa na nikatolewa.

Vyama vya wafanyakazi havina msaada kwa wafanyakazi tangu enzi za JPM ila huko nyuma enzi za JK vilikuwa msaada sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…