Kuna mambo ambayo yanahusu CDM kama chama na mambo ambayo CDM itakuja kufanya ikishika madaraka kwa taifa. Changamoto zinazoulizwa hapa siyo changamoto za baada ya kushika utawala. Ni changamoto za jinsi ya kujiandaa kuelekea kushinda mwaka 2015. Kwamba ili iweze kushinda yawezekana kuna vikwazo ambavyo vitafanya CDM isishinde kirahisi (vinaweza kuwa vya ndani au nje ya chama). Hizi ndizo changamoto.
Unafikiri ni vitu ambavyo viko ndani ya CDM au kuhusiana na CDM ambavyo vinaweza kuwa vizuizi vya kuweza kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa na ule wa Rais na wabunge?
Kuhusu vizuizi vya ndani,kikubwa(ambacho kina indirect correlation na maadui wa nje),ni hilo suala la udini na pengine ukanda(hili halina nguvu).
La udini linapokuwa exploited na kiongozi wa ndani,ni tatizo kubwa sana.Ni tatizo kwasababu utakuta kiongozi huyo badala ya kujaribu kuzifuta hisia hizo kwa wananchi,basi anazitumia kwa manufaa yake binafsi kwasababu tu ya kupata nafasi ya kugombea urais.
Kwa mfano kumekuwa na almost in a simultaneous kind of fashion,kuona kiongozi akicapitalize kwenye issue ya udini kwa maneno ambayo yana mwelekeo wa kuwaaminisha wananchi kuwa ni kweli kuna udini.Na hilo linatokea sambamba na wakati ambao kuna shughuli ambayo ni muhimu kwa chama kujijenga.(mfano uchaguzi,m4c nk)
Hapo tatizo ni kubwa kabisa kwa uongozi kwasababu sioni kama kuna jitihada makini na za makusudi kabisa za kujaribu kulidhibiti hilo.
Viongozi wenye dini ambazo inasemekana haipewi nafasi kwenye chama,ndiyo hao ambao walitakiwa wawe msitari wa mbele kukanisha taarifa ama hisia hizo,yani wawe kama mabalozi wa kupingana na hilo kwa nguvu zote(kama ni kweli wanaamini hakuna udini).Lakini imekuwa tofauti.
Hilo linanipa mashaka sana given the fact kwamba uongozi kwa ujumla hawaonyeshi dhamira ya kupambana na hali hiyo.
Kukiwa na umoja ndani ya chama (uongozi),basi ni rahisi kujipanga(badala ya kulumbana kugombea madaraka),na kujikita zaidi kupeleka ujumbe kwa wananchi wengi kwa kadri ya uwezo wao.(especially vijijini)
Kwa upande wa mambo ambayo ni nje ya chadema,kubwa ni la serikali ya ccm kutumia dola kudhibiti ukuaji wa chama hicho.Tumeona wanavyotumia polisi,usalama wa Taifa pamoja na makundi kama green guard,na wakati mwingine kutumia makundi ya dini ili kuleta mvurugano.
Yote hayo ni kujaribu kuidhibiti demokrasia na kuwanyima wananchi kuitumia haki yao ya kuwachagua viongozi na vyama wanavyovipenda ama wanavyoviona kuwa vitawaletea mabadiliko kwenye maisha yao.
Ninaamini hata kama chadema watakuwa na sera na itikadi nzuri kiasi gani,kama hawapewi nafasi na uhuru wa kuwafikia wananchi ili kuwaelewesha kuhusu mipango yao kwa Taifa,basi haijalishi,kwasababu kitakachokuwa kikizungumziwa ni hayo ya unyanyasaji na umwagaji damu,chama tawala kikijaribu kuitumia nafasi hiyo kuwa pakazia chadema kuwa ni chama cha fujo,pia hilo linaondoa ile focus.(mfano toka yale mauwaji ya Iringa na Morogoro,ni kama m4c imeyumba)
Na ukishawaingizia wananchi hofu,basi kwa namna moja ama nyingine,utakuwa umepunguza kasi ya wananchi hao kujitokeza kukiunga mkono chadema.
Sasa sijui hilo litakuwa fixed kwa kutumia katiba mpya ama ni kitu gani?
Kwasababu ndiyo maana niliamini kuwa kupigania katiba mpya ndilo jambo la kwanza na la msingi kabisa.Inavyoonekana,ni kama vile tuko chini ya utawala wa chama kimoja.