Kuelekea 2015: Changamoto Kuu za CHADEMA ni nini?

Nooo haijalala kihivyo mkuu wangu!unarahisisha mno!!kama unategemea chama pinzani kukamata dola kirahisi hivyo utakuwa unakosea sana,japo hairidhishi sana lakini tukubali tu kuwa chadema inakimbia!japo spidi yake bado ni ndogo kuliko tulivyotegemea au kutaka ila lazima mbio tuziite mbio!!haina maana timu iliyoshinda kwa goli moja tuiite kuwa imelala,kwa kuwa tu tulitaka ishinde kwa goli nyingi zaidi,kingine ni kuelewa nafasi ya kila mwanachama,mpenzi,na kila mpenda mabadiliko kuchukua hatua stahili pale alipo au anapoweza kufikia,haina maana kuwa mwanachama huku unasubiria kiongozi wa chama kilekile aje kukubembeleza kukipigia kura chako!!badala ya wewe kuwaelimisha/kuwashawishi/na hata kuwaomba wale wa mrengo tofauti na wako wakuunge mkono kukiunga chama chako mkono!! Ila pia kweli kuna sehemu ambazo nguvu inahitajika zaidi,bahati mbaya sana si sehemu moja au mbili,bali sehemu nyingi tofauti,ambazo bado itakuwa ngumu kwa Dr slaa,Mbowe,Tlissu na wengine wachache wenye ushawishi mkubwa kupafikia na kuweza kutoa special assistance huko,kwa muda upi?kwa uwezo upi?kwa uchumi upi?hapo ndipo panapohitaji subira na umakini wa hali ya juu!!kuna sehemu ambazo chama kinaweza kushinda uchaguzi bila hata ya kutumia nguvu nyingi,ila inahitajika subira na umakini mkubwa kuzijenga sehemu kama hizo ambazo mwisho huitwa ngome ya chama fulani,kama lema aliweza kuwashawishi watu elfu,wewe hushindwi kuwapata watu kumi,anza sasa!!ingia kwenye mbio ili uweze kukosoa kile unachojua ugumu wake,badala ya kujaribu kuufyeka msitu huku ukiwa nyuma ya keyboard,ukinyanyua kichwa ndiyo unagundua kumbe ulikuwa unacheza game,kisha unadai umedhulumiwa heka kumi za msitu ulioufyeka kwenye computer yako,shtuka.
Watu wa vijijini hawamuhitaj Mbowe,Slaa ama Zitto wanahitaj kuiona CDM kama taasisi na uongoz wa mashinani ambao watakua karibu nao na wanaokaa nao maeneo yao ni udhaifu wa hali ya juu kuwategemea viongoz wa kitaifa kufanya kitu ambacho kingetakiwa kifanywe na Uongoz wa mkoa.
 
Kwa matokeo ya chaguzi ndogo zilizofanyika jana inadhihirisha wazi kabisa CDM tuna safari ndefu na ngumu kuelekea uchaguz wa 2015 kama kweli tumedhamiria kuchukua dola.

Kumekuwepo na hoja nyingi dhaifu juu ya kwa nini CDM wameshindwa angalao kupata nusu ya viti vya udiwani ambavyo vilikua wazi.Wanajaribu kutoa lawama kwa tume ya uchaguzi juu ya uandikishaji wa wapiga kura wapya hii ni dhaifu sana kwa sababu kama sababu ni hii huko tuliposhinda walijiandikisha?

Wakat mwingine ni bora kukiri udhaifu wa uongoz wa CDM juu ya mahusiano yao na viongozi wa mikoani mpaka mashinani.Imedhihirika wazi viongozi wa makao makuu wana mkanganyiko wa kiutendaji na uongozi wa chini hamna mrejesho kuhusiana na shughul za CDM kila siku je wanawajibika kwa wanachama je wanafanya kazi za chama ama wanawasubiri viongoz wa kitaifa ndio waende nao kwa wanachama.

Mabaraza ya chama yamelala usingizi au ni kama hayapo mfano. BAWACHA hata haijulikan na kwanini wameshindwa kuwashawishi wanawake kujiunga na CDM au tatizo ni uongozi kung'ang'ania mfumo dume.

Ukiangalia wengi walioichagu CCM jana ni wanawake ambao ndio wapiga kura wengi na wana mwitikio na hamasa ya kipekee ya kisiasa.

Ni aibu kwa matokeo ya jana tuache unafiki CCM IMECHOKWA LAKINI CDM IMELALA.

Naomba utoe mapendekezo specific sasa, nini kifanyike? Je, wewe unafanya nini katika eneo lako?
 
CDM haishindi kwa sababu watanzania (hasa wasomi) ni waoga. CDM ina wapiga kura wengi lakini haina wapigiwa kura. Ikifika wakati wa uchaguzi, ukiangalia wanaojitokeza kuchukua fomu za kugombea na CDM ni aibu... Wasomi (ambao naamini wengi wa viongozi wazuri ndimo walimo) mko wapi???...
 
Jana kwenye uchaguzi wa daraja mbili asilimia zaidi ya 75% walikuwa akina mama. vijana waliopiga kura hawafiki hata 10%, lakini ushindi ulienda chadema.
Kwa taarifa zilizopo tume ya uchaguzi wanatarajia ku update daftari la kupiga kura mwakani, ambapo asilimia kubwa ya vijana ambao ndio chachu ya mabadiliko na mtaji wa chadema watajiandikisha kupiga kura.

Safari ya CHADEMA kushinda 2015 ni laini kama maini
 
Wilbroad Slaa – Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi

WAHENGA waliamini kuwa tabia na hulka ya binadamu haibadiliki hata akiwa na umri mkubwa kiasi gani. Chukulia mfano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Wilbroad Slaa. Huyu kwa umri wake, kwa asili yake ya kupitia mifumo ya dini ya Kikristo madhehebu ya Kikatoliki, asingekuwa mtu wa kutunga, kusema na kuwaaminisha watu ukweli. Huyo ni mtu ambaye alikuwa padre, kiongozi mkubwa wa kiroho. Usingemtegemea kabisa kutunga na kuwaambia watu uongo. Kwa hakika, tabia yake hiiya kutunga na kusema uongo inazua maswali kuhusu mfumo mzima wa kulea watoto katika Seminari na kufundisha mapadre katika Kanisa hili.

Mtu kama Slaa – mzushi, mwongo, mnafiki asiyeheshimu watu anaweza vipi kufikia hatua ya kuwa padre; baya zaidi aliweza vipi kupanda ndani ya mfumo huo hadi kufikia kuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC). Nasema haheshimu watu kwa sababu mtu anayetaka watu wamchangue awaongoze, hawezi tena kushiriki katika tabia ya kuwadanganya na kuwafanya wapumbavu. Lakini Bwana Salaa hili halimnyimi usingizi. Majuzi, Ijumaa, kule Sikonge, Tabora amezua na kutunga jipya. Amedai kuwa Julai 2, mwaka huu, 2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alisafiri kwenda Hong Kong kumwokoa mtoto wake wa kiume, Ridhiwani Kikwete ambaye anadaiwa kuwa alikuwa amekamatwa na mihadarati siku moja kabla, yaani Julai Mosi.

Huu ni uongo wa dhahiri kwa sababu ratiba ya Mhe. Rais Kikwete katika siku hizo anazozitaja Slaa iko wazi.
Julai Mosi, akitumia Ndege ya Rais, alisafiri kwenda Rwanda ambako alihudhuria Sherehe za Miaka 50 ya nchi hiyo na akalala mjini Kigali. Julai 2 alisafiri kwenda Bujumbura kuhudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Burundi. Alirejea Dar es Salaam Julai 3 na Julai 4 alikutana na ujumbe wa Kampuni ya IBM na Mjumbe Maalum kutoka Zimbabwe. Julai 5, alikwenda Dodoma ambako aliendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri na kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo. Sasa alikwenda Hong Kong lini? Ama alikuwa Burundi na Hong Kong siku hiyo hiyo? Slaa anadai pia kuwa alipowasili Hong Kong, Mheshimiwa Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Philip Marmo ambaye alimpeleka kwenye mkutano na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hu Jintao. Huu ni uongo mwingine wa dhahiri na ambayo sijui unamsaidia nini Slaa. Slaa anasema uongo kuhusu Balozi Marmo kwa sababu ratiba ya Mheshimiwa Marmo kwa siku sita za mwezi Julai nayo iko wazi na siyo kificho.

Kwanza, Ubalozi wa Tanzania katika China hauko Hong Kong bali uko mjini Beijing na Mheshimiwa Marmo hajawahi hata kufika Hong Kong. Taarifa kutoka Hong Kong amekuwa anazipata kutoka kwa Balozi Mdogo wa heshima wa Tanzania Mheshimiwa Clement Chan. Hata juzi, Ijumaa, Oktoba 26, Balozi Marmo alikutana na Bwana Clement Chan. Balozi Marmo anapanga kutembelea Hong Kong kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi ujao, Novemba, 2012. Angalia ratiba ya Mheshimiwa Marmo katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu:
Julai Mosi, Balozi Mamro alikuwa ofisini Beijing. Julai 2, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Mongolia mchana na usiku alihudhuria Sherehe za Siku ya Djibouti kwenye Hoteli ya Lengedane mjini Beijing. Siku nzima ya Julai 3 alishiriki katika warsha ya Kampuni ya China Chemicals Techonologies Group ambayo inataka kufungua viwanda cha madawa na mbolea nchini Tanzania. Asubuhi ya Julai 4, Balozi Marmo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Sichaun Honda Group inayowekeza katika miradi ya Mchuchuma na Liganga na jioni ya siku hiyo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Mawasiliano ya ZTE. Julai 5, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Venezuala Day na Julai 6 alijiunga na Mabalozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Forum on Trade na Cooperation na jioni alihudhuria Sherehe za Rwanda Day. Sasa, Balozi Marmo alikwenda lini Hong Kong kumpokea Mheshimiwa Rais kama siyo uongo?

Katika siku zinazotajwa, Bwana Ridhiwan alikuwa Dar es salaam muda wote. Kwa hakika, Ridhiwan hajapata kufika Hong Kong ama China katika maisha yake yote. Nchi pekee inayokaribia China ambayo amewahi kuitembelea ni Dubai kwa sababu hata India hajapata kufika. Ratiba hizi za Mhe. Rais na Mheshimiwa Marmo na ukweli kuwa Ridhiwan hajapata hata kufika China ama Hong Kong ni ushahidi usiopingika kuwa Mzee Slaa kwa mara nyingine ametunga, yeye amekuwa bingwa wa goofing. Huyu ni mtu anayezeeka vibaya. Tunaamini kuwa ameanza kuchanganyikiwa pengine kwa kuzidiwa na jukumu ya kulea mtoto-mjukuu na kumtunza mchumba Bi Josephine ambaye wanaishi kama vimanda kwa sababu huyo mama bado anayo ndoa halali. Pole sana Mzee Slaa kama Josephine na mwanae amekushinda mrudishie mwenye mali yake.
 
Watu wa vijijini hawamuhitaj Mbowe,Slaa ama Zitto wanahitaj kuiona CDM kama taasisi na uongoz wa mashinani ambao watakua karibu nao na wanaokaa nao maeneo yao ni udhaifu wa hali ya juu kuwategemea viongoz wa kitaifa kufanya kitu ambacho kingetakiwa kifanywe na Uongoz wa mkoa.
Wanakuhitaji wewe na mimi na ukweli uliobeba haki,ustawi,na vigezo vinavyoitofautisha chadema na ccm,tlp,cuf,nccr nk,umenielewa.
 
Wewe ni msemaj wa ikulu ama nani?ili 2kujibk vizur ama ni hekaya za abunwasi
 
Kwa matokeo ya chaguzi ndogo zilizofanyika jana inadhihirisha wazi kabisa CDM tuna safari ndefu na ngumu kuelekea uchaguz wa 2015 kama kweli tumedhamiria kuchukua dola.

Kumekuwepo na hoja nyingi dhaifu juu ya kwa nini CDM wameshindwa angalao kupata nusu ya viti vya udiwani ambavyo vilikua wazi.Wanajaribu kutoa lawama kwa tume ya uchaguzi juu ya uandikishaji wa wapiga kura wapya hii ni dhaifu sana kwa sababu kama sababu ni hii huko tuliposhinda walijiandikisha?

Wakat mwingine ni bora kukiri udhaifu wa uongoz wa CDM juu ya mahusiano yao na viongozi wa mikoani mpaka mashinani.Imedhihirika wazi viongozi wa makao makuu wana mkanganyiko wa kiutendaji na uongozi wa chini hamna mrejesho kuhusiana na shughul za CDM kila siku je wanawajibika kwa wanachama je wanafanya kazi za chama ama wanawasubiri viongoz wa kitaifa ndio waende nao kwa wanachama.

Mabaraza ya chama yamelala usingizi au ni kama hayapo mfano. BAWACHA hata haijulikan na kwanini wameshindwa kuwashawishi wanawake kujiunga na CDM au tatizo ni uongozi kung'ang'ania mfumo dume.

Ukiangalia wengi walioichagu CCM jana ni wanawake ambao ndio wapiga kura wengi na wana mwitikio na hamasa ya kipekee ya kisiasa.

Ni aibu kwa matokeo ya jana tuache unafiki CCM IMECHOKWA LAKINI CDM IMELALA.

Hakuna kitu kingine zaidi ya hiki chadema wapunguze gharama za maandamani na mikutano ya hadhara na hivyo wawakumbuke viogozi wa mikoa, wilaya na matawi kupata posho tokana naruzuku na ndio hao watakaoandaa wapiga kura.
 
Chadmea hawan tofauti na Obama. Kuremba kwiiiiingi kumbe kichwani hamna kitu.
 
Chadema wanadhani harakati .za chama kukamat dola ni maandamano na wengi hawataki chama chao kikosolewe au kiongozi wao yeyote aguswe na wengi hata vijijini wanategemea sana mtandao wa viongozi wa juu tofauti na ccm ambayo imejiimarisha kila ngazi tuko hapa 2015 wengi watakuja kulia hapa,wanataka kuuaminisha umma kuwa wote watanzania wameichoka ccm jumbo ambalo si kweli nguvu kubwa walotumia hiendani na matokeo hata Dr slaa jana Igunga aliwahakikishia wananchi kuwa anataarifa wanaongoza kata karibu zote huku akijua .ni uongo kila siku mtaendelea kulia kwa kuwa mnafanya propaganda zaidi ya hali halisi
 
Sikatai kuandikisha wapiga kura wapya ila ni sababu dhaifu sana....

Hii sababu ingekuwa dhaifu serikali kupitia tume yao wangesha andikisha lakini hii ni very key kwa ushindi wa ccm hamtaona wakiandisha wapiga kura wapi siku za karibuni, trust me!
 
Habari zenu wapenda mabadiliko wote humu JF. Napenda kutoa hoja hii ya kiukombozi kuhakikisha 2015 nchi hii isiwe mikononi mwa Wadhalimu CCM tena. Kabla sijatoa maoni yangu ya nini lifanyike. Niweke kwanza siraha wanazotumia CCM ili kuhakikisha wanaendelea kubaki madarakani.

Naomba ifahamike kuwa CCM imekuwa ikitumia njia nyingi kuhakikisha inabaki madarakani. Nikianzia 1995 CCM wamekuwa wakijenga hofu kwa wananchi kuwa wakichagua upinzani amani na utulivu unatoweka huku wakijitapa wao ndo waanzilishi wa amani, kwa mbinu hizo wanachi waliwaamini wakaiweka madarakani. 2000 wakaongeza udini dhidi ya CUF bila kusahau siraha yao inayowafanya waamine kwa wananchi. 2005 wakaja na msemo mpya wa ari, nguvu na kasi mpya. Huku wakimalizia na uleule msumari wa moto kwa wapinzani Amani na utulivu. 2010 tena wakaongeza siraha mpya, wakaleta "Udini Ukabila na ukanda dhidi ya CHADEMA" bila kusahau siraha yao ya siku zote Amani na Utulivu. Inaonekana Amani na utulivu ndiyo silaha wanayoitegemea CCM kuzidi kuwahada na kuwatia upofu watanzania wasiweze kutambua haki zao,....Maoni na mapendekezo yangu;.

Kwa vile CHADEMA imesha ingia mioyoni mwa wengi kwa sasa, Ndo chama pekee kitakacho kiondoa CCM madarakani kama tu itafanya mambo yafuatayo..

1. Kuondoa hofu waliyojengewa watanzania kuhusu Amani na utulivu.
2. Kutoa elimu ya uraia hasa vijijini ambako bado wanawaamini hawa wanyonyaji, na wafujaji wakubwa wa rasilimali za nchi yetu.
3 kuhakisha wanafika vijiji vyote vya Tanzania.
4. Kuwaeleza wanachi madhara makubwa endapo wataichagua CCM tena 2015.
5. Kutoa sumu zote za Udini, Ukabila na Ukanda zilizopandikizwa na CCM.

Njia ambazo zitumiwe ni.

1. Kuchapisha vitabu,vipeperushi vingi vinavyoelezea sera na mikakati ya CHADEMA
2. Kuwepo na Radio na Tv ya Chama. Na
3. Kuhakikisha makamanda wanasambazwa nchi nzima kwa ajili ya kueneza sera nyumba hadi nyumba (kama wafanyavya Mashahidi wa Yehova kueneza imani yao)......

Hitimisho.. UKOMBOZI HAUPATIKANI KILELEMAMA.
 
fukuza tuntemeke co.i.e juliana shoza,mtela mwampamba,habib mchange(hivi ni vidagaa),ukushavitimua unakuwa umetuma message kwa mfadhili wao(wote mnamjua)
 
1.Viongozi wa Kitaifa wawe representative wawakilishe nchi nzima watoke mikoa yote
2.Katika chaguzi mbalimbali wakwepe kuonekana kuwa wanachaguana au kuteuana kikabila mfano wachaga kuwa sehemu kubwa ya uongozi wa chama katika maeneo mbalimbali ya nchi iwe ni Arusha ,Morogoro, Dar, Tanga, Mwanza n.k (ni mfano tu)
3.Watoe nafasi kwa watu wengine ambao pia wanaonekana kukubalika katika jamii, mfano Zito Kabwe kukataliwa kushika nafasi za juu za uongozi wa chama ilipunguza kura za chama "for sure 2010 Chadema ilikuwa inachukua nchi" . inapoonekana mnapigana vita ndani ya chama inapunguza mvuto kwa wananchi
 
Nimefurahishwa sana kwa namna CHADEMA walivyofanyia kazi baadhi ya mapendekezo yaliyopendekezwa katika thread hii. Ninaamin mengi mazuri bado yanakuja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom