Kuna ambao wanaridhika na CDM kama chama cha upinzani;
wakikosoa utawala wa CCM, wakikosoa watawala wa CCM na wakitoa ushauri mbalimbali kwa serikali na hawa hufurahia na kuridhika pale ambapo serikali inapochukua mapendekezo ya CDM. Je inatosha kuwa chama cha upinzani chenye kukosoa na kushauri serikali na taasisi zake? Je inatosha kwa viongozi wa upinzani kukosoa wale wa CCM na kuisaidia serikali itawale?
Niliwahi kuandika huko nyuma mada ya kwamba jukumu la chama cha upinzani siyo kusaidia serikali kutawala bali ni kuhakikisha wanaiangusha serikali iliyoko madarakani ili wao wapate nafasi ya kuingia kwenye uongozi huo na kutekeleza sera zao.
Mada hiyo ya Aprili 2011 inaeleza kwa kina kuwa siyo jukumu la CDM kuikosoa serikali ili itawale vizuri. Lengo lolote la kukosoa serikali ni kuidhoofisha ili hatimaye ianguke (collapse) au wananchi waikatae kwenye uchaguzi mkuu.