Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,228
- 44,409
Ili kiweze kuja kushika madaraka ya utawala wa nchi yetu na hatimaye kuliongoza taifa CDM inahitaji kuaminiwa na wananchi wengi zaidi na zaidi ya kuaminiwa inahitaji kukubaliwa kuwa ni chama cha kisiasa ambacho kinaweza kuwa mbadala wa CCM na hivyo kuweza kushika hatamu ya uongozi wa taifa.
Kuanzia kuanzishwa kwake hadi leo hii miaka ishirini imepita na sasa CDM kina uzoefu mkubwa kuliko ule uliokuwepo wakati TANU inashika uongozi wa nchi. Ikumbukwe TANU kama chama cha kisiasa kiliundwa rasmi mwaka 1954 na miaka saba baadaye kilikabidhiwa nchi. Kimsingi TANU ukilinganisha na CDM kilikuwa na changamoto kubwa zaidi kuliko! Kuanzia utawala wa Kikoloni, ukoloni Afrika, ukosefu wa wasomi, miundo mbinu ya mwanzo wa karne ya ishirini n.k. Ni wazi basi kwa kila kipimo CDM leo kama vilivyo vyama vingine vikongwe vya upinzani nchini imefika mahali ambapo inaweza kupimwa ikapimika.
Wakati maelfu ya Watanzania wakizidi kujitokeza kukiunga mkono na kukiamini maelfu pia wapo ambao hawajakiamini na hawajakikubali. Wale wenye kukubali wanakubali kwa sababu nyingi kubwa yawezekana ikiwa ni imani iliyojengwa ya kuwa CDM imesimama kama chama cha upinzani ikifanya kazi yake kwa umashuhuri na hivyo kuonekana kuwa mwiba kwa watawala. Kuna ambao wanaridhika na CDM kama chama cha upinzani; wakikosoa utawala wa CCM, wakikosoa watawala wa CCM na wakitoa ushauri mbalimbali kwa serikali na hawa hufurahia na kuridhika pale ambapo serikali inapochukua mapendekezo ya CDM. Je inatosha kuwa chama cha upinzani chenye kukosoa na kushauri serikali na taasisi zake? Je inatosha kwa viongozi wa upinzani kukosoa wale wa CCM na kuisaidia serikali itawale?
Niliwahi kuandika huko nyuma mada ya kwamba jukumu la chama cha upinzani siyo kusaidia serikali kutawala bali ni kuhakikisha wanaiangusha serikali iliyoko madarakani ili wao wapate nafasi ya kuingia kwenye uongozi huo na kutekeleza sera zao. Mada hiyo ya Aprili 2011 inaeleza kwa kina kuwa siyo jukumu la CDM kuikosoa serikali ili itawale vizuri. Lengo lolote la kukosoa serikali ni kuidhoofisha ili hatimaye ianguke (collapse) au wananchi waikatae kwenye uchaguzi mkuu.
Wakati naendelea kufikiria maoni yangu mwenyewe kuhusu mwelekeo wa CDM kushika dola mwaka 2015 na changamoto zilizopo natoa nafasi kwa mjadala huru kwa wapenzi, mashabiki, wanachama wa CDM na wakosoaji wengine kujaribu kuanisha changamoto ambazo wanaziona zinaikabili CDM kuelekea kushika dola 2015 na hasa kuangalia zile changamoto ambazo zisiposhughulikiwa kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 zinaweza kuifanya CDM isifanye vizuri sana.
Katika kuangalia changamoto hizo nina presume kuwa watu wanakubaliana katika mengi mazuri ambayo yamekwisha fanya hadi hivi sasa na CDM.
Unaamini kuna changamoto kubwa zinaikabili CDM sasa hivi na ambazo zinaweza kuwa kizuizi kwa CDM hatimaye kuweza kushinda uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge, ule wa Serikali za Mitaa na hatimaye kuiondoa CCM madarakani?