Nooo haijalala kihivyo mkuu wangu!unarahisisha mno!!kama unategemea chama pinzani kukamata dola kirahisi hivyo utakuwa unakosea sana,japo hairidhishi sana lakini tukubali tu kuwa chadema inakimbia!japo spidi yake bado ni ndogo kuliko tulivyotegemea au kutaka ila lazima mbio tuziite mbio!!haina maana timu iliyoshinda kwa goli moja tuiite kuwa imelala,kwa kuwa tu tulitaka ishinde kwa goli nyingi zaidi,kingine ni kuelewa nafasi ya kila mwanachama,mpenzi,na kila mpenda mabadiliko kuchukua hatua stahili pale alipo au anapoweza kufikia,haina maana kuwa mwanachama huku unasubiria kiongozi wa chama kilekile aje kukubembeleza kukipigia kura chako!!badala ya wewe kuwaelimisha/kuwashawishi/na hata kuwaomba wale wa mrengo tofauti na wako wakuunge mkono kukiunga chama chako mkono!! Ila pia kweli kuna sehemu ambazo nguvu inahitajika zaidi,bahati mbaya sana si sehemu moja au mbili,bali sehemu nyingi tofauti,ambazo bado itakuwa ngumu kwa Dr slaa,Mbowe,Tlissu na wengine wachache wenye ushawishi mkubwa kupafikia na kuweza kutoa special assistance huko,kwa muda upi?kwa uwezo upi?kwa uchumi upi?hapo ndipo panapohitaji subira na umakini wa hali ya juu!!kuna sehemu ambazo chama kinaweza kushinda uchaguzi bila hata ya kutumia nguvu nyingi,ila inahitajika subira na umakini mkubwa kuzijenga sehemu kama hizo ambazo mwisho huitwa ngome ya chama fulani,kama lema aliweza kuwashawishi watu elfu,wewe hushindwi kuwapata watu kumi,anza sasa!!ingia kwenye mbio ili uweze kukosoa kile unachojua ugumu wake,badala ya kujaribu kuufyeka msitu huku ukiwa nyuma ya keyboard,ukinyanyua kichwa ndiyo unagundua kumbe ulikuwa unacheza game,kisha unadai umedhulumiwa heka kumi za msitu ulioufyeka kwenye computer yako,shtuka.