Kwanza nitambue mchango mzuri sana wa MCHAMBUZI, kwa kweli unastahili sifa na pongezi. unakaa na kufikiria sana kabla ya kwenda kwenye keyboard. huwa napenda kusoma michango yako ambayo inazama kwa kina. tatizo ni kwamba wengi wetu hatupendi vitu vinavyozama. tunapenda vitu vya kiudaku udaku hivi! lakini pia niseme katika hilo kwamba wako wengi tu hapa JF ambao wanazama na kuchambua mambo kwa kina.
Pili nimpongeze aliyeleta mada hii, MM. heshima kubwa mzee.
Nitachangia katika maeneo mawili: Kwa Watanzania wote, na pili kwa CHADEMA. Nianze na yale ambayo nadhani ni muhimu sisi sote Watanzania, tukiongozwa na hali yetu ya Utaifa, Uzalendo, Utanzania, tunatakiwa kufanya. Pamoja na mengi ambayo uongozi thabiti wa chama kama CHADEMA unaweza kufanya, naamini kwamba viongozi hao watakuwa bora zaidi pale tu watakapopata changamoto njema na yenye afya kutoka kwa wingi wa Watanzania. ni watanzania wenyewe, hasa walio na uchungu kwamba mambo hayaendi sawa katika nchi yetu, hao ndio wanaweza kuielekeza CHADEMA na kuiwezesha ifanye kile kinachotakiwa. tunaweza kufanya haya siyo hasa kwa kununua kadi, ambalo nalo ni jambo jema tu, lakini nazungumzia hapa kufanya kazi za kujitolea kujenga chama. kila mtu katika kada yake na uzoefu wake na ujuzi wake anaweza kuangalia anawezaje kuchangia mabadiliko? wataalamu wa IT wanaweza kusaidia katika kufuatilia taarifa, maoni, na mambo yanayojitokeza na yenye umuhimu kwa chama, na kuyawasilisha kwa uongozi. Haya tunayojadili hapa ni mojawapo ya ushiriki, lakini unahitajika uwe mpana zaidi. Tusione kwamba kuna wenye chama ambao ni CHADEMA, na sisi ni watu tofauti. yetu macho! tunasubiri wakosee tuwaseme. Nadhani CHADEMA inahitaji sana ushiriki mpana wa watanzania ili kuwawezesha kuwa chama bora zaidi. Na hasa kama kuna uwezekano mkubwa wa CHADEMA kuwa mshindi katika sanduku la kura hapo 2015. Jinsi uwezekano huu unavyozidi kuwa mkubwa, ndivyo wale ambao kazi yao ni kutafuta tiketi ya kupata mafanikio binafsi na jamaa zao, watakavyojazana katika chama ili wajipange kuendeleza ulaji chini ya chama kipya. Business as usual! Tunaweza kukabili hali kama hii kwa wale wenye nia njema kushiriki kwa vitendo na kuacha kuwa watazamaji.
Pili, kwa CHADEMA, nikirejea mchango wa MCHAMBUZI kuhusiana na itikadi. suala la Itikadi ni muhimu sana kwa sababu linatoa mwanga wa mwelekeo wa chama katika kutekeleza kazi zake. lakini hapa nadhani tunahitaji kuwa na sehemu mbili tofauti. Itikadi ya chama na mwelekeo wa taifa. Chama cha TANU na baadae CCM, kilkuwa na itikadi yake. baadae CCM wameacha itikadi iliyoelezwa vizuri katika Azimio la Arusha, wakaingia katika itikadi ya siri lakini ambayo kutokana na tunayoyaona, ni aina ya uliberali ambao naomba niuite ULIBERALI KOKO. tumefika mahali tunahitaji kama taifa tuwe na mwelekeo. Kwa hali hiyo, pengine si jambo zuri sana kuachia mambo ya itikadi kwa chama. tukifanya hivyo tutaacha uwezekano wa chama kinachochukua madaraka kutuvuruga mno. tunahitaji kuamua ni mwelekeo gani tunautaka, kisha tujiimarishe hapo. itikadi za vyama zibakie ni kwa vipi watatufikisha tunapotaka kwenda kwa haraka, uhakika na gharama ndogo zaidi.