CHADEMA isijisalimishe kisiasa

CHADEMA isijisalimishe kisiasa

Nicolas J Clinton Gabone

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
897
Reaction score
559
CHADEMA ISIJISALIMISHE KISIASA, HISTORIA HAIANDIKWI KWA KUNYAMAZA

RAI YA,
Nicolas Jovin Clinton Gabone

Kwanza kabisa, historia ya mijadala ya maridhiano ya kisiasa hapa Nchini inahitaji kutazamwa upya. Je, maridhiano hayo yamewahi kuleta mabadiliko, au yamekuwa yakitumika kupunguza presha ya kisiasa bila kugusa kiini cha matatizo, huku Chama cha Mapinduzi kiki-buy time?

Kuanzia kipindi cha Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, viongozi wa upinzani walipoalikwa Ikulu ya Magogoni kwa mazungumzo, kulikuwa na matumaini ya kufungua ukurasa mpya wa siasa za majadiliano, ushindani na uwajibikaji. Hata hivyo, matokeo hayakuleta mabadiliko ya mfumo. Badala yake, ilionekana Chama tawala kuendelea kuvigawanya vyama vya upinzani na kuvivuruga kupitia ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, huku upinzani ukiendelea kukabiliana na changamoto zake bila uwanja sawa wa kufanya siasa Nchini.

Baadaye, katika awamu ya tano, kulionekana tena juhudi za mazungumzo baada ya viongozi wa CHADEMA kwenda Mwanza katika maadhimisho ya Uhuru kwa nia ya kujenga mazingira bora ya utawala wa sheria na uwajibikaji. Lakini nguvu ya kisiasa haikubadilika kwa kiwango kilichotarajiwa, kwani CCM iliendelea kuimarika huku upinzani ukiendelea kudhoofika katika mazingira ya ushindani finyu. Katika kipindi cha Rais John Magufuli, uongozi wake ulikuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi wengi wa kawaida, jambo lililobadili kabisa mazingira ya siasa za ndani. Baada ya kifo cha Rais Magufuli, Tanzania iliingia katika awamu nyingine ya matumaini ya maridhiano. Kukutana kwa viongozi wa CCM na upinzani, kulionekana kama fursa ya kujenga daraja jipya la siasa. Mimi nilipinga hadharani kwamba mpango ule ulikuwa danganya toto, kwani CCM haina nia ya dhati ya kuacha uwanja sawa na haki wa kufanya siasa, hususani kwa vyama vyenye nguvu na viongozi wenye ushawishi kwa umma.

Je, matunda ya maridhiano hayo yako wapi? Je, yalileta mageuzi ya msingi katika mfumo wa uchaguzi? Je, yalifungua njia ya Katiba mpya yenye kukidhi matarajio ya wananchi? Nchi haiwezi kuendelea kutegemea mazungumzo ya viongozi bila kushughulikia maswali ya kikatiba, kisheria, uwajibikaji wa taasisi, uhuru wa mifumo ya uchaguzi na usawa wa kisiasa.

Baadaye, suala la Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu na changamoto za kisheria alizokutana nazo ilizua tena mjadala kuhusu nafasi ya upinzani. Kwa mtazamo wangu, kinachozua mjadala siyo mtu binafsi, bali aina ya mfumo wa utawala unaoweza kuvumilia mawazo mbadala.
Wapo wanaoamini mchakato wa maridhiano umekuwa ukitoa muda zaidi kwa mfumo uliopo kuendelea bila mabadiliko ya msingi. Mimi mpaka leo naamini kwa muundo, imani na matendo ya CCM, haiko tayari kwa dhati kuachia mazingira ya haki ya siasa za ndani.

CHADEMA, isijisalimishe kisiasa, historia haiandikwi kwa kunyamaza

Mabadiliko makubwa yamezaliwa pale wananchi walipokataa kuzoea hali waliyoona siyo ya haki. Chama cha upinzani kinapoanza kuogopa kupaza sauti kwa kuhofia kuwakwaza walioko madarakani, kinakuwa kimeanza kujenga kaburi lake kisiasa. Upinzani hauanzishwi kuwa mapambo ya demokrasia, unaanzishwa kuhoji, kukosoa, kushinikiza uwajibikaji, kuonesha njia na kuwasemea wale ambao sauti zao hazisikiki.

Katika uwanja wa siasa, ukimya huonekana kama hekima, lakini unaweza kuwa kivuli cha kushindwa. CHADEMA haipaswi kuondoka kwenye msimamo wake wa sasa kwa sababu Chama cha siasa hakipimwi kwa namna kinavyowafurahisha wenye mamlaka, bali kwa namna kinavyowakilisha matarajio ya umma uliokiamini. Kwa sababu Chama cha siasa kinapopunguza nguvu yake ya kuhoji, kupinga na kushinikiza uwajibikaji na mabadiliko kinaanza kupoteza sababu yake ya msingi ya kuwepo.

Uzoefu wa Afrika Kusini unaonesha kuwa mfumo wa ubaguzi wa rangi haukuondoka kwa sababu watawala waliamua ghafla kuwa wema. Ulianza kusambaratika kwa sababu watu walikataa kukubali kwamba ubaguzi ulikuwa hali ya kudumu. Harakati hizo zilionesha kuwa nguvu ya kisiasa haipimwi kwa ukubwa wa silaha wala ofisi, bali kwa uwezo wa watu kusimama kwenye wanachokiamini.
Katika demokrasia iliyokomaa au mseto, upinzani haupaswi kuonekana kama adui wa serikali. Upinzani ni kioo kinachoonesha sehemu ambazo watawala hawawezi kuziona wakiwa ndani ya mfumo wa mamlaka. Serikali yenye nguvu haiogopi kukosolewa wala maswali magumu. Tanzania haiwezi kujengwa kwa makofi pekee, inajengwa kwa mijadala, tofauti ya mawazo na ushindani wa sera.

Kwa CHADEMA, huu ni wakati ambao historia inakiangalia. Wananchi hawahitaji Chama kinachosema kila kitu ambacho ni rahisi kusikia, wanahitaji Chama kinachoweza kusema ukweli hata pale ukweli huo unapokuwa mgumu. Kwa upande wa CCM, Chama kinachotawala kina jukumu kubwa zaidi. Ukuu wa Chama haupaswi kupimwa kwa muda wa kukaa madarakani, bali kwa uwezo wake wa kuvumilia ushindani na kujibu changamoto kwa hoja. Demokrasia yenye afya haihitaji upande mmoja kuwa dhaifu, inahitaji pande zote kuwa na uwezo wa kushindana kwa hoja na sera.

CHADEMA haipaswi kuacha nafasi yake ya kisiasa kwa sababu ya hofu, shinikizo au ushauri unaoweza kuifanya ipoteze utambulisho wake, bali inaitaji mabadiliko ya kimkakati kulingana na mazingira ya siasa za ndani. Mabadiliko hayo hayamaanishi kuacha misingi ya amani, sheria na demokrasia. Ushindi wa kweli wa kisiasa haupatikani kwa ulegevu, bali kwa kujenga hoja zenye nguvu na kuonesha uwezo wa kuongoza.
 
ok.:KKonaW:
 
Hakika maridhiano huwa ni hadaa za watawala kuwadanganya wapinzani na wapewe vyeo vya uongo na kweli watulie siasa zipoe tazama enzi za Cuf kule Zanzibar baada ya kufa kule wameingia ACT mambo yaleyale kugawana madaraka hakuna la maana hivyo uzoefu unaonyesha ni utapeli tu mwingine wa CCM. Hivyo CDM wako sahihi kwa uzoefu wa huko nyuma kuna vya msingi vya kufanya ambavyo CCM walifanya ulaghai hawakutekeleza kwa ukaidi wao lakini tumeona tulipofika
 
Chadema haiwezi kufanya huo ujinga.
 
Katika mtego ambao cdm hawapaswi kuuvaa sasa ni hicho kiitwacho maridhiano. Bora wabaki peke yao kuliko kuwa kwenye wingi wa hadaa.
 
Back
Top Bottom