Ukweli unabakia pale oale kuwa jamii inayo haki ya kuangalia kama kuna connection kati ya Kubenea na Lowasa au la?
Tulishawahi kujiuliza humu ndani why kila kukicha magazeti ya Mengi ndio yako frontline kumuandika Mkapa ktk kila negative angle wanayodhani itawafaa, baadhi walitoa majibu na wengine bado walibisha kwa kejeli au kupuuziakabisa.
Lowassa kama mwanasiasa wa juu kabisa ktk jamii yetu achilia mbali madhira ya kisiasa aliyokutana nayo, kwa msingi huu anabaki kuwa ni sehemu ya muhimu kwa jamii yetu.
Mleta hoja anachojaribu ni kutupatia fursa wana JF kuangalia upande wa pili wa shilingi, waswahili wana kamsemo ka shari hivi" Nyundo iligongwa kabla ya kugonga"
Twende chini na tuangalie mzizi wa habari hizi maalum za Lowasa ktk kila front page ya Mwanahalisi takriban 90% tangu kuanzishwa kwa gazeti hili.
Tufungue milango ya kukubali kutofautiana kwa hoja na pengine kutokukubaliana waungwana.
Nampongeza mtoa hoja na wakati sasa wa kuangalia connection kati ya Lowasa na Kubenea, niwakumbushe tu kuwa Saed Kubenea alianza kung'ara ktk media zetu kwa kasi kuanzia February 2005 pale CCM waliposema sasa ruksa kwenda front kwa wagombea.
Baada ya ushindi wa kambi ya JK chini ya ukamanda wa Edward ndipo hapo Kubenea alianza kurusha live mitizamo yake dhidi ya wana mtandao na taratibu akaanza kuifikia target yake Edward Ngoyai Lowasa.
Jamvi hili lijitupe ndani na kutufumbua macho juu ya hawa mahasimu wawili kwa faida ya umma na kumhukumu mtoa hoja na wachangiaji wanaomuunga mkono,
He was our pm, still is our leader and people do have some respect for him.
Twende kazini wakuu
FDR Jr, sidhani kama unakosea sana, ila ninachokiona kwako ni unapotosha kwa makusudi kwa hiyo hujakosea katika jitahada zako za kupotosha. Namkumbuka Lipumba wakati wa kampeni za mwaka 2000 alikua anasema hawezi kumuita Rais Mkapa mwongo, lakini alisema Mkapa hasemi kweli. Na wewe sasa naona hujakosea kwani umepatia kupotosha ambalo ndio lengo.
Ukweli unabakia pale oale kuwa jamii inayo haki ya kuangalia kama kuna connection kati ya Kubenea na Lowasa au la?
Anza wewe utupe hiyo connection, labda Lowassa alimchukulia mwanamke Kubenea maana walianza kusema waliommwagia acid waligombea mwanamke.
Tulishawahi kujiuliza humu ndani why kila kukicha magazeti ya Mengi ndio yako frontline kumuandika Mkapa ktk kila negative angle wanayodhani itawafaa, baadhi walitoa majibu na wengine bado walibisha kwa kejeli au kupuuziakabisa.
Hakuna magazeti yanayotwa 'ya mengi' kuna Nipashe, Thisday, Guardian, Kulikoni, Acha Umbeya na kadhalika.
Lakini suala la Mkapa halina tofauti na Lowassa. Mbona ZOmbe anaandikwa? Mbona Kasusura aliandikwa? Ninachotaka kukwambia ni kwamba suala si Mkapa wala Lowassa, hoja ni kwamba hawajaiba? Si mafisadi? Leta habari hapa ambayo Mkapa ama Lowassa kasingiziwa na haina ushahidi watu wajadili si kusema tu juu juu kwamba wanaandikwa sana. Kiwira Mkapa hakuhusika? NBC haijauzwa na Mkapa? Mtoto wa mke wake aliyezaa na Mramba (Peter Maro) hajakabidhiwa nyumba za TTCL aziuze na nusu hajamuuzia mama yake? kwa uchache tu. Lowassa hajahusika na Richmond? Lowassa hajahusika na jengo la UVCCM? Nagu, Lukuvi, Masilingi hawajamkana? Mbona wao hawajafukuzwa kama Nape? Sasa wanaondika au kusema ndio wanaokosea na wanaoiba au kuhujumu ndio washangiliwe?
Lowassa kama mwanasiasa wa juu kabisa ktk jamii yetu achilia mbali madhira ya kisiasa aliyokutana nayo, kwa msingi huu anabaki kuwa ni sehemu ya muhimu kwa jamii yetu.
Ni kweli ndio maana lazima ajadiliwe kwa maovu yake na kama akijenga shule kule Monduli ni wajibu wake, kwa tafsiri ya habari si habari ni sawa na mbwa kumng'ata mtu. Itakua habari ikiwa mtu atamng'ata mbwa.
Mleta hoja anachojaribu ni kutupatia fursa wana JF kuangalia upande wa pili wa shilingi, waswahili wana kamsemo ka shari hivi" Nyundo iligongwa kabla ya kugonga"
Hapo umepatia lakini njoo na HOJA ama jadili habari na gazeti husika si Kubenea, Mengi na Lowassa au Mkapa.
Twende chini na tuangalie mzizi wa habari hizi maalum za Lowasa ktk kila front page ya Mwanahalisi takriban 90% tangu kuanzishwa kwa gazeti hili.
Si kweli, kumekua na habari za watu wengi akiwamo Rostam, Jeetu Patel, Hosea, Karamagi, Msabaha na kadhalika na matokeo yake umeyaona kwa kamati ya Mwakyembe kupata nguvu na yeye kumwagiwa acid.
Tufungue milango ya kukubali kutofautiana kwa hoja na pengine kutokukubaliana waungwana.
Nakubaliana na wewe kwa HOJA na habari husika
Nampongeza mtoa hoja na wakati sasa wa kuangalia connection kati ya Lowasa na Kubenea, niwakumbushe tu kuwa Saed Kubenea alianza kung'ara ktk media zetu kwa kasi kuanzia February 2005 pale CCM waliposema sasa ruksa kwenda front kwa wagombea.
Si kweli, Kubenea ameanza kung'ara baada ya kumwagiwa acid na gazeti lilianza kupanda chati baada ya uchaguzi 2005 na si kabla yaani feb, 2005.
Baada ya ushindi wa kambi ya JK chini ya ukamanda wa Edward ndipo hapo Kubenea alianza kurusha live mitizamo yake dhidi ya wana mtandao na taratibu akaanza kuifikia target yake Edward Ngoyai Lowasa.
Jamvi hili lijitupe ndani na kutufumbua macho juu ya hawa mahasimu wawili kwa faida ya umma na kumhukumu mtoa hoja na wachangiaji wanaomuunga mkono,
He was our pm, still is our leader and people do have some respect for him.
Hapa umeshindwa kujificha kwa kumuita Lowassa kamanda na kwa kweli kwa kusema Lowassa na Kubenea ni MAHASIMU WAWILI. Hapo umejivua nguo