KUBENEA Vs LOWASSA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KUBENEA Vs LOWASSA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntaramuka, Sep 9, 2008.

 1. Ntaramuka

  Ntaramuka Senior Member

  #1
  Sep 9, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Binafsi ninamheshimu sana Said Kubenea kwani ni miongoni mwa waandishi wenye misimamo hasa kwa yale wanayoamini kuwa ni kweli, lakini wasiwasi wangu unakuja baada ya kusoma makala zake nyingi nimegundua zinamhusu Lowassa, kitu kilichonifanya nidhani kuwa kuna tatizo kati ya wawili hawa na si ufisadi kama anavyochukulia Kubenea kama mwanvuli.

  Maana kila toleo, tena kwenye ''front page'', utakuta mara Lowasa hivi, mara Lowasa vile, ilimradi tu amseme Lowasa.

  Sio kama ninamsemea Lowasa, hapana. Ila tu kama kweli Kubenea unania ya dhati ya kupambana na ufisadi, basi sema juu ya ufisadi na sio Lowasa tu kila siku, mbona kuna mafisadi wengi tu nji hii.

  Leo ni Jumanne, kesho Mwanahalisi litakuwa mtaani, habari kuhusu Lowassa ninatarajia kuikuta tena kwenye front page.

  Hata watu wa haki za bina damu wanasema "hate the the vice and not the person".

  Nakushauri bwana Kubenea utafute namna nyingine ya kukemea ufisadi la sivyo watu wataanza kupoteza imani na wewe.
   
 2. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Ndugu,

  Nasikitika kukuambia kuwa hujui unachosema; unaacha kujadili issue ya Msingi kuwa Lowassa ni fisadi unataka tumjadili Kubenea.

  Iwapo Lowassa ni fisadi na gateti la Kubenea limadhamiria kupiga vita ufisadi kuna ubaya gani wakimuandika fisadi Lowassa na ufisadi wake kwenye kila toleo?
   
 3. C

  Chuma JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Awaguse wote....!!!
   
 4. I

  Iga Senior Member

  #4
  Sep 9, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TUSISHANGAE kuona baadhi ya viongozi wetu wakiugua maradhi ya ajabu ajabu katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

  Huu utakuwa ni ujumbe kuwa jamaa hawa wanatuongoza ndivyo isivyo. Na wamesahau kuwa sehemu kubwa ya viongozi itakwenda motoni kwa kukosa kumwogopa Mumba, uadilifu, rushwa, dhuluma, kutaka uongozi wakati hawauwezi na ni wababishaji, na kujilimbikizia mali wakati watu wao wanakufa kwa uhitaji, njaa na magonjwa ya kila aina.
   
 5. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2008
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haya ni mawazo ya kifisadi nayo! Yaani Kubenea kuconcentrate na Lowasa ni tatizo!!!!! Kubenea kama anayoandika kuhusu Lowasa ni ya kweli mwache aendelee kuandika mpaka lowasa asuffocate au ayeyuke kabisa!! Maana hatuwezi kuwa tunashika habari hii kesho ile, si mafisadi watapumua sana! Kila mtu ashike mraba wake ikiwezekana. Kubenea na mraba wa lowasa wengine na wa EPA wengine wa vijisent, kiwira nk! Na wewe mtoa maada shika mraba wako mpaka tuuone ukiisha, sio kuanza tu halafu unaachia njiani!
   
 6. C

  Cool Girl Member

  #6
  Sep 9, 2008
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata mimi inanikera ,fisadi ni lowasa peke yake?kubenea sema ulilonalo moyoni kila siku lowasa tulio wengi tumechoka na nyinyi waandishi mmezidi kopotosha umma wa watanzania!
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  UKITAKA KUMPIGA NYOKA ANZA KICHWA KWANZA. LOWASSA ni kichwa cha ufisadi Tanzania. MENGINE NI BLAH BLAH.

  Hata magazeti yote yakiandika kila siku, habari za ufisadi wa Lowassa hazitakwisha maana hata leo kuna ufisadi mwingine unafanyika, ndio maana wakati kina mwanyika wanaanza kuchunguza EPA, kina Lukanza na wenzake walikuwa wanachoma nyama kule Monduli na walichangia katika harambee hadharani pale Arusha. Kumbukeni.

  Suala la Nape ni ufisadi mwingine wa Lowassa ambao uko katika chati, sasa unategemea nini? Gazeti linalotaka kuandika ukweli kuhusu ufisadi haliwezi kumkwepa Lowassa hata kwa mawe.

  Kama una uhusiano na Lowassa, nenda kamsalimie binti kutoka Handeni anayeitwa Mwajabu Ibrahim, anayefanya kazi nyumbani kwake na ambaye alipojiuzulu 'aka-mjiuzulisha' mtoto wa watu ili ahame naye. Mwambie akupa kadi zake za benki ukaone ana fedha kiasi gani ukilinganisha na za kwako unayehangaika na kazi usiku na mchana. Hiyo ni ili mujue tunajua mengi.
   
 8. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  You cant really separate the two.Vice has no brain or bank account for that matter...
   
 9. C

  Cool Girl Member

  #9
  Sep 9, 2008
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  suala sio kuwa kumfahamu,mafisadi wengiiiiiiiiiiiiiiiiiii jamani eeeeeeeeeeeeeeeeeeehh,lowasa lowasa lowasa lowasa,mafisadi wengine wanarelax kwa kuona hawaguswi na kubenea,na bado wanaendeleza umaaluni wao kwa kuona kwamba anasemwa ni mmoja!kama kweli kubenea anapiga vita ufisadi awaseme wote!
   
 10. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
   
 11. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Wale wale! Nani asiyejua kuwa mafisadi wanatumia pesa waliyotuibia kujisafisha? ni pale watakapopigwa mawe na wananchi wenye hasira kali hadi waikimbie nchi.
   
 12. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Safi sana Halisi na wote mnaomuunga Kubenea mkono. Habari za Lowasa zime dominate media kwa kuwa kila kitu anachofanya private na official ni cha Kifisadi. Hakuna fisadi kama Lowasa Tanzania nzima, RA ni cha mtoto. RA is the best friend of EL ili tu kupata mipitishio ya mipango yake. He is clever kuwa karibu na political shots. Hata mpaka niingie kaburini hakuna wa kunishawishi kuhusu ufisadi wa Lowasa. Naona tena mnataka kuzua uzushi kwa Kubenea kama yale ya Aziz Mongi kumfungia Kubenea kisa deni la 50,000 na kumtangaza ndani ya jamvi hili. Jamani heshimuni hili jamnvi ni takatifu si la wazushi na la vibaraka wa mafisadi.

  Lowasa anatumia mbinu zote kutaka kumaliza uhuru wa vyombo vya habari. Anatamani avinunue vyote kama RA basi tu plan hizo in vain. Kweli nimeamini humu jamvini kuna sisi tunaopinga mafisadi na wengine wanatubeza.

  Marekani kama kweli watafungia mafisadi kwenda kwao basi waanze na Lowasa. Big up Kubenea, cheers dedicated JF members and guests. Shame to Fisadi's na vibaraka wao.
   
 13. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kubenea ,hawa ni miongoni mwa wale ambao wamekuwa wakikutumia sms za vitisho kila kukicha, usiogope maana ulizaliwa siku moja na utakufa siku moja.

  Lowassa anatumia mbinu ya kupre empty gazeti la kesho na haswa akijua fika kuwa tayari mapambano yake na NNAPE yamechukua sura mpya hivyo anaamua kuhakikisha kuwa gazeti la kesho haliendi front na story yake ili kuwafanya wajumbe wa NEC kufanya maamuzi mazito.

  Hajui kuwa gazeti tayari linakaribia kumaliza kazi yake ya kuuweka ukweli hadharani ,na mpaka sasa mbona hajaenda mahakani kama alivyoahidi siku moja akiwa amejifanya kakasirika sana ?

  Lowassa , siku za ufalme wako zinahesabika na haswa kipindi hiki unapoamua kuwahonga watu na haswa Mchungaji mmoja mwanasiasa aliyepewa milioni 50 akiwa hotel moja jijini DSM juzi , na alikabidhiwa advance na Makamba kuwa akianza kumshughulikia Mbowe atapewa zote, na kesho kaitisha mkutano na waandishi wa habari pale hotel ya Travetine.

  Lowassa , pesa hizi zitawatokea puani kwani lengo la kutaka kusema eti Mbowe alipoenda kusoma aliona kuwa ufisadi wa EPA unaanikwa na hivyo ilikuwa mbinu ya kukimbia nchi kitu ambacho kesho kitasemwa na mchunga kondoo huyu asiyekuwa na haya wala aibu, kwanza aulizwe amemaliza kulipa alichokiita deni la Rostam Aziz? huku zikiwa ni fedha kwa ajili ya kulishitaki mwanahalisi?

  Mapambano haya yataendelea , kwani nchi hii itayumba kama watu wema tukiendelea kukaa kimya kwa hofu ya kupoteza vyeo vyetu na masilahi yetu.

  Kubenea songa mbele daima tupo nyuma yako.
   
 14. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Halisi ,sasa umeamua kuweka ukweli hadharani kuhusiana na Mwajabu, kwani hata miye nimesikia habari zake na ana tuaccount tuko pale Barclays, na benki nyingine huku akijuzungusha jijini na rav4,benz na vitara moja nyeusi , kumekucha jijini.
   
 15. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
   
 16. Ntaramuka

  Ntaramuka Senior Member

  #16
  Sep 9, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Siamini kama mapambano haya tuliyonayo leo dhidi ya ufisadi yatafanikiwa iwapo tutaendelea na mbinu za sampuli hii.

  Vita dhidi ya ufisadi haiwezi kufanikiwa kwa kumnyoshea kidole mtu mmoja(fisadi mmoja) , wala kikundi fulani tu cha mafisadi, ni lazima ziwepo juhudi za makusudi kabisa kukemea UFISADI popote unapofanyika. Kwenye hiyimisho la MARANYA hapo juu anasema HAKUNA KUWAPA MAFISADI NAFASI YA KUPUMUA. Lakini kwa staili hii TUNAWAPA nafasi ya kupumua kwa sababu tuna concetrate kwa fisadi mmoja tu huku tukiwaacha mafisadi kibao wakipumua tena kwa raha mstarehe huku wakiendeleza ufisadi kwa KASI, NGUVU na ARI kubwa sana.

  Hata katika mchezo wa mpiara, tazama jinsi timu pinzani inavyofungwa kirahisi kwa sababu tu wachezaji wanaconcetrate kumkaba mchezaji mmoja tu ambaye wao wanadhani ndiye mkali wa timu. TAIFA STARS ilipocheza na SENEGAL wengi tuliamini mchezaji hatari alikuwa AL-HAJI DIOUF na wengine wenye majina makubwa hivyo kuwakaba zaidi wao lakini kumbe kuna akina MAMADOU NIANG.

  Kukoncetrate kwa Lowassa kama sio deep thinker hauwezi kuona madhara yake. Akina ROSTAM, NCHIMBI, D. YONA nk. wanapumua vizuri sana na wanafanya ufisadi mkubwa tu.

  Ninaendelea kusisitiza TUPIGE VITA UFISADI NA MAFISADI WOTE, LOWASSA NI FISADI LAKINI UFISADI SIO LOWASSA.
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  tena toka ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho, labda ataona aibu na kuacha
   
 18. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2008
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Wapiganaji wenzetu, Mbona mnatubania?? Ikoje hii ya Mwajabu?? Wengine ndio tunaisikia leo pengine kutokana na Our Ears Not being On The Ground Deep Enough!! Tujuzeni Tafadhali.
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh inaingia akilini sasa atakaye sema kesho ni mchungaji MTIKILA........
  Kweli Mtikila ana njaa tayari kesha nunuliwa tena kumshambulia Mbowe...hii aibu sana.
  Hawa Mafisadi wana watu wao wamo humu wanachungulia mijadala humu kisha wanapeleka data kwa wakuu wao wanao walipa....kitaeleweka tu.
   
 20. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #20
  Sep 9, 2008
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ninyi ndiyo mnataka kupotosha uma wa watanzania wala sio kubenea.Maana matatizo yaliyopo sasa hivi mnataka tuyazungumze lini?
  Ninampa moyo KUBENEA aendelee tu kwani watanzania tunaoipenda nchi yetu tuko pamoja nae na tunapambana na ufisadi kwa sehemu yetu nae aendelee kwa sehemu yake.
  Ninyi mnopinga vita hivi inaonyesha mko upande ulioshika mpini ndiyo maana mnatoa mawazo mgando.Tunajua hii ni dawa chungu ndiyo maana imeanza kuwapa shida lakini tutaendelea mpaka mtaacha ufisadi.
  Hata fisadi ana watoto,mke,jamaa,ndugu,marafiki na wote hawa wanafaidika na ufisadi wake. Hivyo tunategemea kupata criticism kutoka kwake na hao wanofaidika na ufisadi wake.
  Mungu Ibariki Tanzania
   
Loading...