KUBENEA Vs LOWASSA

KUBENEA Vs LOWASSA

Binafsi ninamheshimu sana Said Kubenea kwani ni miongoni mwa waandishi wenye misimamo hasa kwa yale wanayoamini kuwa ni kweli, lakini wasiwasi wangu unakuja baada ya kusoma makala zake nyingi nimegundua zinamhusu Lowassa, kitu kilichonifanya nidhani kuwa kuna tatizo kati ya wawili hawa na si ufisadi kama anavyochukulia Kubenea kama mwanvuli.

Maana kila toleo, tena kwenye ''front page'', utakuta mara Lowasa hivi, mara Lowasa vile, ilimradi tu amseme Lowasa.

Sio kama ninamsemea Lowasa, hapana. Ila tu kama kweli Kubenea unania ya dhati ya kupambana na ufisadi, basi sema juu ya ufisadi na sio Lowasa tu kila siku, mbona kuna mafisadi wengi tu nji hii.

Leo ni Jumanne, kesho Mwanahalisi litakuwa mtaani, habari kuhusu Lowassa ninatarajia kuikuta tena kwenye front page.

Hata watu wa haki za bina damu wanasema "hate the the vice and not the person".

Nakushauri bwana Kubenea utafute namna nyingine ya kukemea ufisadi la sivyo watu wataanza kupoteza imani na wewe.

Kuna usemi wa kiswahili "pilipili iliyo shambani inakuwashia nini" Sioni mantiki ya wewe kulete hii topic ilhal unajua kuwa hivi sasa ule mkataba "mbovu" kupita jote wa ujenzi wa jengo la UVCCM ndio unajadiliwa kwenye vikao vya CCM sasa unataka kutuambia Kubenea atakuwa amefanya dhambi kuipa "mshiko" story aliyoibua! Nina wasiwasi kuwa umetumwa! na sipendi kusema unamtetea Lowasa! kwani sio kweli! huyu ndie alpha na R.A ni Omega wa Richmond asiposakamwa Lowasa asakamwe nani? katibu kata anaekula rushwa ya elfu 10? Be analitical plz.

Kubenea ndio alikuwa wa kwanza kuandika kwa kina kuhusu ufisadi wa UVCCM baada ya kuibuliwa na mhe Nape Nnauye kwahiyo anahaki ya kufanyia follow up mpaka atakapo ona mwisho wake! na wengi tunanunua nakala kujua inaendeleaje? si alitishia kushitaki?? nadhani hiyo ndio solution na sio kukutuma uje na mada inayochefua angalia wengine humu kwenye forum wana mimba changa usije kuwatapisha. "Kubena he is hunting what he can kill he cant hunt what he cant kill" unataka aandike ufisadi wa mtu asie kuwa na ushahidi nae? ili iweje? elewa yeye ni mwandishi na anawakilisha chombo cha habari na anapaswa kuandoka habari zenye ukweli na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na sio fununu na majungu ya vijiweni maana mengi yanasemwa kwenye vijiwe vyetu vya kahawa lakini havina uthibitisho. Waacheni waandishi wa play they are part jamani msiwasakame! na mkumbuke kumtetea fisadi ni ufisadi pia.
 
LOWASSA NI MWIZI, MLAFI: KWA NINI ASIANDIKWE HATA KAMA NI KILA SIKU?
Sokomoko umenikuna! Hawa mapandikizi ya akina Nchimbi, Rostam, Karamagi na Lowassa katika JF yanatia kichefuchefu. Baba zima lenye watoto linajitokeza kumtetea mwizi na kutaka kumkatisha tamaa mpambanaji Kubenea! Sababu kubwa? Kapewa pesa! Hizi pesa ndo zinawashikisha kuta hivi hivi! Lowassa si mtu wa kutetea, ni mwizi tena mwizi mzuri sana ambaye hapendi hata senti tano impite machoni bila kuikimbilia! Sasa mwizi wa aina hiyo asisemwe ? Kubenea endelea, endelea, endelea na msimamo wako. Hata MwanaHalisi ya kesho na kesho kutwa tunataka kujua fisadi Lowassa anasema nini! Usiwasikilize akina chakubimbi Ntaramuka. Hii ni vita ya kujikomboa sisi wanyonge! SONGA MBELE KUBENEA!
 
Binafsi ninamheshimu sana Said Kubenea kwani ni miongoni mwa waandishi wenye misimamo hasa kwa yale wanayoamini kuwa ni kweli, lakini wasiwasi wangu unakuja baada ya kusoma makala zake nyingi nimegundua zinamhusu Lowassa, kitu kilichonifanya nidhani kuwa kuna tatizo kati ya wawili hawa na si ufisadi kama anavyochukulia Kubenea kama mwanvuli.

Maana kila toleo, tena kwenye ''front page'', utakuta mara Lowasa hivi, mara Lowasa vile, ilimradi tu amseme Lowasa. Sio kama ninamsemea Lowasa, hapana. Ila tu kama kweli Kubenea unania ya dhati ya kupambana na ufisadi, basi sema juu ya ufisadi na sio Lowasa tu kila siku, mbona kuna mafisadi wengi tu nji hii.

Leo ni Jumanne, kesho Mwanahalisi litakuwa mtaani, habari kuhusu Lowassa ninatarajia kuikuta tena kwenye front page. Hata watu wa haki za bina damu wanasema "hate the the vice and not the person". Nakushauri bwana Kubenea utafute namna nyingine ya kukemea ufisadi la sivyo watu wataanza kupoteza imani na wewe.

Mkuu sana, wewe ni ndugu yetu sasa hatuwezi kukuacha uharibikiwe hivi hivi tunakuona, hao mafisadi Nchimbi na Lowassa, watakufikisha pabaya, kama walipomfikisha Rais wetu sasa hivi,

Ninaamini kuwa una akili nyingi sana, lakini ulikolalia kuna wengine wameamkia huko, mafisadi wana tabia moja in common huwa ni watumiaji wazuri sana wa wnaojipeleka kwao, tena kwa bila malipo wakati mwingine kunyamza ni busara pia kama huna hoja ya msingi hasa hapa JF,

Kwa sababu sio vigumu sana kujua nia na madhumuni yako na hii mada, mkamalizie ya Nape kwanza maana ya Kubenea yaliwashinda na tindikali zenu mlizonunua kwa mafisadi kama wenyewe, maana waliwauzia iliyo-expire, ndio maana Kubenea is still going strong.
 
Hakuna mwananchi aliyempa Kubenea dhamana yoyote kuhusiana na raslimali zetu, yeye ni mpiga kelele kama mimi na wewe. Sidhani kama mimi kichuguu nitakuwa na kosa lolote nikisema kuwa mtu fulani aliyepewa dhamana ya kueongoza nchi hii ni fisadi. Vile vile sidhani kama nitakuwa na kosa nikiendelea kusistiza kuwa jamaa huyo ni fisadi endapo nitaona kuwa hachukuliwi hatua zozote za kisheria. Kubenea siyo polisi wa nchi hii; yeye ni mtoa habari tu, na habari atakazotoa zinategemea na vyanzo vyake vya habari. Kama vyanzo vyake vingi viko kule alikokalia Lowasa, basi sioni ubaya kwake kuendelea kutupa habari hizo. Nina imani kuwa waandishi wengine watatupatia habari kutoka kona nyingine. Naona hapa ni kama Division of labour; yeye ana utaalamu wa kupata hjabari zihusuzo Lowasa, mwache afanye kazi yake, Shigongo ana utaalamu wa kupata habari za udaku na huwa anafanya hivyo. Tutakapopata mwenye utaalamu wa kutuletea habari za ndani za Kikwete tutampokea tu. Tusilaumu wajumbe
 
HUyu ni PAPA; lazima aanguke kwanza; maana mnaona anafurukuta kwa kutumia hela alizokwisha zivuna kwetu wananchi; so Kubenea shughulikia hiyo kitu mpaka iyeyuke kabisa ndio tuje kwa mafisadi wengine maana tukiruka ruka tutakosa mwelekeo; ningependa siku moja kesi ya fisadi inafika mahakamani; ukweli wa mafisadi wote ungejulikana; Lowasa alisema anaenda mahakamani; alikuwa anamtishia mtu kwa nyau?
Mafisadi wamo humu ndio wanaondika utetezi wa Ufisadi; kama habari inakukera usinagalie au ziba masikio wenzio tunafuatailia kwa karibu sana mambo haya ( sio mzalendo na huenda Dr Slaa hajaona jina lakko tu ungekuwa ktk List of Shame)
 
Binafsi ninamheshimu sana Said Kubenea kwani ni miongoni mwa waandishi wenye misimamo hasa kwa yale wanayoamini kuwa ni kweli, lakini wasiwasi wangu unakuja baada ya kusoma makala zake nyingi nimegundua zinamhusu Lowassa, kitu kilichonifanya nidhani kuwa kuna tatizo kati ya wawili hawa na si ufisadi kama anavyochukulia Kubenea kama mwanvuli.

Maana kila toleo, tena kwenye ''front page'', utakuta mara Lowasa hivi, mara Lowasa vile, ilimradi tu amseme Lowasa.

Sio kama ninamsemea Lowasa, hapana. Ila tu kama kweli Kubenea unania ya dhati ya kupambana na ufisadi, basi sema juu ya ufisadi na sio Lowasa tu kila siku, mbona kuna mafisadi wengi tu nji hii.

Leo ni Jumanne, kesho Mwanahalisi litakuwa mtaani, habari kuhusu Lowassa ninatarajia kuikuta tena kwenye front page.

Hata watu wa haki za bina damu wanasema "hate the the vice and not the person".

Nakushauri bwana Kubenea utafute namna nyingine ya kukemea ufisadi la sivyo watu wataanza kupoteza imani na wewe.

Nenda kaombe nafasi kwenye magazeti ya New Habari Corporation uandike humo. Usituletee masihara hapa tuko serious na mambo ya ufisadi ya maendeleo ya nchi yetu pamoja na vizaqzi vijavyo. Kubenea Mbeleeeee!!!!!!!
 
Binafsi ninamheshimu sana Said Kubenea kwani ni miongoni mwa waandishi wenye misimamo hasa kwa yale wanayoamini kuwa ni kweli, lakini wasiwasi wangu unakuja baada ya kusoma makala zake nyingi nimegundua zinamhusu Lowassa, kitu kilichonifanya nidhani kuwa kuna tatizo kati ya wawili hawa na si ufisadi kama anavyochukulia Kubenea kama mwanvuli.

Maana kila toleo, tena kwenye ''front page'', utakuta mara Lowasa hivi, mara Lowasa vile, ilimradi tu amseme Lowasa.

Sio kama ninamsemea Lowasa, hapana. Ila tu kama kweli Kubenea unania ya dhati ya kupambana na ufisadi, basi sema juu ya ufisadi na sio Lowasa tu kila siku, mbona kuna mafisadi wengi tu nji hii.

Leo ni Jumanne, kesho Mwanahalisi litakuwa mtaani, habari kuhusu Lowassa ninatarajia kuikuta tena kwenye front page.

Hata watu wa haki za bina damu wanasema "hate the the vice and not the person".

Nakushauri bwana Kubenea utafute namna nyingine ya kukemea ufisadi la sivyo watu wataanza kupoteza imani na wewe.

Mi naona sasa kama wewe ndio unachochea moto wa Lowassa kuandikwa zaidi.

Labda tungefanya kama poll hivi tujue magazeti yenye habari za Lowassa yanajilinganisha vipi na yale yenye habari nyingine,nina uhakika kabisa kuwa yenye habari za Lowassa yatauzika zaidi kuliko mengine.He has created a feeding frenzy!

Sasa labda kama unafahamiana na Mh Lowassa,ungemshauri siku nyingine asiache mambo yake wazi namna hio.Kwa sababu what we read abt him IS newsworthy.

Unasahau kuwa huyu ni PM aliyekaa muda mfupi sana kuliko wote na ni wa kwanza kujiuzulu kwa kashfa.sasa hata kama ni ratiba yake ya kwenda chooni,anachokula,watu anaowatembelea...wengi wangependa kujua yote hayo labda.Kujua ni mtu wa aina gani raisi wao aliwaletea.

Wewe angalia Uingereza wakimng'ang'ania mtu,kama wakati wa Princess Diana.Hata akienda gym wanae,kwa sababu wanajua waingereza wengi wana interest ya kujua yote hayo.

Na huyu bwana nae ndio hivohivyo,kajiletea balaa mwenyewe,and now we are feeding on it.....nobody is throwing up yet.
 
Nashukuru sana wakuu kwa jinsi mlivyojadili mada hii niliyowasilisha. Kikubwa nilichojifunza ni kuwa sote tunachukia ufisadi tena sana kwani kwani kuna baadhi wamechangia tena kwa jazba hii imenidhhirishia kuwa kweli yuko vitani. Ninawahakikishieni kuwa pamoja katika vita hivi dhidi ya ufisadi ila tu tulitofautiana kimtizamo juu ya namna ya kushughulikia ufisadi na mafisadi.

Mimi nilikuwa naamini kuwa vita dhidi ya ufisadi ni vita dhidi ya mafisadi WOTE KWA WAKATI MMOJA lakini nimejifunza kuwa ni lazima tuanze na VINARA wa ufisadi kwanza kwani mchangiaji mmoja amesema ukitaka kumuua nyoka mpige kichwani, na mwingine akasema kumshughulikia Lowasa kwanza ni sawa na kumuwinda Simba porini kwani yeye ndiye mfalme wa pori kama Lowassa alivyo mfalme wa mafisadi.

Lakini kupitia mjadala huu nimejifunza mengi sana.
Tuendelee kuchangia

Mumgu ibariki Tanzania
 
Ukisikia kuishiwa hoja ndio huku sasa, huwezi kuifanya hoja yako isimame mpaka uende personal? sasa niambie na wewe Kubenea au Nape ni nani kwako? wajombazo au wapwazo?

Kubenea na Nape wote ni wapiganaji wa Tanzania na wanapinga ufisadi, kwa jina lingine ni Wazalendo wenye nchi. Sina undugu wa damu nao bali nina undugu wa Kitaifa na kina Kube na Nape. Period. Sina undugu wa kitaifa na mafisadi na vibaraka wao.

Mimi ni kibaraka wa Wapiganaji wote wa Tanzania katika kukomboa hata kile kidogo kilichabaki kwa ajili ya kizazi cha Tanzania.

Siwezi kuishiwa hoja hata kidogo. Hata ukinipa siku nzima naweza kuchangia post zote humu ndani tena with evidences nikitaka. Ni kwa vile tu nabanwa na office outputs. Ukitaka retreave my postings uone zilivyo beba mantiki.
 
Hizi pesa ndo zinawashikisha kuta hivi hivi! Lowassa si mtu wa kutetea

Naona mkuu una jazba kweli na hawa vibaraka uchwala wenye njaa za mchwa kuja kuwatetea wezi wa TAIFA.
 
HALISI January 2005 mpaka June 2005 niambie Saed Kubenea alikuwa anashughulika na nini? Ni nani aliyeripoti kwenye media kuwa pale Chimwaga kuna Baba wa Taifa aliyekuwa akimwaga mapesa on behalfa of Mtandao?

HALISI Rejea hoja yangu niliyomuhoji Kubenea atueleze wana JF kama WALE WALIOPO KISUTU WAKITUHUMIWA KUMDHURU YEYE NDIO WATESI WAKE? jamvi liliipokea hoja lakini hatukupata picha nzuri na kesi iko mahakamani mpaka sasa.

HALISI Ni nani aliyelia 1995 baada ya JK kunyimwa ugombea wa? Ni nani aliyekuwa nyuma ya media ktk miaka 10 ya Mkapa kwa niaba ya JK? Ni nani asiyejua kuwa ujio wa JK Ikulu ni kivuli cha Edward ? Ni nani atakayemtenga Edward toka kwa JK kiubinadamu? Kwanini huyu Mheshimiwa Lowasa asiitwe ndie kamanda wa harakati za JK 90-2005.

HALISI Wewe na mimi tunafahamu kuwa UVCCM ya kaka yangu Guninita walimhitaji 1.SAS 2. Edward na 3.Jakaya mwaka 95, matokeo hayakuwa walivyopanga na wahanga mpango huo walikuwa ni Edward na Guninita ambaye aliamua kuiacha na CCM yenyewe

HALISI Umesoma Mwana-Halsi la leo? Aaah ofcoz unalo kabla hata halijatoka angalia nakala zako zote fanya hesabu ya primary utaona it is more than 90% niliyoisema.

HALISI Ni wajibu na haki kumheshimu yeyote yule anayewakilisha wananchi ktk mamlaka, si haki kuwaona watu wa Monduli kuwa si wazalendo au wendawazimu kwa kutomheshimu kiongozi waliyemchagua awawakilishe, ikiwa Mh.Pinda amebainisha kuwa Mh.Lowasa yeye amewajibika kisiasa sasa iweje huyu mtu asiheshimiwe japo kwa uamuzi huo na ni vipi tumheshimu Pinda ambaye ndiye mbainishaji?
HALISI Nasisitiza kumheshimu kiongozi yeyote ambaye ana ridhaa ya umma hata kama ameshutumiwa ktk shughuli zake na baadae kuwajibika, nitakuunga mkono ktk kumlaani na kumbeza kwa kila namna pale kiongozi yeyote ambaye ameaminiwa kimamlaka na umma kisha akatuhumiwa na ikathibitika mbele ya sheria kuwa amevunja sheria ya nchi na kuwajibishwa kisheria kwa adhabu na siyo vinginevyo.

HALISI Ili haki itendeke ni lazima kwetu sisi wana JF tujikite ktk kuchambua mambo ktk sura zote mbili za coin, tuelimishe, tujadili, tushutumu na tupongeze.

SAED KUBENEA NI MWANAHARAKATI ANAYETAKA TUAMINI KUWA YEYE ANAPIGANA NA VIONGOZI WASIOWAAMINIFU KWA TAIFA HILI
EDWARD NGOYAI LOWASA NI MWANASIASA ANAYETAKA TUAMINI KUWA YEYE NI KIONGOZI SAFI KWA MAENDELEO YA TAIFA HILI.

HALISI Rejea msimamo wangu kuwa kila mtu anayo haki ya kusikilizwa mbele ya sheria ili kuipatia fursa mamlaka ya kisheria kufanya maamuzi yasiyo na upendeleo kwa ANAYETUHUMU NA ANAYETUHUMIWA.

HALISI Wote hawa Kubenea na Lowasa wanayo haki ya kuitumia fursa hiyo baadala ya kutumia njia zisizo rasmi ktk kuwapa haki wananchi wote dhidi ya Wahujumu wa nchi yetu.

HALISI
 
Mkuu sana, wewe ni ndugu yetu sasa hatuwezi kukuacha uharibikiwe hivi hivi tunakuona, hao mafisadi Nchimbi na Lowassa, watakufikisha pabaya, kama walipomfikisha Rais wetu sasa hivi,

Ninaamini kuwa una akili nyingi sana, lakini ulikolalia kuna wengine wameamkia huko, mafisadi wana tabia moja in common huwa ni watumiaji wazuri sana wa wnaojipeleka kwao, tena kwa bila malipo wakati mwingine kunyamza ni busara pia kama huna hoja ya msingi hasa hapa JF,

Kwa sababu sio vigumu sana kujua nia na madhumuni yako na hii mada, mkamalizie ya Nape kwanza maana ya Kubenea yaliwashinda na tindikali zenu mlizonunua kwa mafisadi kama wenyewe, maana waliwauzia iliyo-expire, ndio maana Kubenea is still going strong.

Wanasema mtu mwenye hekima husikiliza sana na kuongea kidogo! Kuna watu wazima humu wanaongea pumba!hawana hoja ya msingi!inashtua kuona kuna watu wa aina hii na hatujui wapo wangapi na wanadhamira gani kwa Taifa letu!

Sidhani kama ni haki kumsakama Kubenea sidhani kama anatumia pesa za EPA au RICHMOND, Meremeta na Twin tower kuchapisha habari za mumsakama Lowasa. Nasema hivii Lowasa, Rostam, Nchimbi, Makala na Jakaya wana haki kusakamwa kwani wamejitakia wenyewe wangekuwa makini saa hiizi sote tungekuwa busy kujenga nchi tusingekuwa tunatetea mafisadi kwani time hiyo tusingekuwa nayo!

Enyi watumwa wa ufisadi eleweni wanajf ni watu waliomakinika wanauwezo wa kunusa kila aina ya makala inayojaribu kuwasafisha wanaonuka kwa ufisadi. Eleweni Watanzania wa sasa sio wale wa enzi za Tanu! Msiwadanganye wanaowatuma bora muwaeleze ukweli kuwa kazi ni kubwa kuliko wanavyothani! Sina uhakika kama mtaweza kutubadilisha mawazo siku moja tuamke tumsifu Lowasa, Rostam na JK kuwa wanajenga nchi! Sidhani kwani hawa watu wana mawaa na huju JK kajitakia mwenyewe! alikuwa hana haja kulipa fadhila kwani asingelipa ingekuwa nini?
 
Ndugu,

Nasikitika kukuambia kuwa hujui unachosema; unaacha kujadili issue ya Msingi kuwa Lowassa ni fisadi unataka tumjadili Kubenea.

Iwapo Lowassa ni fisadi na gateti la Kubenea limadhamiria kupiga vita ufisadi kuna ubaya gani wakimuandika fisadi Lowassa na ufisadi wake kwenye kila toleo?

Sio sawa! LAbda kama hujasoma habari zenyewe. Anarudia kile kile kila siku kama anamfundisha mtoto bwana! Mimi binafsi nimemshusha sana hadhi ndugu yangu Kubenea. Angeheshimika sana kama angesema mara moja mbili anaenda kwa mambo mengine alafu anakuja kukumbushia tena. Sidhani kama huo ndio uandishi....
 
......huo urefa wa wanahabari ulipewa na nani mwenzetu!!!........si uache kusoma maandiko yake..........kwani wewe ni nani hasa wa kumshushia mtu hadhi.........WHO CARES ABT MSONGORU KUMSHUSHIA HADHI WHOEVER.....na hivi kumshuhsia hadhi mtu ndio unafanya nini......kwa kuja hapa JF na kutuambia kuwa wewe unasoma habari zile zile kutoka kwa kubenea!!......acha hizo mazee

.......ni nani hasa anayejishusha hadhi.....yule anayeng'ang'ania kusoma kile kile ambacho anakidharau (which is you) au yule aliyeamua kwa dhati kupambana na FISADI kutumia kalamu yake!!.......
 
Oh! Niliandika bila kusoma maoni wa wengine. Naomba niseme hivi, sote tuna nia moja....Nadhani kuna wachache tu wenye nia mbaya na Taifa hili na haiyumkini tutwashinda. Ila jamani to be honest, kutoka kwenye mtima wa moyo wangu kabisa, uandishi wa jinsi hiyo sio wa karne ya sasa. Mimi naamini kubenea ana masikio na amesikia atajua yupi mwenye nia njema na yupi mwenye nia mbaya nae.

Narudia, hata kama wote tukaside kwa Kubea, ukweli utabaki palepale, SIO UANDISHI WA KISTAARABU.
 
Oh! Niliandika bila kusoma maoni wa wengine. Naomba niseme hivi, sote tuna nia moja....Nadhani kuna wachache tu wenye nia mbaya na Taifa hili na haiyumkini tutwashinda. Ila jamani to be honest, kutoka kwenye mtima wa moyo wangu kabisa, uandishi wa jinsi hiyo sio wa karne ya sasa. Mimi naamini kubenea ana masikio na amesikia atajua yupi mwenye nia njema na yupi mwenye nia mbaya nae.

Narudia, hata kama wote tukaside kwa Kubea, ukweli utabaki palepale, UANDISHI HUU SIO WA KITAALAM NA WA KISASA.
 
Binafsi ninamheshimu sana Said Kubenea kwani ni miongoni mwa waandishi wenye misimamo hasa kwa yale wanayoamini kuwa ni kweli, lakini wasiwasi wangu unakuja baada ya kusoma makala zake nyingi nimegundua zinamhusu Lowassa, kitu kilichonifanya nidhani kuwa kuna tatizo kati ya wawili hawa na si ufisadi kama anavyochukulia Kubenea kama mwanvuli.

Maana kila toleo, tena kwenye ''front page'', utakuta mara Lowasa hivi, mara Lowasa vile, ilimradi tu amseme Lowasa.

Sio kama ninamsemea Lowasa, hapana. Ila tu kama kweli Kubenea unania ya dhati ya kupambana na ufisadi, basi sema juu ya ufisadi na sio Lowasa tu kila siku, mbona kuna mafisadi wengi tu nji hii.

Leo ni Jumanne, kesho Mwanahalisi litakuwa mtaani, habari kuhusu Lowassa ninatarajia kuikuta tena kwenye front page.

Hata watu wa haki za bina damu wanasema "hate the the vice and not the person".

Nakushauri bwana Kubenea utafute namna nyingine ya kukemea ufisadi la sivyo watu wataanza kupoteza imani na wewe.

sina shaka!

sina shaka wewe ni mmoja wa watu walionunuliwa na mtandao wa mafisadi katika njia yao ya kujisafisha. wote tunafahamu kama wapo katika jitihada za kujisafisha mafisadi wakiongozwa na lowasa wapo katika jitihada za kujisafisha na tuhuma zao za kweli kupitia magazeti yanayoaminiwa na kuanzisha magazeti yao.

vile vile hata watu binafsi ambao wanazo nafasi hapo walipo ya kuongea na wakasikiwa na watu kama hapa JF pia mmenunuliwa, hivyo ndugu, tumekugundua kama unataka kumsafisha FISADI LOWASA, HAPA SIO MAHALA PAKE TUNA MAMBO MENGI YA KUYAJADILI.

ONGELEA VITU VITAKAVYOJENGA SIO KUMWONGELEA MWANDISHI ANAYEFICHUA MAOVU HATA KAMA NI YA MTU MMOJA KILA SIKU AS LONG AS NI UKWELI, MWACHE
 
Sio sawa! LAbda kama hujasoma habari zenyewe. Anarudia kile kile kila siku kama anamfundisha mtoto bwana! Mimi binafsi nimemshusha sana hadhi ndugu yangu Kubenea. Angeheshimika sana kama angesema mara moja mbili anaenda kwa mambo mengine alafu anakuja kukumbushia tena. Sidhani kama huo ndio uandishi....

Mzee hutendi haki hapo, Watz tunasahau kirahisi sana nampongeza sana Kubenea nadhani anatujua haswa tulivyo watz, nina mifano kwa hili ukilitaka nitakuambia na kukuthibitishia. Nilibahatika kuonana na huyu jamaa nilipokuwa Tz recently, hes simple n open minded, kwenye kujadili issue ni msikivu na anapenda kuchangia kidogo. Msonguru, tunahitaji akina Kubenea wengi na akina Balile wachache bwana,

Ushi
 
......huo urefa wa wanahabari ulipewa na nani mwenzetu!!!........si uache kusoma maandiko yake..........kwani wewe ni nani hasa wa kumshushia mtu hadhi.........WHO CARES ABT MSONGORU KUMSHUSHIA HADHI WHOEVER.....na hivi kumshuhsia hadhi mtu ndio unafanya nini......kwa kuja hapa JF na kutuambia kuwa wewe unasoma habari zile zile kutoka kwa kubenea!!......acha hizo mazee

.......ni nani hasa anayejishusha hadhi.....yule anayeng'ang'ania kusoma kile kile ambacho anakidharau (which is you) au yule aliyeamua kwa dhati kupambana na FISADI kutumia kalamu yake!!.......

NI UHURU WANGU WA MAONI TU LAKINI PIMA MWENYEWE KAMA NI SAWA KWENYE ULIMWENGU WA SASA KWA MATOLEO SITA KUWA exPM FRONT PAGE! TENA KWA KURUDIA RUDIA KILE KILE.
 
Mzee hutendi haki hapo, Watz tunasahau kirahisi sana nampongeza sana Kubenea nadhani anatujua haswa tulivyo watz, nina mifano kwa hili ukilitaka nitakuambia na kukuthibitishia. Nilibahatika kuonana na huyu jamaa nilipokuwa Tz recently, hes simple n open minded, kwenye kujadili issue ni msikivu na anapenda kuchangia kidogo. Msonguru, tunahitaji akina Kubenea wengi na akina Balile wachache bwana,

Ushi

Nashukuru Ushi kwa Lugha yako ya kistaarabu, nashukuru sana. Ila Sidhani kama umelisoma gazeti lenyewe kwa wiki zote hizo. Ni fedheha kwake yeye mwenyewe. Nasema nikiwa singamani na upande wa Lowasa hata Chembe.
 
Back
Top Bottom